Kila Jumatatu kuanzia Saa 4 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) limekuwa likiendesha Jukwaa la Sanaa ambapo wasanii na wadau wa sanaa wamekuwa wakipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali yahusuyo kazi zao.
Wadau wanakaribishwa kwenye Jukwaa Jumatatu ijayo ya Tarehe 16.8.2010 ambapo mada itakuwa Mchango wa Vyombo vya Habari Katika Kulina Maadili Ya Mtanzania itakayowasilishwa na Mtaalam Kutoka Mamlaka ya Mawasililano Tanzania (TCRA).
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakimsikiliza kwa makini,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe wakati akiwasilisha mada kuhusu Changamoto Katika Tunzo za Muziki Tanzania
Meneja wa Kilimanjaro lager ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Tunzo za Muziki Tanzania, George Kavishe (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake Jana Jumatatu. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Ghonche Materego na Katibu wa CAJAtz,Michael Bumbuli.
Mkongwe wa miondoko ya Reggae, Ras Inocent Nganywagwa, akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa. Picha na habari na Afisa Habari wa BASATA,Alistide Kwizela
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...