Kaka Michuzi,
Kwanza nakutakia mfungo mwema wewe
Kwanza nakutakia mfungo mwema wewe
na waislam wengine popote ndani na nje ya Tanzania.
Nimeona niandike haka kameseji kadogo kwa Watanzania wenzangu kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi. Na kameseji kangu ni juu ya malumbano yaliyoshika kasi kipindi cha hivi karibuni kutokana na kauli kama mbili tatu zenye utata kutoka kwa kiongozi wa waajiri (Serikali) Mh. Rais wa JMT na kauli nyingine ya kutoka kwa Kiongozi wa vyama vya wafanyakazi TUCTA.
Nachopenda kukizungumza ni kusikitishwa kwangu na namna upande wa serikali unavyoshughurikia hilo tatizo. Kumekuwa na press conference nyingi za watendaji waandamizi wa serikali tena wa kada za juu na matamko mengine yasiyo rasimi. Wote kwa pmoja wanasema TUCTA inakiuka, Sheria na Taratibu kujaribu kumpigia chapuo mgombea mmoja. Juu ya hilo mimi sijui kama serikali wapo sahihi au laa, wala sihitaji kulijadiri.
Kinachonisibu ni hivi, Je, Huu ndio utaratibu unaopaswa kufuatwa na serikali yetu kujibizana wafanyakazi kupitia media? Mimi binafasi kwa mtazamo wangu naona serikali inakosea na kwa kufanya hivyo inalifanya suala la TUCTA kuwa kubwa. Kwanza baada ya mheshimiwa Rais kutoa tamko kiitifaki haitakiwa watu wa chini yake kuendelea na matamshi labda wawe wametumwa na Rais mwenyewe. Mh. Rais alishasema msimamo wa serikali sasa hawa watumishi wa chini ya rais wanatoka na vitamko kila kukicha vya kusema nini? Hawa wanamchonganisha Mh. Rais/serikali na wananchi.
Hawa wanasiasa na watendaji wetu na wanaelewa taratibu, huwezi kwenda habari malezo ukatoa ujumbe unaomlenga kumfikia katibu mkuu wa TUCTA, ukidhani Mgaya kama katibu mkuu wa TUCTA ameupata? Una uhakika gani hajaenda kuzika ndugu yake huko Ludewa ambako hata gazeti halifiki? Tumewapa simu na fax ofisini kwao, tunalipia bili za simu hizo kwa ajili ya nini? Kwanini hawawezi kumpigia katibu mkuu wa TUCTA kumuomba kama sio kumuamrisha wazungumze? Tumewanunulia computer tumewaungia na Internet masaa yote wanatumia hizo internete kufanya nini??? Badala ya kukaa kwenye computer hizi wakaomba mkutano na TUCTA kwa njia ya chati, SKYPE, hata wakatumia hata kuandikiana e-mail na kujibizana kufikia muafaka wanatoka na kukaa vibarazani hapo habari maelezo na kutusumbua wakulima ambao sisi wenyewe tunawaza bei ya kahawa na kama tutapaa mvua next year. Kibaya zaidi wana ma-land cruiser yetu, tumewanunulia ili waweze kuyakimbiza zinapotokea emergency kama hizi, huyu bwana wa utumishi wa umma (kwa mfano) angeenda na lile cruiser lake ofisini kwaMgaya akamwambia anamthamini Mgaya kama mtanzania na zaidi kama mfanyakazi na anatambua mchango wa wafanyakazi sio tu katika ujenzi wa taifa hili lakini pia katika siasa za Tanzania, sasa basi, anamuomba waongee kesho au siku yoyote kungekuwa na shida gani??
Muda umefika sasa wa serikali kujua kuwa haipo juu ya wananchi wake? Serikali imewekwa na sisi wananchi ili itutumikie? Serikali inawajibika kwetu na si vinginevyo. Kauli za ubabe na vitisho haziwezi kuisaidia serikali kutawala. Serikali zilizofanikiwa kuongoza vizuri duniani kote ni zile zilizoongoza kwa kufuata utawala wa sheria na taratibu. Hawa watumishi waliotoka na kauli za vitisho wanamuabisha JK, sio hulka yake, hawa ndio wanamshauri vibaya Rais, wanatumia vibaya ofisi zao na madaraka yao? Kwanini hawatakai kuona kuwa wafanyakazi nao ni Watanzania wenye haki ya kusikilizwa na kuzungumza nao wanakimbilia kwenye magazeti, redio na TV?
Natoa wito watedaji wakuu wa serikali waache kutujaza hasira wananchi, watafute njia nyingine muafaka ya kushughurikia suala la wafanyakazi. Serikali watafuteni TUCTA zungumzeni, sisi kama wananchi tungependa kusikia kuwa serikali na TUCTA wamefikia muafaka huu, Kwishney!!! Hizi blaa blaa zingine hazituhusu.
Naamini Serikali yangu itanisikiliza kwa masrahi ya Watanzania na amani ya nchi yetu.
Mungu Ibarki Tanzania
Hekima,Umoja na Amani
Zibaki kuwa ngao zetu
Jackson Mbogela
Mdau wa Makete
Mkuu mtoa mada, kwanza hongera kwa hoja yako. Pili, Mkuu Misupu nakushukuru kwa kuweka mada hiyo hapa globuni.
ReplyDeleteTatizo ninaloliona, zile kura ambazo Mh. Rais alisema kama TUCTA wanataka kumnyime, na wamnyime, lakini mishahara yao hatapandisha. Lakini ajabu ni kwamba serikali hiyo hiyo ya JK imepandisha mishahara kinyemela (kimya kimya) na kupunguza kodi na hayo ndio yaliyokuwa kwenye hoja za TUCTA tangu awali walipokuwa wanaongelea madai yao.
Serikali iliposikia kwamba TUCTA wanachimba mkwara kuwa watampakulia pilau mgombea ambaye anahitaji, CCM na serikali wame-panic maana kura 350,000 ambazo Kikwete aliziona ni chache sasa zimekuwa nyingi. Mzee Mwinyi amenukuliwa na magazeti akisema upepo wa kisiasa ndani ya CCM si mzuri. Kwa hiyo minyukano ndani ya CCM na minyukano mingine nje ya CCM inatishia kupunguza kura za Kikwete na pia kasi ya Dr. Slaa moto wake ni mkali, CCM wameingiwa na kiwewe.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, ame-quote sheria inayokataza TUCTA kuongelea makubaliano ya mishahara na serikali, lakini haikatazi TUCTA kuamua wampe nani kura. Vyama vya wafanyakazi kihistoria ndio ambavyo vimezaa vyama vya siasa ama vimechangia sana katika jitihada za kuleta mabadiliko. Tuna mifano mingi tu ya Afrika Kusini, Zambia, Zimbawe, na kwingineko.
Hayo tunayoyaona ni kwamba CCM inatapatapa. Kikwete hawezi kurudi kwenda kujibu hoja za TUCTA maana walimvua nguo tangu alipoambiwa kwamba information alizopewa hazikuwa sahihi na hata madai ya JK kwamba kuongeza mishahara wangehitaji serikali ikakope nje, waliomsaidia kupiga hesabu walimdanganya.
Kwa hiyo ili ku-save face inabidi Mkulu atume hao watu wa chini yake. Kosa lao ni kwamba hawako organized, kila mmoja anakuja kusema lake na wengine wanaishia kutishia tu kwamba sheria imevunjwa, ukiuliza sheria gani wanakupatia sheria ambayo haiko applicable.
Kila la Heri JK, lakini mwaka huu angalau Mgaya na TUCTA yao wamekushikisha adabu, next time kabla ya kutoa hotuba hutaropoka ama kutoa kauli za dharau na kejeri kwa wapiga kura ambao ndio waajiri wako. Kila kura ina-count kwenye ushindi.
Sasa wewe ndugu unasema huu ujumbe utaikia serikali, kivipi? Serikali wanakuja kusoma blog ya Michuzi? Nafuata kauli yako uliyosema kuwa serikali iwatumie ujumbe moja kwa moja TUCTA, siyo kutegemea ataona kwenye TV nk.....
ReplyDeleteNYIE CHADEMA FUNGUENI BLOGU YENU HII NI BLOGU YA JAMII.
ReplyDeleteTENA ACHENI UWONGO WENU ETI KUWA BAADA YA SERIKALI KUONA SIJUI DR. SLAA SIJUI NINI. KIKAO KILICHOKAA KUKUBALIANA NA NYONGEZA ZA MISHAHARA KILIKAA TAREHE 8 MWEZI MAY NA MAKUBALIANO YAKAFIKIWA YA KUONGEZA NA KUPUNGUZA KODI. JE HAPO CHADEMA WALIKUWA WASHAMTANGAZA MGOMBEA WAO? NA JE JK ALIKUWA AMEKWISHATOA TAMKO LA KUSEMA SITAKI KURA ZA WAFANYAKAZI?
TAMKO HILO ALISEMA "KAMA WATAENDELEA NA KUDAI KILE AMBACHO HAKIWEZEKANI...... NA KUTISHIA ETI HAWATAMPA KURA...........
HATA INGELIKUWA MIMI NISINGEKUBALI KUTISHIWA TENA BAADA YA KUFIKIA MAKUBALIANO.
SWALI LA KIZUSHI, CHAMA CHA LABOUR CHA UK KILIUNGWA MKONO NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI, LAKINI JE LABOUR ILISHINDA KWENYE UCHAGUZI MKUU ULIOPITA?
NA WALIOKUWA WANALILIA TORY WASHINDE SASA HIVI MBONA CHAMOTO WANAKIONA!
HUENDA NITAKUWA NIMEENDA NJE YA MADA, HATA HIVYO, NAOMBA KUPEWA UFAHAMISHO KUHUSU KIWANGO CHA ELIMU CHA MGAYA, KIONGOZI WA WAFANYAKAZI.
ReplyDeleteTarehe Sun Aug 15, 12:03:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous:
ReplyDeleteSisi sio Chadema, sisi ni Watanzania! Why are you so myopic and paranoid? Uliambiwa hili jamvi ni la CCM? Kama ulivyosema, hili ni jamvi la jamii, na jamii ni Watanzania wote regardless wanashabikia chama kipi.
Huyo mdau alosema nyie Chadema tafuteni blog yenu kalipuka anahitaji zima moto...Kusema ukweli kama tunahitaji maendeleo na haki tunahitaji watu wachache na sio wengi na mmojawapo ni Mgaya...Go go Mgaya go.
ReplyDeleteWewe unayeuliza elimu yake unadhani itakusaidia nini wakati Degree za awadi bongo zimejaa
Sasa mnajificha nini wakati inajulikana wazi kuwa Mgaya ni Chadema na anawaburuza wafanyakazi waichague chadema. Hivi mnafikiri wafanyakazi wote watachagua Chadema? Kuna wanachama wa CCM, CUF, TLP, na haiwezekani kuwalazimisha watu wachague Chama chake, ndio maana mtu ameuliza kiwango cha elimu cha Chadema.
ReplyDeleteHuyo mtoa mada ana blogu yake huku kwa Michuzi kaja kujitangaza tu, hii ishu imejadiliwa kwa mapana na watu kibao wamechangia huko kwenye blogu ya gazeti ilipotoka.
Pili wengi wenu mko nje ya nchi lugha zenu na IP address zenu zinaonyesha.
Tatu wimbo wa kura za wafanyakazi ni wa Chadema, ndio maana TUCTA waliwaalika viongozi wa Chadema kwenye sherehe za May 1. Sasa mnakataa nini na mnaitumia TUCTA kwenye kampeni zenu za uchaguzi?
Hii ni blogu ya jamii bwana sio kila mtu anashobokea siasa blogu ya Chadema ipo, na nyie mna blogu zenu au watu hawaji huko? Au mpaka tuwataje kwa majina ingawa mmetumia anony.?
Nyie CHADEMa mnakera na uongo wenu sasa! Kwa uongo wa dhahiri namna hiyo mkipewa nchi itakuwaje? Halafu huyo mgaya atapata wapi kura za wafanyakazi ili azipeleke anakotaka yeye? Au anadhani sisi wafanyakazi ni misukule wake wa kutekeleza matakwa yake ya kisiasa? Kura zetu tutapeleka tunapoona sisi panafaa, sio anakotaka Mgaya!
ReplyDeleteSisi tukiwa wafanyakazi mshahara tumeongezwa tunamshukuru JK na serikali yake. Sasa haya mengine mnayoyasema TUCTA au Kaimu Katibu mKuu hayatuhusu. Muradi tumeongezwa mshahara JK kura yetu tunampa. Basi.
ReplyDeleteSasa huyo Slaa mwenye kiu ya kubadilisha katiba ya nchi ilhali sisi wafanyakazi tunajua masalhi yetu yanalindwa na Katiba kura yetu hatumpi hata.
wewe unayeuliza degree itakusaidia nini? mbona tuna viongozi wengi tena wazuri ambao hawana degree! hizo degree za dar ambazo wengi wana copy vyeti vya jamaa, ndiyo nini? Dr. Dr. Dr. mbona umasikini unaendelea mbali na na Dr zenu. Watanzania tunajua kuandika reports nzuri na kutayarisha mikutano ili tuweze kupata vidollar kama allowances. We need those people who can deliver siyo nyie kukaa na kuandika reports ambazo hazina hata maana yoyote kwa maendelao ya watu na taifa lao! Kasome katika nchi za watu ndio tujue mna degree!
ReplyDeleteTatizo letu watanzania tunapenda polojo na kusahau hoja za msingi. Angalia kweli kima cha chini cha mshahara cha 200,000 kitakizi mahitaji ya mwezi? TUCTA wanachosema nikweli tena wanabidi waungwe mkono kupata ufumbuzi wa wanyonge. Angalia hao waheshimiwa hapo Bungeni posho zao ni kubwa kuliko wanachokifannya ndio maana watu wanahonga kuelekea Bungeni. Mr Mgaya kama angekuwa na Tamaa au ubinafsi basi angewania Ubunge, lakini ameweka maslahi ya wanyonge mbele hata kuhatarisha maisha yake, he needs our support. TUCTA kipindi hiki cha uchaguzi ndio kizuri kupata mahitaji yenu wala msibabaike na vitisho vya Kapuya. Kama kweli ni uvunjaji wa sheria Mahakama peke yake ndio jibu.
ReplyDeleteelimu ikusaidie nini wee annon apo juu???
ReplyDeleteivi wangapi wana u-profesa na wameprove takataka likija swala la uongozi bora na matokeo ya mtu kuwapo uongozini?angalia matajiri wagunduzi wote duniani wana elimu gani ndo ubweke apa!!!
sifuri kabisa