Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu katika mahojiano na nguli la habari Mzee Makwaia wa Kuhenga katika kipindi cha Channel Ten cha 'Je Tutafika?' cha wiki hii.
Home
Unlabelled
bosi wa shirika la nyumba la taifa alonga sehemu ya 2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JAMAA ANAONEKANA KICHWA NATUONA UBORA WAKUWEKA VIJANA MAMBO YANAONEKANA WANAYOYAFANYA, LAKINI MIMI NAWASIWASI HIYO PROJECT WANAYOTAKA KUIFANYA HAITAWANUFAISHA WANANCHI WA KAWAIDA,KWANI KILA MTU ANAJUHA KWAMBA ENEO KAMA LA UPANGA WATANZANIA WENYE ASILI YA ASIA WANAPENDA KUKAA WATATOA PESA YEYETO HILE ILIMRADI WAKAE UPANGA.
ReplyDeleteMIMI NAONA SEREKARI INATAKA KUWAJENGEA WAO SIO WALALA HOI NA KIGEZO GANI WATATUMIA ILI WATU WAPATE HIZO NYUMBA?
MIMI NAONA KWANZA JAMAA ANGESUBIRI MPAKA WAWEZE KUJUA JINSI GANI KUWEZA KUJUHA WATU WANASHIDA YA NYUMBA KWELI NDIO HAPATE KWANI KILA MTU HATATAKA HIZO NYUMBA ZA UPANGA HATA WALE WANANYUMBA TAYARI KWAHIYO HAWASAIDI WATANZANIA WAKAWADA WALA NINI.TUKIANGALIA NCHI KAMA YA UK WATUWANAWEKA KWENYE QUEUE NAKUWEZA KUPATA NYUBA NI KUTOKANANA JINSI GANI UNASHIDA JEE TANZANIA INAWEZEKANA KUMBUKA HUKU CORRUPTION FREE COUNTRY.
Pamoja na kumkubali huyu Mkurugenzi, mimi ninaomba sana sana sana, huu mradi wao wa Matrilioni USIJE UKAHARIBU JIJI LETU na MIJENGO inayoumiza macho.
ReplyDeleteHali inayoendelea sasa hivi maeneo ya mjini tunaona majengo mazuri yaliyojengwa miaka ya 1950's yakibomolewa na kujengwa majengo hovyo hovyo. City center inabadilika na itakuwa kama Kariakoo kwa majengo ambayo hayana dira ya kupenedezesha jiji. Karibia majengo yote mapya yaliyojengwa Morogoro Road yako out of character. Tusipoangalia, Dar itabadilika na kuwa A VERY BIG VILLAGE as opposed to A MODERN CITY.
Kwa hiyo basi, nakuombeni sana NHC, nyumba za Upanga ni nzuri sana na zimefanya Upanga iwe Upanga. Tafadhalini msizibomowe. Mkitaka sana kubomoa nyuma, nendeni Manzese, mbagala, , nunueni plot za watu, jengeni.
Anon unaesema asubiri, muda wa kusubiri kufanya mambo umekwisha. Asubiri nini? Tumechoka kusubiri, Action ni muhimu kwa sasa.
ReplyDeleteBwana Mchechu, hiyo model ya developers na purchase financed by mortgage unayotaka kupursue ina athari zake bila proper safeguards. Tatizo linakuja thamani ya nyumba inapokuwa inflated na easily available credit au kuipande mwingine artificial demand ya nyumba fueled by easily available credit.
ReplyDeleteTumeona masokomengi ya nyumba yameishia kuangusha uchumi wa nchi nzima kama ilivyokuwa Thailand in late 90's na kinanchoendelea sasa in the western world. Model hii, ina winners na losers, Developers, property surveyors na conveyancers are winners wanapate pesa zao haraka wakisha uza nyumba na losers ni wanunuzi na lenders soko liki crush. wanunuzi ukikosa kazi ukishidwa ulipa mortgate unapokonywa nyumba. Kwa bank soko liki crush thamani ya nyumba inashuka ku-reflect true market value na wakiuza nyumba watapata hasara, na hii ina-affect banks lending abilities na kuimpact real economy.
Namshukuru sana mkurungenzi kwa kutueleza shirika letu linafanya nini, shirika hili linatakiwa kuwa kwenye mfumo wake wa mwanzo wa kuwa na nyumba ambazo zitakuwa rahisi kwa wapangaji wa kawaida ili kumwezesha mfanyakazi wa serikali kulipa deni au pango, kwa kuangalia gharama za ujenzi na wakati uliopo, kwahili mwalimu hatapata nyumba, polisi hatapata nyumba, na kodi ipande kutokana na wakati, lakini kama alivyosema mkurugenzi kwamba ni kujenga na kuuza ni kweli niubunifu wa kisomi na husio wapa taabu shirika kwani ukinunua nyumba wao basi wewe utabaki unadaiana na modgage lender wako, katika hali ya Tanzania na hili linanitia mashaka sana kwasababu kwanza watu hasa wafanyakazi hela hawana, ila hapa tusipokuwa na uangalifu zaidi tutajenga ngome nzuri za rushwa ili mtu apate hela ya kuonyesha benki ili aweze kukopa /kununua nyumba, pili mkurugenzi angeongea na lender ambao ni benki waimalishe kampuni za insurance ambazo zitawadhamini hawa wakopaji, ili tuwe na uhakika kabisa nilazima tuwe na kampuni madhubuti sio kama shirika la bima ambapo nyumba imeungua lazima claims zinakuwa kama unachumbia au unatafuta mpenzi au hii ni rahisi make itachukua miaka kumi na tano hujapata hata malipo, haya ni mambo ya kuangalia sana,Tatu ni lazima jiji lihusishwe na watu waanze kulipa tax ya majengo hii itasaidia jiji kuwa katika nafasi nzuri ya kusafisha maeneo na kuchukua uchafu kutoka majumbani na bei hizi zipangwe na majiji na miji husika kwa kuhusisha watu wa NHC, hili serikali kuendelea kupata hela ni vyema kuwe na heritence tax pale mwenye nyumba anapokufa hili litazuia kuwa na watu wavivu wanaosubiri kurithi nyumba za wazazi wao na mwisho kuuanza kuuza nyumba hizo bila serikali kupata kitu mfano serikali imepata nini kwa waliouza nyumba za magomeni na kariakoo? na kama beki zitanunua nyumba hizo au NHC kwa kukata heritance tax kwa wale ambao hawataweza, hili litafanya wale waliouza kuendelea kununua nyumba mfano kama nyumba ya urithi ina thamani ya milioni mia tatu let say kodi ya urithi ni ten percent basi hawa kama ni ndugu wawili wanabaki na hela ya kununua nyumba zao ladba na kubaki na hela kidogo huu ndiyo utaratibu mzuri, mkurugenzi asiongee kujenga na kuuza tu.
ReplyDeleteNne, Tumefika wakati Tanzania tunahitaji kuwa na branch ya Royal institute of chartered surveyor hawa jamaa watatusaidia ku-control price of materials, lazima tuwe na national specification materials, Nationa price/preambles mambo kama haya yatatoa mwanga mzuri na tutakwenda kwa pamoja katika technology mpya ya ujenzi, ina maana ninaposema national specification materials hili nina maana kwamba standards za madirisha kivipimo lazima zifanane, milango hivyohivyo mbao za kenchi hivyo hivyo sio kila mmoja anaezeka anavyotaka, na mlango wa chumbani naweka kwasababu mke wangu mkubwa au mwembamba, ndugu mkurugenzi haya yote yatasaidia kwani huwezi kupata hata mtu mmoja wa kuiba hata shilingi kwenye mamilioni ya miradi hiyo. Mimi nashauri kwamba sasa tunahitaji kuanza kujenga hata nyumba za mbao hizi ni nyumba nzuri kwa ulinzi wa mazingira, ni suala la kukata mti na kupanda mti,hili nalisema kwani nimesikiliza maongezi ya mkurugenge wa NHC yeye hakugusia environmental katika mazungumzo yake yeye kazama kwenye kodi tu, hapa lazima tufikirie mawe, mchanga, na kusafirisha haya materials ni vipi vitasumbua mazingira yetu? je inawezekana tukawa na offsite materials kama nyumba za mbao, kama steel buildings, kama timber panels building, au la tunaweza dredge mchanga na mawe kutoka baharini, sasa hili lazima watu wa jiji watuongoze katika strategy plans zao hapa ndugu zangu watanzania tutafanikiwa vizuri sio mtu anakuja anatwambia tunajenga nyumba na kuuza tunamshangilia huyu jamaa kichwa bado huyu jamaa kama anataka kufanyakazi anayokazi nzito mbeleni.Lakini kwakushirikiana au public consultation itaongoza miradi hii japo najua halmashauri za miji wao kila kitu sawa, hapa nahisi tunahitaji kufuata mlolongo mzuri wa mazingira, na wataalamu wengine.
PKahatano BSC(hons)PD&QS(UK) HND in Construction(UK)
Mdau wa corruption free country, umesahau BAE systems ni ya wapi?
ReplyDelete