Asalaam Aleykum,
Kaka Michuzi na wadau wote wa globo hii.
Tunamshukuru Allah kutujaalia sote kufikia kumi hili la pili la mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, na hivyo tunawaombea baraka, afya na amani wadau wote wa globo hii waliojaaliwa kufunga Ramadhani na ambao hawakujaaliwa. Kaka michuzi, sisi Leeds Swahili Community tunawashukuru sana watu wote waliohudhulia muhadhara wetu wa leo uliofanyika katika ukumbiwa Mabegate Mill na kisha kufuturu kwa pamoja kwenye ukumbi wa Ebbo Garden
Shukurani za Pekee zimuendee Muhadhiri ; SALUM KHATIBU na wenzie kutoka London
Kwa wengine ambao hamkupata nafasi ya kushiriki nasi kwa safari hii, tunahakika Inshaalah tutashirikiana nanyi safari ijayo. Hata hivyo kwa upendo wenu tumeona tushiriane nanyi kwa kuwaonyesha baadhi ya matukio kama ifuatavyo:

Pichani juu ni Ustaadh Malick (mwenye koti) akifungua muhadhara na kumkimkaribisha rasmi muhadhiri Ustaadh Salum Khatib na pembeni kushoto mwenye miwani ni mwenyekiti Amran Rashid

Baadhi ya wahadhiriwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini
maada ya Familia na Tabia Bora (wazazi na watoto)
Wahadhiriwa wakifuatilia muhadhara
Watoto kwa wakubwa wakifuatilia mawaidha
Futari imeshaandaliwa...
wadau wakifutari
Futari ikiendelea
Leeds Swahili Community inawatakia Ramadhani
Mubaraka na Inshaallah Allah atupokelee Swaumu zetu

Asalaaam Aleykum

Wabilah Tawfiq
Mwenyekiti Amran Rashid,
Mjumbe Ustaadh Malick








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wapi Dr.Mahir?
    Maashaallah, naona maustaadh wengi mliwakilisha,

    ReplyDelete
  2. Hivi siku hizi hakuna wanawake waislamu? AU ndiyo dini?

    ReplyDelete
  3. Hii fuatilia kwa makini mbona ina utata? Naona kama kuna waliouchapa usingizi....

    ReplyDelete
  4. Hebu yafikirieni haya:

    Mosi, naani ni lazima mkae chini....jangwani ni mahema shauri ya kuahamahama ...kubeba beba mameza na viti ni shida! Lakini sio kila mahali ni jangwani!

    Pili, wakati wa kuiyta waumini kuswali..hakuna haja ya kupaaza sauti. Siku hizi mifumo ya kupaza sauti ipo mingi; hata hivyo, ni pamoja na teknolojia ya saa. hakuna haja ya kuwakumbusha waumini saa ya kuswali imefika kwa kupaza sauti!

    Ni mawazo tu...soma na ukae kimya hapa mtndaoni; tawanya kwa wenzako!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...