Bw. Alistair Horsburgh, Mkurugenzi wa Export Showroom, walio-supply matrekta hayo akionesha jarida la kampuni hiyo inayoongoza kwa usafirishaji wa bidhaa nzito toka sehemu yoyote duniani kuja Bongo. Viongozi wa CRDB, wakulima wa pamba wa Chunya na wa Export Showroom na wadau wengine, katika picha ya pomoja

Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei akiwa na Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Export Showroom Bw. Zubeir Masabo (shoto) wakifurahia kuwasili kwa muda muafaka matrekta hayo na matela pamoja na majembe yake
Mabosi wa Export Showroom wakijumuika na wadau katika hafla hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charels Kimei akikata utepe kama ishara ya kukabidhi matrekta 20 kwa viongozi wa Chama cha Ushirika cha Chunya leo kwenye sherehe zilizofanyika TAZARA jijini Dar. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Chunya; Ndg. Sebastian Mogela
Sehemu ya matrekta 20 ambayo CRDB imekabidhi leo




Dk Kimei akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji mizigo mizito ya Uingereza, EXPORT SHOWROOM, Bw. Alistair Horsburgh (mtasha) wakati wa makabidhiano hayo ya matrekta hayo leo.

Benki ya CRDB leo imekikabidhi Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku cha Chunya vifaa vyenye thamani ya dola 804,264.84 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania 1.2 bilioni) ili kukiwezesha Chama hiki kujenga maghala sita ya kisasa kwa ajili kuhifadhia tumbaku, kukununua matrekta 20 yenye plau na matela yake 20 ili kuongeza uzalishaji. Kati ya matrekta hayo 20, 19 yatakwenda kwa Wakulima wa tumbaku wa Chunya, mkoani Mbeya wakati moja litakwenda kwa Wakulima wa Mkwese, Manyoni, Singida.

Jana usiku, trekta hizi zilitolewa bandarini kwa muda uliopangwa na supplier na wakala wa usafirishaji mizigo mahiri wa uingereza ya EXPORT SHOW ROOM, jambo ambalo Bw. Kimei alilisifia mno kwa kuweza kutua mzigo katika muda muafaka.

Dk. Kimei kasema trekta hizo za Massey Furgeson ni za kisasa kabisa, zenye tela zinayotumia nguvu za kihaidroliki hivyo kuwa na uwezo wa kupakua mizigo zenyewe. Trekta hizi zina nguvu ya kani 175 au kwa kitaalam Horsepower.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jim Kibesa aaaaaaah mzee wa Reading!

    ReplyDelete
  2. Mmh Mwanangu Zuberi Masabo shavu dodo! Nakukubali na I hope umshaacha yale mambo yako zama zile Alharamain

    ReplyDelete
  3. Je, kuna uwezekano wa sera-pingana kati ya ma-Waziri (Kabineti) wetu; kwa mfano, baina ya Waziri Wassira (Kilimo) na Mwakyusa (Afya) kuhusu ulimaji wa zao la biashara la tumbaku na madhara ya matumizi ya tumbaku (ambayo yanapigwa vita duniani)?

    Hapa Amerika, uzalishaji wa zao la tumbaku umepigwa vita kiasi cha uzalishaji huo kudidimia katika majimbo tumbaku: North Carolina, Kentucky, Virginia, Tennessee, South Carolina, Georgia, Pennsylvania, Ohio, Connecticut na Indiana.

    Katika gazeti moja la Kiingereza, iliandikwa, kwa kifupi, “ (Special Seats, CCM) wanted to know if the ministry had any plans to set aside funds for educating tobacco farmers and users on the adverse effects of tobacco to their health.”

    Na katika kumjibu m-Bunge huyo, Waziri Wassira alitamka:

    “We are not concerned with this matter. We deal with agriculture. This falls squarely under the Ministry of Health and Social Welfare.”

    Waziri Wassira alisidi kusisitiza kuwa wizara yake itaendelea kuhimiza ukuzaji wa zao la tumbaku, kwani madhara yake yhayahusu wizara yake:

    “These adverse effects are for the Health ministry to deal with.”

    Swali la m-Bunge Stella Manyanya lilimshangaza Spika Samuel Sitta, ambaye alimkosoa m-Bunge uliza na kumpongeza Waziri Wassira:

    ‘What that again? Some of us depend on the crop and now you are fighting against it?...You (the minister) are the right person for us.”

    Sasa tunaona tunavyosaidiwa ili kuongeza “productivity” katika kuzalisha tumbaku, kama ilivyoandikwa kwenye blog hii:

    ”Benki ya CRDB leo imekikabidhi Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku cha Chunya vifaa vyenye thamani ya dola 804,264.84 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania 1.2 bilioni) ili kukiwezesha Chama hiki kujenga maghala sita ya kisasa kwa ajili kuhifadhia tumbaku, kukununua matrekta 20 yenye plau na matela yake 20 ili kuongeza uzalishaji. Kati ya matrekta hayo 20, 19 yatakwenda kwa Wakulima wa tumbaku wa Chunya, mkoani Mbeya wakati moja litakwenda kwa Wakulima wa Mkwese, Manyoni, Singida...”

    Kwa kifupi tu, haiingii kichwani! Badala ya kuwekeza katika mazao ya chakula, tunawekeza katika zao changizo la saratani! Hata huko Uingereza leo kuzalisha zao hili ni ”skandali” kubwa!

    Ni kwa nchi zetu tu (only in African countries)! Amerika au Uingereza leo hii kujigamba kuzalisha zao la tumbaku ni aibu kubwa kutokana na madhara ya tumbaku na athari yake kwa ugonjwa wa saratani!

    Tafakari!

    ReplyDelete
  4. Ankal mbona umevuruga habari

    Hii kampuni kazi yake kubwa ni sourcing sio kusafirisha mizigo.

    ReplyDelete
  5. Huyo jamaa wa tatu kutoka juu ni mbumbumbu wa lugha. Ondoa upuuzi hapa.

    Kilichoniacha hoi ni hii ya msichana kumshikia mwavuli jibaba zima. Ustaarabu wa wapi huu?

    ReplyDelete
  6. Mtajibeba mwaka huu!

    ReplyDelete
  7. Bradha, huyo TULI huyo me huwa ananiKILL sana huyo!

    Hivi unaweza kuniunganisha nae vipi?

    ReplyDelete
  8. Hongereni sana kaka zangu, am so proud and happy for you.

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa Aug 04, 04:16:00 AM hapo juu, jibu hoja iliyojengwa na huyo umwitae, "mbumbumbu wa lugha".

    Kuna ukweli kwa yale aliyosema: sera pindana!

    Ni sawa na biashara ya madawa ya kulevya! Ndi, wenguine wanatajirika; wengine wanaangamia hadi kufa!

    Rudi nyuma, na utafakari kuliko hilo jibu pumba lako!

    ReplyDelete
  10. ingekua mazao ya chakula ningeunga mkono sana,but anyway they know wat they r doing,
    namuona ndugu yangu Masabo hapo! u go brother!!
    Mariam-USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...