Mpiga Galoon maarufu Zanzibar,Nassor Abdallah akikitendea haki kifaa hicho usiku wa kuamkia leo katika tamasha la ZIFF linaloendelea katika viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar
Nassor Abdallah (kati) akiwa na wenzake jukaani.
Mwanamuziki wa bendi ya Taiwa toka Afrika Kusini akipuliza Vuvuzela orijino wakati wakitumbuza usiku wa kuamkia leo katika tamasha la ZIFF.
Mpuliza mdomo wa Bata (Saxophone) wa Bendi ya Taiwa toka Bondeni akifanya vitu vyake huku mwenzie akimsapoti.
Shoo la ukweli toka kwa Taiwa liliangushwa na kumfanya kila mtu aliyekuwepo ngome kongwe kunyanyuka kucheza.
Hawa ni Royal Echoes kutoka Ghana nao walifanya vizuri sana katika Tamasha La ZIFF linaloendelea kufanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Mpiga Gita na mwimbaji wa Kwetulobo akilicharaza kisawasawa gita lake huku akiimba kwa hisia kubwa.
Wacheza shoo wa Kwetulobo wakifanya vitu vyao Kwetulobo wakiwainyesha umahiri waoo.
Wadau wa ZIFF wakibadilishana mawazo wakati tamasha likiendelea,kulia ni Prof. Martin Mhando,Edward Lusala na Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...