Ankal,

Juzi nilipita mitaa ya Kariakoo kufanya shopingi na vijana wangu hatimae nillingia duka moja la jamaa yangu anaeuza nguo.

Kilichotokea ni kwamba alinifungia nguo za watoto lakini nilipoangalia baadae nikaona kwa ndani ya bahasha kuna “ sticker”! kama zinavyoonekana hapo pichani.

Tofauti yake na sticker origino ni kwamba hizi hazina namba;

Sijajua sticker hizi nyeti zimefikaje kwa watengeneza mifuko wa Kariakoo labda wahusika wa Kamati ya usalama barabarani wanaweza kulisemea hili

Pia sina uhakika wa sticker zilizopo kwenye Baadhi ya magari. Je, inawezekana hali hii ikachangia ajali zinazosababishwa na ubovu wa magari?

Wadau mnasemaje?

-Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nchi hii kila kitu kinawezekana na ukiuliza sana utaambiwa SIO RAIA.

    ReplyDelete
  2. kaazi kweli kweli umeshawaharibia wenzio ..... waache apate ... si afadhali wao wanaiba kidogo kuliko mafisadi mamilioni na matilioni , isitoshe nani amabye hajui tanzania hawako serious na kitu chochote ? juzi juzi hapa wameleta ishu ya kusahili namba sasa iko wapi ? hamna kitu , hizo stika kwa taarifa yako zinauzwa maduka ya spea za magari kibao bei chee chee tembea uone , bahati nzuri au mbaya sina gari ila ningenunua tu hapo ....

    kazi kwenu wahusika...

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni njia nyingine ya kuendeleza matumizi baada ya matumizi yaliyokusudiwa kuwa yamejitosheleza. Binafsi kama karatasi haikutumika kwa mambo ambayo ni ni ya siri kama hili na ambayo hata namba hazijawekwa sioni ubaya kutumika kwa matumizi mengine kama ulivyofanyiwa. Watanzania au niseme waafrika tulio wengi tunapenda kumiss use au kutumia vibaya resorces. Watu mnasema tuhifadhi miti wakati end result yake ndio hiyo. Hapo utakuta ni mchina kafungua kasehemu ananunua unwated papers anaserve purpose nyingine. ANYWAY NISIENDE NJE YA JAMBO LKN NINAHITAJI NAMBA ZA CLOUDS FM TAFADHALI ANDIKA TU HAPA NITARUDI KUCHECK.

    ReplyDelete
  4. Mtoa Maoni #3 uwe unasoma post vizuri kabla hujatoa maoni yasiyo kuwa na kichwa wala miguu!!

    Private CARDS!

    ReplyDelete
  5. HATA HIZO STIKERS ORIGINAL MBONA HAZISAIDIA KUPUNGUZA AJALI? STICKERS ZA USALAMA BARABARANI ZINAUZWA TU MITAANI KIASI KWAMBA HATA MTU AMBAYE HANA GARI ANAWEZA KUNUNUA. POLISI WA USALAMA BARABARANI WENYEWE HUWA WANAUZA TU HUKO BARABARANI TENA WANAWEKA NA JUU.

    KWA UFUPI STICKERS ZA BARABARANI NI MRADI WA WATU WA KUKUSANYA PESA NA WALA SI KWA AJILI YA KUSAIDIA KUPUNGUZA AJALI BARABARANI. VIONGOZI WA SERIKALI WANAJUA SANA HII NA KAMA ILIVYO KAWAIDA YAO HAWACHUKUI HATUA YEYOTE ILE. NA HAWAITAJI KUCHUKUA HATUA KWANI WAKIOMBA KURA ZA UCHAGUZI WANASEMA TUMEFANIKIWA KITU FULANI HATA KAMA SI KWELI NA WATANZANIA WALIO KWENYE MKUTANO WANAPIGA TU MAKOFI MENGI TU NA KUSEMA USHINDI NI LAZIMA.

    ReplyDelete
  6. Ankali kutokana na ka ujuzi kangu kadogo ka mambo ya utambuzi na mambo ya forensic nimegundua kuwa kosa lipo kwa wachapishaji wa nyaraka hiyo kwani kuna kitu kinaitwa disposal of printed matters ndicho ambacho hakikuzingatiwa hapa uliyemkuta nacho ni yule ambaye huenda kununua printed matters zilizo kuwa disposed isivyo na kuzitumia kufungia bidhaa za wateja wake bila kujua kuwa kuna athari kwa upande mwingine.

    ReplyDelete
  7. AFADHALI MDAU UMEWEKA ISSUE YA STICKER HAPA!!! HUU NI WIZI MCHANA KWEUPEEEE TENA KWENYE TAASISI NYETI KAMA POLISI ILIYOPASWA KUZUIA VITENDO KAMA HIVYO. NASEMA HIVI NIKIWA MHANGA WA MCHEZO HUU MCHAFU! NENDA PALE O'BAY POLICE STATION, PAKI GARI LAKO NJE, INGIA OFISINI YA RTO JIELEZE KUWA UNAHITAJI STICKER, WANAWEZA KUJA KUKAGUA GARI AU WAKAANGALIA KWA MBALI TUU HALAFU "ANAKUUZIA" STICKER! AJABU NA WIZI WENYEWE UTAONA KUWA STICKER ZIMEANDIKWA BEI NI 3,000 LAKINI WAO WANATAKA 5,000 HALAFU HAWATOI RISITI ZA SERIKALI, SASA HIYO 2,000 INAKWENDA WAPI?

    ReplyDelete
  8. mbona nyingi tu zipo za deal...pia hata kama ni original survey ya haraka haraka asilima 90 zinatolewa sticker bila hata ya kukagua matairi kama ni vipara au laa, hivyo sticker za usalama barabrani hazihusiani kabisa na usalama wa magari,ni mojawapo tu ya source ya mapato....

    ReplyDelete
  9. Mtoa maoni no.4 kama wewe umeelewa mbona hujachangia ?kichwa wala miguu ya nani? usinichokoze watu, kwanza akili huna.

    ReplyDelete
  10. Mnagombana nini? hapa ni bongo, tumia ubongo wako uishi!

    ReplyDelete
  11. mimi wananishangaza Zain na BP kuwa sehemu ya wizi huu maana hizi zinatembezwa maofisini for TSh 7000!! Halafu mbona quality mbovu sana jamani? sasa nyinyi sponsors mmetoa nini maana printing cost ya sticker haizidi 400/-

    ReplyDelete
  12. Watu wote hapa wanazungumzia wizi.

    Je ukisikia kesho basi lilifeli breki likaua watu wote waliokuwapo, na mmoja wa hao labda ni wewe mwenyewe au ndugu yako au mtu wako wakaribu nakadhalika, halafu basi hilo lina sticker. Wakati kabla ya kupewa sticker hii breki ilitakiwa ikaguliwe, aliyekuuzia sticker angeweza kuzuia ajali hii kama angekagua na mwenye gari angeweza kuzuia ajali hii kama angeng'ang'ania gari yake ikaguliwe ili hitilafu kama hizi zienguliwe na kuepusha ajali kama hizi.

    Je hapa itakuwa ni uwizi ulitembea au ni uuaji wa makusudi ulitendeka?

    Sasa kiongozi gani aje kuzuia hii wakati sisi wenyewe tungeweza kulitatua hili tatizo?

    Tanzania haitabadilishwa na viongozi ila kila mmoja wetu ana wajibu na uwezo wa kuibadilisha tanzania kwa sehemu yake hata iwe kidogo vipi, at the end kibaba kitajaa mnajua tena kidogokidogo hujaza kibaba.

    Watanzania kesho mkisikia kwenye vyombo vya habari gari iliua kwa hitilafu kama hizo tafadhali msikimbilie kumsingizia Mungu eti ni mapenzi yake watu walikufa kwa sababu atachukia na kuwaadhibu.

    ReplyDelete
  13. Hii bongo ni balaa, vitu vingi vinanakiliwa kwa ujanja, kuna Road licence,kadi za magari nk, huwezi juwa ghafla illa wenyewe wakikukagua sawax2 watagunduwa,wiki ya usalama magari hayakaguliwi ipasavyo huo ni mradi wa Police na wakubwa zao!! Maana Zain na BP hutoa sticker zaidi ya Million 5 kwa TZ nzima, kuna za 3,000 gari ndogo, 5,000 gari za biashara na magari makubwa mpk 10,000, sticker mil,3 kila moja chukulia 3,000 ni Million 900 ni mradi wa vigogo!! huku mtaana ndio 5,000 hiyo 2 ni ya hao askari!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...