Vodacom yamwaga Vifaa kwa Vilabu Ligi Kuu

Vodacom Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 290 kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza alisema ni matumaini ya kampuni yake kwamba vifaa hivyo vitakuwa ni kichocheo cha kuinua kiwango cha soka hapa nchini.

Alisema huu ni msimu wa tisa tangu Vodacom ianze kudhamini Ligi hiyo na kwamba Vodacom inafarijika kuona kiwango cha soka kikipanda.

Mbali na kukabidhi zawadi hizo, alivishauri vilabu kutafuta njia nyingine za kuongeza mapato ikiwamo kutafuta wadhamini wengine ili kukabiliana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za uendeshaji wa vilabu.

Alisema msimu huu Vodacom imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kudhamini ligi hiyo.

Alisema kati ya hizo shilingi milioni 667 zimetengwa kwa shughuli za uendeshaji wa Ligi ikiwemo nauli za timu pamoja na gharama nyingine kama posho za marefa.

Rwehumbiza alisema msimu huu vifaa vimeboreshwa zaidi na kuvitaka vilabu kuvitumia vifaa hivyo kuboresha Ligi.

Alivipongeza Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya vizuri msimu uliopita na kuvitakia kila lakheri msimu huu.

Aidha Mkuu wa Udhamini huyo alitoa rai kwa vilabu kuvitumia vifaa hivyo kama changamoto ya kufanya vizuri katika Ligi ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11na hivyo kutupatia mwakilishi bora wa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Vodacom, nadhani ni utaratibu mzuri mnaoutumia kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zote zinazoshiriki ligi kuu, hii inatoa ushindani sawia kwa timu zote.Sikubaliani na baadhi ya wadhamini wanaotoa msaada kwa baadhi ya timu,hii inaupendeleo wa kiaina kiakili na hivyo kuzipa timu nyingine mazingira ya kujiona tayari hawana nafasi ya kushinda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...