Ankal, shikamoo,
Natumaini umeamka salama na swaumu
Natumaini umeamka salama na swaumu
inaendelea vizuri. Tumepokea ujumbe huu
na tunaomba utusaidie kutangaza:
______________________________________________
The Program Coordination Unit at the International Organization for Migration (IOM) is investigating how the Tanzanian diaspora is affected by the creation of the East African Community Common Market.
______________________________________________
The Program Coordination Unit at the International Organization for Migration (IOM) is investigating how the Tanzanian diaspora is affected by the creation of the East African Community Common Market.
The Tanzanian diaspora is made up of people who are from Tanzania but who either live abroad currently, or lived abroad in the past.
This research is timely to us here at Vijana FM since we have recently been discussing things like citizenship, empowerment, the Common Market, and returning home.
To fill out a survey,
please select one of the links below:
Survey for current Tanzania diaspora members
Survey for former Tanzania diaspora members
Survey for current Tanzania diaspora members
Survey for former Tanzania diaspora members
Thank you, Isabelle Pugh, for letting us know about this.
________________________________________________
Source: http://vijana.fm/
________________________________________________
Source: http://vijana.fm/
Mimi ni Mtanzania. Naishi Marekani na nina pasi ya TZ na Marekani. Nina elimu ya juu ya Biashara (, B.Sc., na MBA kutoka Boston University). Nimerudi wiki ya jana kutoka Tanzania. Inasikitisha kuona kuwa Tanzania inarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kilichobadilika ni nyumba mpya tu zinajengwa. Barabara ni mbovu vile vile, askari bado wanasumbua wananchi, fedha inazidi kushuka thamani, maisha ya watu wa hali ya chini inazidi kudidimia na ufisadi bado unaendelea mpaka leo. Maji na umeme bado shida. Madawa hospitalini ni shida. Niliumwa jumamosi lakini nikapata daktari jumatatu. wikiendi huwa hawafanyi kazi za kutibu. Serikali bado inaomba misaada kulipa madeni na gharama za kuendesha nchi. Hayo maendeleo wanaosema viongozi wetu yako wapi?
ReplyDeleteNimesubiri miaka 20 ili nione maendeleo kabla ya kurudi, lakini sioni kitu. Sina haja tena ya kurudi nyumbani. Nimeuza nyumba yangu niliojenga mwaka juzi na kukaana uraia wa Tanzania. Sina haja tena ya kurudi nyumbani wala kutumia elimu yangu huko.
na wewe hapo juu utakuaje na pasi mbili wakati tz haina dual citizenship...mmmmmhhhhhhhahahahhahahah msomi huyooooo
ReplyDeleteMnakimbia nchi halafu mnasema inarudi nyuma. Itajengwa na nani kama nyie mnakimbia? Rudi hapa ujenge nchi ndio ufungue mdomo....longo longo wakati nyie mko kwenye nchi waliojenga wengine..It wasn't easy for them neither ..Remeber they started in 1492 hao wameeanza kuijenga nchi yao...Usione vinaelea vimeundwa...Njoo uunde cha kwako hapa na watoto wako wakukumbuke kesho
Mdau wa kwanza, pole kwa yote. Hali ya nchi yetu inaumiza mno. Lakini jawabu sioi sisi wananchi kusema 'sina haja tena ya kurudi nyumbani'. Kumbuka, si wewe mwenye haja, ni nchi yako ndio ina haja. Hali ya kimaendeleo inawezekana haijabadilika (au inarudi nyuma), lakini hali ya kisiasa inabadilika. Na hali ya siasa ni msingi wa mambo mengi, ikiwa pamoja na maendeleo, elimu, uraia na ufisadi.
ReplyDeleteHivyo basi, nakushauri na kukuomba, hali hii ya kisiasa ikishabadilika na kukaa sawia, urudi nyumbani hata kama si 'mazima' ili na wanachi waliobaki nyumbani wapate mwanya wa kuonja raha ya maendeleo.
HALAFU MICHUZI BANIA KAMA KAWAIDA YAKO
Shukrani Michuzi kwa kutusaidia kuwasilisha ujumbe!
ReplyDelete@ Anon, Sun Aug 15, 05:54:00 AM,
Jasho na damu ya watu ilimwagika wakati hiyo nchi unayoishi sasa hivi inajengwa. Na hakuna "short-cut" ya kuleta maendeleo Bongo; huwezi kukaa sehemu fulani miaka 20 halafu unarudi ukitegemea kila kitu kitakuwa shwari au tambarare kama Mamtoni. Nani atajenga na kuendeleza nchi kama sio mimi na wewe?
Kulalamika kama hivi na kuendeleza porojo haisaidii, na ndio chanzo cha fikra za watu, ujenzi na maendeleo ya nchi yetu kudumaa! Utategemea watu walio na elimu makini waje na mawazo ya kuchochea maendeleo...
Na kwa wale vijana mnaoanza kuwa na mawazo potofu kama haya, someni maoni ya watu hapa:
http://vijana.fm/2010/07/21/vijana-wa-tanzania-tuamke/
http://vijana.fm/2010/07/27/ze-utamu-arudi-kuwapangusa/
Jumapili njema.
Mfano wa mafisadi kama unaishi moshi angalia idara ya maji Moshi ulinganishe na Tanesco. Yote ni mashirika ya uma lakini Idara ya maji walishajikombowa na rushwa siku nyingi, Nenda Tanesco ni mafisadi wakubwa sasa niambie ukichukuwa form tu ni unaanza kulipa. Yani unahitaji service ili wapate pesa lakini inabidi ununuwe kila service the same na Tanesco Arusha hao wahasibu ni wezi wakubwa. Sasa ufisadi wa mchana namnahiyo tutafika kweli?
ReplyDeleteMimi ni anony wa kwanza wa Marekani-Tanzania.
ReplyDeleteKila mtu anasema kuwa sisi wasomi ndio turudi na kuleta maendeleo. Tatizo ni kuwa hatupewi nafasi ya kuleta maendeleo.
Nilishakaa Tanzania miaka mitano baada ya kupata elimu yangu Marekani lakini kila kona nikienda mafisadi wananisubiri. TRA na polisi walikuwa wananiandama kama vile mimi ni jambazi sio mfanyabiashara aliyoleta ajira kwa watu 15. Fomu zote za mwanahesabu wangu zinakataliwa mpaka nilipe chochote TRA. Nilifanya biashara kwa shida kwa kuwa kama mteja amesahau kuchukua risiti basi natozwa faini mimi mfanyabiashara kwa kuwa naambiwa nakwepa kodi.
Nchi inajengwa kwa kutumia wasomi. Nchi kama Latvia, Turkey, Chile na Brazil waliteuwa wasomi wa Marekani kuwapa program serikali ya jinsi ya kuendesha nchi, jinsi ya kupata kodi zaidi, jinsi ya kuleta biashara na viwanda kutoka nje. Serikali ina dharau ya hali ya juu kuhusu utumiaji wa wasomi wa Kitanzania, hatiheshimiki kabisa. Ndio maana nikasema kuwa wenzetu walitumia miaka 20 tu kama Malaysia na Singapore na sio miaka 200 kama Marekani au 500 kama Ulaya kuleta maendeleo nchini kwao. Sisi, miaka 20, tunaonyesha barabara za misaada, viwanja vya misaada na watoto wetu wanazidi kufa na njaa na bila matibabu. Wadau wanaosema niwe na subira na nije kusaidia nchi, nasema nimeshajaribu kuja na kufanya biashara na kujenga nyumbani lakini nimeshindwa na mafisadi na serikali ya Tanzania haina program yoyote ya kutumia wasomi kuleta maendeleo. Ni rahisi kwao kuomba misaada kuliko kunipa support kuendesha kiwanda changu bila ya usumbufu. Hamna mfanyabiashara yoyote duniani kotote vile, anayeweza kufanya biashara kw ausumbufu na TRA inaongoza kusumbua wafanyabiashara wadogo wadogo kama mimi na kuwaacha wakubwa kwa kuwa wanapata posho kubwa.
Ninaamini kabisa, hakuna watu wazalendo kama wasomi ambao wameishi ughaibuni, hasa katika nchi zilizoendelea. Wanajua misingi, gharama na thamani ya kufikia maendeleo.
ReplyDeleteLakini cha kusikitisha, hawana nafasi ya kuendeleza nchi pale wanaporudi nyumbani. Wakijaribu kufanya biashara wanaishia kuwa wahanga wa vitendo vya kidhalimu vya TRA na serikali ya kifisadi. Na kama hali hii itaendelea basi maadui zetu ujinga, umaskini, maradhi na viongozi mafisadi(na wasio wawajibikaji) wataitumbukiza nchi hii katika shimo la umaskini uliokithiri.
Poleni sana ndugu zangu mnaoishi Marekani, wenye uchu wa maendeleo kama mimi. Natumai ya kwamba tutakuwepo katika siku ambayo watanzania watataka mabadiliko ya kweli na kutaka mchango wetu.