Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal kwa wananchi wa mji wa Dodoma leo jioni katika hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia katika uwanja wa michezo wa Jamhur mjini Dodoma leo jioni
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo jioni wakati wa kuwatambulisha mgombea mwenza na mgombea Urais wa Zanzibar leo jioni.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na msanii Flora Mbasha aliyejumuika na wasanii wengine kutumbuiza wakati wa hafla ya kuwatambulisha wagombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na mgombea mwenza katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo jioni. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

CCM imepata kichwa kingine (Dk. Mohamed Gharib Bilal) cha kumsaidia Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru!
ReplyDeletehivi ni lini kutakuwa na upinzani hapo tanzania?tumechoka na hao ccm.
ReplyDeletemdau wa pili hapo juu,
ReplyDeleteWewe unayeona kuna umuhimu wa kuwa na upinzani nenda kaazishe chama. Wenzio hawaoni kama kuna umuhimu huo ndio maana wengi wanaingia CCM..!!!
Be the change you want.
FLORA MBASHA ZIMEKUPENDEZA NGUO ZA CCM DADAANGU. ILA HATA USINGEVAA KIJANI NA NJANO PIA UNGEPATA KAZI YA KUTUMBUIZA DADA, SIKU NYINGINE USIJE UKALAZIMIKA KUFANYA HIVYO
ReplyDeleteMbona wapo akina mama wanaoweza? yupo Samia Suluhu, yupo Maua Abeid, yupo Zakhia Hamdani, yupo Kidawa, yupo Amina Salum, yupo Fatuma said yupo Waride bakari na wengi wengine.
ReplyDeleteZamu hii ilikuwa yao katika nafasi ya mgombea mwenza ambaye ni makamu wako
kwa mpango wa akina mrema kwenda kuisifia ccm vile,kwa kitendo alichofanya mrema ni stail ya kampen kwa ccm!!unadhan kawashawishi wananch wangapi ambao hawakuwa na mpango na ccm!!! na makada wa ccm kuchangia chadema cjui lin kutakuwa na upunzan wa kweli TZ
ReplyDeleteKha.....kwani huyu Dr. Bilal si alikufa jama, au amefufuka. Sio yule wa BOT?
ReplyDeletewewe mdau wa Tarehe Tue Jul 13, 01:35:00 PM... acha ukenge.. aliyekufa ni Bilali siyo Dr.Balal
ReplyDeletehiyo Podium hapo namna gani tena!! hivi CCM siku hizi wanakwenda na rangi NYEKUNDU????
ReplyDeleteFlora mbasha anaanza taratibu kuiimbia CCM nae baada ya uchaguzi utamwona amekuwa mfanyakazi wa BOT Kama ilivyokuwa kwa Vicky Kamata mwaka 2005. Alianza na vijinyimbo vyake vya kuisifia CCM baada tu ya uchaguzi akawekwa BOT sasa kaacha mziki anapulizwa na kiyoyozi. Natamani ningekuwa mwimbaji ningetunga vijinyimbo vya uwongo ilimradi kuisifia CCM then najikuta BOT.Kaka michuzi usiibane hii pls.
ReplyDeleteCCM IMEMPA HUYO DR MOHAMED GHARIB BILAL NAFASI HIYO KWANI SI KWA KUWA NI MZURI BALI INAMUOGOPA SANA KWA VILE ANAKUBALIKA SANA ZANZIBAR NA KWA VILE WAMEMNYIMA NAFASI YA URAIS ZANZIBAR SO WAMEONA ATALETA VURUGU ZANZIBAR NDO WAMEMPE HIYO KUMPOZA YEYE NA KUNDI LAKE ZANZIBAR, HIYO NI KUZIMA UPINZANI NADI YA CCM, AKILI MU-KICHWA BABU WEEEE
ReplyDeleteKaribu, Dr. Mohamed Gharib Bilal utuletee nuklia kwa matumizi ya amani!
ReplyDelete