Home
Unlabelled
Dk. Shein afutarisha dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
mr mkapa umefunga? au unawapunja wenzio!
ReplyDeleteKweli Mkapa wewe umefunga au unadoea.Itabidi tukuimbie ule wimbo wa "wakristo tokeni wakristo tokeni mnatudoea" LOL.Kumbe ftar inaweza kuliwa mezani sio jamvini tu.Ni mara ya kwanza kuona ndugu zetu wakipata ftar mezani.Michu usinibanie.
ReplyDeleteDr .Shein,je umewakumbuka kuwafuturisha maskini walio na njaaa?
ReplyDeleteJamani msimseme Mzee wa watu, unaruhusiwa kuwaalika hata wasofunga ili kuonyesha ukarimu.
ReplyDeletemkapa amesilimu nini au masala ya ftari tena uroho tu?
ReplyDeleteHapa mimi ni bongo naipenda, Waislamu na wakristu wanapata futali pamoja...mimi binafsi sina dini nina amini kuwa kuna super power, lakini haya mambo ya dini siamini kabisa. Ninapenda ninapona watu wanaishi pamoja kwa amani bila tatizo la dini au ukabila.
ReplyDeleteJamani iftar au futari ni kifungua kinywa tu ni breakfast(breaking fast) au staftahi. Sasa inaweza kuliwa popote mtu anapotaka, kwa kuwa utamaduni wa waswahili na waarabu ni kukaa kwenye mikeka na majamvi, sio lazima na watu wengine wakae kwenye mikeka na majamvi.
ReplyDeleteWengine siku zote huwa wanakula chakula chao mezani, iwe siku za kawaida au mwezi mtukufu wa ramadhani.
Na nyie acheni uchoyo, futari muhimu ni kile anachokula mtu kwanza, iwe ni maji, tende au hata maziwa, hayo mengine ni maakuli tu kila mtu anakaribishwa kula!
Na Waislam munaofunga huu ndio mwezi wa kuonyesha ukarimu wetu kwa watu mbali mbali bila kujali uwezo na itikadi zao, kuna hekma kubwa ndani yake kwa kufanya hivyo.
manaomzonga mheshimiwa BW Mkapa hamna adabu.
ReplyDeleteHayo si maadili ya kitanzania.
Na kwa waislamu ndo usiseme, chunga funga yako.
Mbona yeye Mkapa hutayarisha futari na kualika waislamu, acheni udini.
tena nyie mnaosema hivyo mwaweza kuwa wakristo.
NAUNGANA NA MDAU HAPO JU ANAEWAKEMEA WACHANGIAJI WA MADA KWA UTOVU WA NIDHAMU. SI HESHIMA KUDAI MKAPA NI MROHO WA FUTARI. JAMANI! INA MAANA MKAPA HANA UWEZO WA KULA CHAKULA ANACHOKITAKA? TUWE WASTAARABU. FIKIRI KABLA YA KUTENDA. SHAME ON YOU!
ReplyDeleteMIE BINAFSI NIMEFURAHISHWA NA WAZEE WETU HAO KUKAA PAMOJA KWA UMOJA. JAPO ANAKOSEKANA HAYATI BABA WA TAIFA, JK NYERERE. HAPO SI MSOSI TU NDUGU WATANZANIA, NAAMINI PIA WANABADILISHANA MAMBO MAWILI MATATU NAMNA NCHI INAVYOKWENDA. KUHUSU MKAPA KWA UPANDE WANGU NAAMINI NI MMOJA WA VIONGOZI WALIOTENDAKAZI VIZURI NA HASA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI. NAKUMBUKA ALIPOKUWA AKIACHIA MADARAKA, KAMFUKO KA CHUMVI KALIKUWA KANAUZWA SH. 50. SASA HIVI NI KATI YA SH 300 HADI 500. TATIZO LAKE KUU MKAPA NI KUUZA NCHI KWA WAWEKEZAJI FEKI NA KIBURI CHA KUDHARAU ANAHABARI WENZAKE WA TANZANIA, KWAKWELI MAISHA MAGUMU WAJAMENI!!! BASI TU WATANZANIA TUNAJINYONGA WA KAMBA ZETU WENYEWE KWA KUSAHAU MACHUNGU YA MAISHA KILA BAADA YA MIAKA 5 UTADHANI TUMEROGWA. TUNANUNULIWA KWA POMBE, FULANA, KIBABA CHA SUKARI AMBAVYO HATA HAVIKAI HATA SIKU 2 LAKINI TWAUZA UTU, UTASHI, NA UHURU WETU KWA GHARAMA NAFUU KWA WANASIASA UCHWARA. TUTAENDELEA KUPIGIKA HADI KIELEWEKE.
huo ni ukarimu na upendo tunaotakiwa tuonyeshe kwenye dini yetu hususani kATIKA HUU MWEZI MTUKUFU....
ReplyDelete