Lil Kim akijiachia vilivyo jukwaani, kwa raha zake isiyo na kifani na nguli wa muziki wa Bongofleva,Sir Juma Nature Jumamosi usiku kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,viwanja vya Leaders Club jijini Dar

Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Lil'Kim ambaye alitua hapa bongo kwa onesho lake moja ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse lililofanyika Jumamosi usiku katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar, na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali, ameahidi kuwa atarekodi baadhi ya nyimbo na msanii nguli wa Bongofleva Sir Juma Nature.

Lil'Kim akiweka bayana hilo jambo alipokuwa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Bw. Joseph Kusaga, amesema amefurahishwa sana na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwa Juma Nature na Watanzania kwa ujumla, hivyo ameahidi kurekodi baadhi ya nyimbo na Juma Nature zikiwemo remix za Mwanadada huyo mwenye manjonjo kibao awapo jukwaani.

Tayari Lil'Kim amechukua nyimbo kadhaa za Juma Nature na kuondoka nazo kwa ajili ya kuzifanyia kazi. Aidha Lil'Kim pia ameukubali sana muziki wa Kitanzania na namna Watanzania wanavyowakubali wasanii wao tofauti na sehemu nyingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ka Michuzi tuwekeeni hii shughuli kwenye youtube!!!

    ReplyDelete
  2. Nature anatisha..angekuwa huku unyamwezini ni level za kina-Jigga..Naona hadi huruma kwa maisha ya ufukara hao vijana wanavoishi wakati they are real superstars.
    check the video on this..

    http://www.globalpublishers.info/video/lil-kim-juma-nature

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Juma Nature, naamini hiyo inazidi kudhirisha uwezo wako ndani na nje ya Bongo.

    Video clip ya Juma Kassim Kiroboto aka Sir Nature na Lil Kim jukwaani hii hapa

    http://www.youtube.com/watch?v=9P4mazemkTs&feature=player_embedded

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    www.makulilofoundation.org
    www.scholarshipnetwork.ning.com
    San Diego, CA

    ReplyDelete
  4. Neema na izidi kuongezeka kwa watanzania wa Kikwete,hii inadhiilisha kuwa Juma Nature yuko juu,tumuombee isije ikwa ya Ms Sumary.Keep it up Juma Nature

    ReplyDelete
  5. juma nature aka kiroboto ni noma,wewe fikiri nature ndo watu wa mwanzo kwenye gemu,lakini hadi leo anakubalika,pia amesaiddia vijana wengi wa kitanzania.pia album yake ya nini chanzo ndo album bora ya bongo flava mpaka leo.inaongelea maisha halisi ya ki tz

    ReplyDelete
  6. Ah shemeji Lil Kim huyo anakuja ... kama vile Fally Ipupa na yule demu wa G Unit.

    Safi sana.

    ReplyDelete
  7. We saw so many of them now,They always come, say that and next day they gone. We never heard of them any more.
    So is the same story, the same bread, the same butter everyday.

    Ciao

    Mbagala

    ReplyDelete
  8. Naona Lil' Kim amechonga pua yake kisawasawa. Amenikumbusha marehemu Michael Jackson.

    ReplyDelete
  9. Jamani yule Mwimbaji wa Reggae aliyewahi kuja bongo na Kusema kuwa amechukua beats za "MIKASI" ya Ngwea kwenda kufanyia kazi, Je naye ameishia wapi? Hatujasikia kitu tena. Ngweair mwenyewe naye bado yupo yupo tu

    ReplyDelete
  10. Unajua kila kitu kina wakati wake unawezaukaona kama utani vile lakini ndo mtu anatoka hivyo Juma endelea kupiga kazi kwa bidii maana bidii haimtupi mtu one day utatoka tu, Hiyo ni dalili ya kwamba haupo mbali na uhalisia wa mambo!

    ReplyDelete
  11. Lil Kim albam yake ya mwisho alitoa lini?The Naked Truth (2005 ??)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...