Habari za leo kaka michuzi,
Nashukuri sana kwa Kuungwa mkono na watu wengi katika urudishaji wangu wa Form ya UBUNGE MUSOMA MJINI (CHADEMA) napenda kupata maoni ya wadau kupitia mail yangu na simu yangu ya rukono 0713275804
vincent_nye@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2010

    kila heri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2010

    You are very courageous to run as CHADEMA coming from your family!I salute you. Best wishes.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2010

    MNACHEKESHA NA HIZO NGUO ZENU, YAANI MKIMUONA MBOWE ANAVAA HIVYO NANYI MNAIGA BASI KUNA MAMBO MWEEEEE, ZIDUMU FIKIRA ZA
    MWENYEKITI

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2010

    Wewe umeamua kwenda kinyume na mategemeo ya familia? Mzee JK Nyerere angekuwa hai angekulaani wewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2010

    Anamlaani na nini? Kwani CHADEMA na vyama vingine vya upinzani si ni matawi tu ya CCM...!! Kama huelewi siasa za Tanzania shauri lako...hivyo vyama vimeanzishwa na hao hao CCM...huoni akina Lyatonga Mrema ati wako Dodoma wanaifagilia CCM wanasema ati kweli CCM ni kiboko...siyo upunguani huo ni nini? How can you defeat someone while you have already gave-in? Huo mchezo wa kijinga wa vyama vingi vivuli wengine hatudanganywi...!! Au Mithupu Unasemaje? Maana na wewe M-CCMMMMMMMMMM kama nini..!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2010

    chadema ni branch ya ccm,hiyo inajulikana wazi,semac division zero flani ndo wanaona eti chama cha upinzani,wewe unadhani wapinzani wa kweli watakuwa hawa form 4liver,chama kizima zito peke yake ndo ana degree,mipango mibovu.ccm inaibeba chadema ili watanzania wasishtuke;ukiisha uchaguzi utasikia ccm imeshinda kwa kishindo na wapinzani watafungua kesi uchwara mahakamani then unasikia kimya.hiyo ndo bongo,ni zaidi uijuavyo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2010

    we anony sun Jul 18, 05:11:00 AM, hayo magwanda ni uniform za chama kama vile kijani na nyeusi kwa CCM au vibarashia na vikoi for CUF au suspender for Democratic Party! Usicheke ni utaratibu tu!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2010

    We anonon wa Sun Jul 18, 04:40:00 AM ni mshamba kama wewe, huna maana, nguo tu ndo zinakushangaza, Mungu akusaidie, jiulize kazi ya Vyama vya siasa bungeni jinsi vinavyosaidia kukumbusha uongozi wa nchi unavyodanganywa mambo fulan fulan, Nguo si hoja, cha msingi KICHWANI, kalia kuulamba wakatihuna kitu kichwani.

    Hongera sana kuchukua form kupitia chadema,cha msingi tupate wa bunge nusu kwa nusu, kazi bungeni itaenda. na wewe anonon wa Sun Jul 18, 01:09:00 PM acha ushamba pia na upotoshaji wa waziwazi, imeandikwa wapi kuwa vyama vya upinzani ni matawi ya CCM,

    Kwa taarifa yako, siku CCM ikishangaa upinzani watachukua nchi,

    Kijana nazidi kukupongeza, na utashinda, si lazima kupitia chama cha babako, ndo maana ukiwa mkubwa unaweza kuacha dhehebu (dini) la baba yako ukaabudu sehemu nyingine ukishaelewa ukweli, ambaye anafuata babake kwa kila kitu ana mawazo mgando.

    si lazima ufuate kila kitu cha babako kama umesoma na kuelewa ukweli.

    hongera kaka na utashinda.

    Hafu wewe mchangiaji unayechemka kwa kusema ndani ya CHADEMA mwenye Digree ni ZITO tu pole sana.Unamjua mnyika, unamjua Slaa, unamjua Halima mdee! na wengine wengi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2010

    Hongera na hii inaonyesha maendeleo ya akili. Wanaosema nguo sijuinini wao wabakie hivyo hivyo wenzao wanaendelea.

    Mungu tubariki na hii ndio mwanzo vyama vya upinzani vikichukua nusu ya bunge tupo heri miaka mitano ijayo wataingia wengi na siasa ya kweliitembee.

    Mtu huwezi kubakia kwenye chama amabacho baba yako alianzisha kama unaona sera za mwanzishaji zimebadilikia..

    I salute you and god luck

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 19, 2010

    Hongera kijana.kaza buti siku za CCM zinahesabika.Hata mwl.angekuwa hai angejiunga na CHADEMA.Watu wenye akili timamu wanajaji chama kutokana na matendo yake.
    Ubora wa chama ni matendo yake,si hoja za nani kakianzisha.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 19, 2010

    hIVI ccm hawana uniform, unashangaa mavazi ya chadema mpuuzi kabisa, nawewe eti mwenye digrii Zito wewe unaamini digrii ndio uongozi, pole unaonekana umesoma vyuo vya siku hizi vya kata, Mithupu siku hizi tunataka tuanze kuona majina ya hawa hamnazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...