Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) na East Afrika Radio kwa pamoja zimezindua kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mratibu wa kampeni wa vituo hivyo Alex Galinoma jana jijini Dar es Salaam, kampeni hiyo ilizinduliwa wiki hii kwenye kipindi cha 5 connect kinachorushwa kila jumatano kuanzia saa moja usiku.
Kituo cha EATV ambacho ndicho kituo namba moja kwa vija na kimechukua jukumu hilo kuwahamasisha vijana kutumia kura yao kutokana na utafiti ambao ulifanywa na kituo hicho kuonyesha kuwa vijana wengi hawashiriki katika kupiga kura.
Ilisema katika kufanikisha hilo, watakuwa wakitumia ujumbe ‘kijana acha kulalamika tumia kura yako’ na kwamba ujumbe huo utakuwa ukirushwa hewani kupitia televisheni ya EATV na East Afrika Radio.
Taarifa hiyo ilisema ujumbe huo unalengo la kuhakikisha kijana anachagua kiongozi bora badala ya kuwaachia wengine shughuli ya kuchagua viongozi na badala yake kuishia kulalamika pindi wanapoona uamuzi mbalimbali wa viongozi unawaathiri.
“Kampeni hii ambayo tumetumia picha za video na sauti za vijana mbalimbali itaendelea hadi Oktoba 30 na vile vile ifikapo Septemba tutazindua kipindi maalum kwa ajili ya uchaguzi kiitwacho uchaguzi Xpress live,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kipindi hicho watajadili mada mbalimbali zenye lengo la kumjengea ufahamu vijana kuhusiana na umuhimu wa yeye kushiriki katika uchaguzi mkuu ili waweze kuchagua viongozi bora na wenye sifa.

Hatua mliyochukua kuhamasisha vijana kushiriki kupiga kura hapo October ni ya msingi sana. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama hamkufanya zoezi hili wakati wa kujiandikisha na kuboresha daftari la wapiga kura, basi kazi yenu yaweza isizae matunda yanayotarajiwa kwasababu watakaopiga kura ni wale tu wenye sifa. Hata hivyo nawapongeza na kushauri media zingine waige mfano huu kwani kuna watanzania wengi wameamua kutopiga kura kwasababu mabalimbali ikiwemo kukata tamaa. NAWAKUMBUSHA KABLA YA UCHAGUZI MKUU 2015 MKUMBUKE KUHAMASISHA WATU KUJIANDIKISHA.
ReplyDelete