Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu kutoka Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Ndg. Alex Martin Owuor (USARO) Wa ( kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni Benjamin Sawe Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) akiongea na waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo kuhusu Mdahalo mkubwa utakao waunganisha Wagombea na Wanarorya wote jimboni Rorya tarehe 18/ 07/ 2010

Chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka wilaya ya Rorya wamejipanga kufanya mdahalo tarehe 18 mwezi huu kwa watangaza nia wa jimbo la Rorya

Mdahalo huo utakuwa juu ya kueleza mikakati ya watangaza nia wa Rorya kwa jinsi watakavyotekeleza masuala ya maendeleo pindi watakapopata nafasi.

Masuala hayo yatakuwa katika maeneo ya Elimu, Afya na Ustawi wa jamii, Kilimo na ufugaji, Maji, Miundombinu, Uchumi, Utawala Bora, Michezo na jinsi ya kuhimiza uwekezaji wilayani.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaotoka Wilaya ya Rorya, Martin Owour alisema kuwa lengo lao ni kuona kuwa wilaya hiyo inasonga mbele.

“Tunataka kuona wilaya yetu inasonga mbele katika masuala mazima ya kimaendeleo,” alisema.

Aliongeza pia wanafunzi wamejipanga kufanya shughuli mbalimbali za jamii kama kuelimisha juu ya masuala ya maendeleo.

“Uelimishaji huu unalenga kuwaelekeza wanajamii kujua masuala` ambayo wangetaka wanaogombea wayatekeleze,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2010

    joni mashaka upo??????????????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2010

    Sasa mbona hii inachekesha...."Wakiongea na waandishi wa habari ambao hawapo kwenye Ukumbi"...sasa hao waandishi wa habari wako wapi? Au ulimaanisha akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo? Au wakiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani? Mbona ninyi watu mnatuchanganya lugha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...