MZEE MWENZANGU WALA KWA HILI SIOMBI MSAADA KWENYE TUTA WALA NINI... UMRI UMEKWENDA NAOGOPA KUVUNJA MGUU.

KWA WALE WANAOPITA MBELE YA LANGO KUU LA IKULU YETU WATAKUWA WAMEONA MABADILIKO YA HIVI KARIBUNI KUWA PAMEPANDWA MAJANI MAZURI NA PANAPEDEZA. PIA WAMEZUNGUSHA VINGUZO VIFUPI VILIVYOPAMWA KWA RANGI ZA BENDERA YETU.
VINGUZO HIVYO VIMEUNGANISHWA KWA MINYORORO MIZITO, AMBAYO INANIKUMBUSHA ILE WALIYOFUNGWA MABABU NA MABIBI ZETU TOKA BARA KUPELEKWA KATIKA GULIO LA WATUMWA BWAGAMOYO. HATA HIVYO WALE WATAALAMU WA VYUMA CHAKAVU WAMESHAFIKA IKULU, UPANDE WA KUELEKEA OFISI YA MWAKAMU WA RAISI WAMESHANYOFOA SEHEMU KUBWA YA ILE MINYORORO TENA KWA SIKU TOFAUTI.

SASA NAJIULIZA KUWA IKULU YETU NI SALAMA KWELI? KAMA MNAVYOJUA PALE WANALINDA WALE JAMAA WANAOOGOPWA NA NYASI ZA UWANJA WA UHURU HASA SIKU ZA SHEREHE ZA KITAIFA, KWA JINSI WANAVYOTIFUA ARDHI. PIA TUNAWAFAHAMU KUWA WAMESOMEA KUPIGA MAKOFI YENYE AKILI. SASA WANAKUWA WAPI WAKATI MATEJA WANAPOHUJUMU PALE IKULU?
IPO SIKU TUTASIKIA WAMERUKA UKUTA KWENDA KUPATA KIFUNGUA KINYWA NA MKUU WA NCHI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    hahahahaa eti wakanywe chai ata ivo si ni "mtu wa watu"?

    wee unaleta mchezo na hili life?acha tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    Umefika wakati sasa wa kukumbatia technology ya CCTV. Weka Camera pande zote na kunakuwa na mtu 24hours anaangia kila sehemu yaani karne ya 21 techniques za ulinzi za enzi za mwalimu.

    Halafu yale mabilioni wanatuambiaga ya kufanyia matengenezo IKULU huwa yanafanya nini kama hawawezi ku-upgrade security system kuwa ya kisasa?. Inashangaza sana enh!, yaani wazee wa chuma chakavu wanatembelea mpaka kwa mkuu wa nchi je sisi wa Tandika si ndiyo tumekwisha kabisa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    hilo si la kujadili, jadili maisha sawa kwa wote na maendeleo ya kasi ya wote na barabara za lami za vijijini ili watu wasafirishe mazao yao kaiakoo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    Si ndo mtu mwingine atapata Tenda ya Kurepea huo uharibifu?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2010

    hahahaha, wakapate kifungua kinywa na Mweshimiwa! Nimecheka sana, lakini hizi njaa! ipo siku minyonyoro itawatokea puani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    Yawezekana hao waliwekwa kulinda hiyo sehemu washegeuza mtaaji.. Si unajua wa Madhabahuni analia madhabahuni

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2010

    ndhani bongo ni bora kulinda benki zaidi kuliko ikulu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2010

    Na wewe mambo ya Ikulu yanakuhusu nini bwana? Wewe ni mpambe wa Ikulu? Achana na mambo ya watu. Take your time!!
    Mdau

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2010

    AISEEEE CHACHA...ARROOOO..HAO MAJAMAA YAKO KWENYE MTADAO WA OFAAA WAKATI WOTEE...MATEJA YANA AKILI KUSHINDA UNAVYOFIKIRI...WAO WAMEPATA DEGREE ZAO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU WEWE SIUMEZOEA UKACHUKUE OXFORD..KAZI KWAKO

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2010

    tatizo lakuajiri watoto wawajomba kuwa walinzi ikifika usiku wanaenda kujirusha. Kweli Tanzania tamu saana kwawalioipatia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...