Askari wa Usalama barabarani akimuokoa sasa hivi jijini Arusha mama mmoja (pichani kati) ambaye hakutambulika jina aliyetaka kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kumgonga mwendesha baiskeli na kuanza kumpiga vibao bila kujali amemuumiza wapi mwenye baisikeli ba kulilia gari lake lilokwaruzwa na mwendesha baiskeli huyo aliye mgonga. Wastaarabu wamekilaani kiitendo cha kumshambulia huyu mama ambaye ameonakana hakuwa na kosa. Habari na Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. "Wastaarabu wamekilaani kiitendo cha kumshambulia huyu mama ambaye ameonakana hakuwa na kosa.."

    Wastaarabu gani hao uchwara?! Kwa hiyo huyo mama kumzaba kibao mtu alieumia ndo ustaarabu. Kasahau uhai wa mtu kakimbilia gari.. ustaarabu wa siku hizi TZ huo! Shame

    ReplyDelete
  2. HAIELEWEKI, ALIYETAKA KUPIGWA NI NANI? MWENDESHA BAISKELI AU HUYO MAMA. KITENDO CHA KULAANIWA NI KIPI SASA MAMA KUMCHAPA VIBAO MWENDESHA BAISKELI AU MAMA ALIYETAKA KUPIGWA NA WANANCHI NA MWENYE MAKOSA NI NANI SASA, KIFUPI HAIELEWEKI IANDIKE TENA

    ReplyDelete
  3. Huu ndio tunaita ushabwa kipumbavu. Huyo mama unasema hana kosa ilhali kamchapa makofi huyo kijana?

    ReplyDelete
  4. NI MUHIMU KUTHAMINIANA KAMA BINADAMU, NA KUPENDELEANA MEMA, NA MAKOSA YANAPOTOKEA NI VEMA KUYATATUA BILA KUSABABISHA MADHARA ZAIDI YA VIWILIWILI AU MALI, NA SHERIA ITUMIKE KUMUONYA MKOSAJI ILI AJIFUNZE KUTOKANA NA KOSA BILA KUKOMOANA. NAMNA HII MAISHA YANAKUWA MAZURI.

    ReplyDelete
  5. Huyu maza analeta ubaunsa A town ; imekula kwake ! babakae

    ReplyDelete
  6. Sheria ya barabara inasema

    "A qualified driver owed duty of care to all(other) road user.

    Sasa sijui kama huyu mama sijui kama analijua hili. Ameshagonga hilo ni kosa la kwanza....Neglegence
    pili....anachapa vibao hiyo ni assault.
    sasa sijui kama atashtakiwa maana huko nyumbani nako ni Rule of Men inayofanya kazi sio Rule of Law ndio maana maendeleo yanakawia.

    ReplyDelete
  7. akina mama wababe hao,kamvunja mtu mguu anamsindikiza na mangumi akatibiwe zaidi ya mguu,tusiokuwa nazo tutakoma

    ReplyDelete
  8. hawa wakina mama ni wakuchapwa vibao! waendesha magari tanzania wakiwa ndani ya magari yao wanajiona kama wao ndo wameutoa maisha wengine takataka!! angecharazwa vibao ndo angeshika adabu

    ReplyDelete
  9. Toka lini ikawa mwendesha gari ndiyo ana makosa dhidi ya mwendesha baiskeli kwa polisi wa traffic

    ReplyDelete
  10. Huo ndiyo ujinga wa kuchukuwa sheria mikononi mwetu. Huyu mama wa watu angeuawa bure bila ya hatia. Inawezekana kabisa ni mwenye baiskeli ndiye mkosa lakini wananchi bila ya kufikiria wanataka kumuadhibu mwengine.

    Akina mama kwa asilimia kubwa huwa waangalifu wakati wanapoendesha magari na wala huwa hawaendeshi kwa spidi kubwa.

    ReplyDelete
  11. wewe ulieandika habari hii ulitakiwa kuifanyia editing ili ieleweke. "Wastaarabu wamekilaani kiitendo cha kumshambulia huyu mama ambaye ameonakana hakuwa na kosa" hapo mwanzo ulisema mama amemgonga mwendesha baiskeli na kuanza pia kumpiga kwa kuwa gari lake limepata mikwaruzo. Je Wastaarabu wanalaani nani sasa, wmenye baiskeli aligongwa na kupigwa vibao au mama aliyegonga na kupiga kijana huyo na watu wakaona siyo vizuri wakata kumshambulia huyo mama?
    Lakini kiustaarabu mwenye gari hatakiwi kumgonga mwenye baiskeli au mtembea kwa miguu. Netherlands ni nchi yenye waendesha baiskel kwa wingi, ukimgonga au mwenda kwa miguu itabidi polisi wajiulize umepata wapi leseni mpaka ugonge mwenye baiskeli au mtembeaji kwa miguu kwa maana kama una leseni ya kuendesha gari ina maana unajua kutumia barabara wale wengine hawajui ila wewe na hata kama katenda kosa hutakiwi kumgonga. Waendesha magari wengi Tz wanaendesha kwa kiburi bila kujali maisha ya watu wengine

    ReplyDelete
  12. Hakuwa na Kosa wakti yeye mwenyewe alijichukia sheria mkononi kumpiga aliyemgonga.. Au we unaona ni sahihi yye kumpiga aliyemgonga. Think clearly mjomba Woinde

    ReplyDelete
  13. Samahani, hebu tunaomba source of information aturekebishie kiswahili tuweze kuelewa hili tukio. Kiswahili hapa kimechanganywa sana, inakuwa vigumu kueleweka. 'Mama hakuwa na kosa' Je inamaanisha kwamba hakukosea kumgonga mwendesha baiskeli? Iwapo kama hakuwa na kosa la kumgonga mwendesha baiskeli, lakini kama alimpiga vibao, tayari hapo ana kosa kwani amejichukulia sheria mkononi, na huo ni udhalilishaji usiovumilika katka jamii iliyostaarabika.

    ReplyDelete
  14. Kweli Kiswahili cha Mwandishi Kimetupiga Nakata Mbwa Kona huyoooooooooo.

    ReplyDelete
  15. Stori nzima imekaa chakachua. Haieleweki nani kampiga kibao nani na mwenye kosa ni nani na wastaarabu ni nani. Yaani mtu habari utafikiri alikuwa kwenye mashindano ya kutuma yaani first in first out na hivyo alikuwa anamuwahi mtu mwingine asitume.

    Ushauri siku ingine kama una ka balckberry kako umeshachukua picha, kama huwezi kupreview kabla ya kutuma. Chukua kalamu na karatasi andika halafu usoma mara tatu kama unaelewa ulichoandika then type kwenye blackberry yako.

    ReplyDelete
  16. Mie naona huyu mama ndio ambaye hakua mstaarabu, yeye alichojua ni kuangalia gari lake bila kuangalia hali ya binadamu mwenzie kwanza. Wananchi walikua na haki ya kumshushia kipigo kwa unyama wake wa kutokua na ubinadamu kwanza wa kuthamini gari badala ya binadamu, hata kama mwendesha baiskeli alikua na kosa ila sio kigezo cha kumchapa vibao!

    ReplyDelete
  17. TAFADHALI MICHUZI, TUNAHESHIMU SANA BLOG YAKO , SO KABLA HUJATUMA CHOCHOTE NI VIZURI UKASOMA KWANZA ILI UWEZE TUMA KITU KINACHOELEWEKA NA KUSOMEKA. HII HABARI HAIELEWEKE KUWA ULIKUWA UNATAKA KUSEMA NINI.
    ANYWAYS, SHERIA ZA BARABARANI ULIMWENGUNI KOTE NA HASWA HUKO WANAKOTENGENEZA MAGARI ZINASEMA,DEREVA KWA DEREVA WAKIGONGANA BASI KUNA MMOJA ANAKOSA BUT UKIMGONGA MWENDESHA BAISKELI AU MTEMBEA KWA MIGUU JUA KUWA WEWE NDIO MWENYE KOSA NA HATA KIFUNGO UNAWEZA KUKIONA NA KUFUNGIWA LESENI. UNAPOKUWA DEREVA NI WAJIBU WAKO KUWA MUUANGALIFU SANA BARABARANI. HII INASIKITISHA SANA, MI NAWALAUMU TRAFFIC, POLICE KWA KUTOFUATA SHERIA. NA PIA HAO INSTRUCTOR WA MAGARI INAWE3ZEKANA HAWATOI MAFUNZO MAZURI KWA WATU WANAPOJIFUNZA MAGARI..
    INASIKITISHA SANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  18. kingangitiAugust 07, 2010

    Eh!kazi kwelikweli mithupu.Tunajua unatingwa kwa kuediti story kibao, lakini uwe makini si unajua ribrogi letu riko juu wazi muda hautoshi.Nilitaka kutetea lakini nimeshindwa hasa baada ya ingwe ya pili kusema," Wastaarabu....kumshambulia...hakuwana kosa.!? wakati yeye ndo kamshambulia kijana wa watu na hao walikuwa tu katika hatihati kutaka kumpiga.Hata hivyo hewala kaka Kiswahili kigumu jamani.Mfano.Nilimkuta hayuko..!, n.k

    ReplyDelete
  19. sheria mkononi si kitendo kizuri kwa namna moja au nyingine, lakini kitu cha kujiuliza kwa nini watu wamefikia hapo?

    hawa jamaa zetu wanajiita usalama wa barabarani hawana jipya, kwa mnyonge subiri kilio, huyo mama kwa kuwa ana hiyo gari basi akaona huyu mwenye baiskeli hana lolote, kwanza kwa dereva ambaye anatambua sheria za barabarani, waweza kuta mtu ambaye wewe wategemea ni mzima kumbe anamatatizo ya kimwili, aidha kiziwi na kuna matatizo mengi ambayo tunatakiwa kwa wale wanaoendesha magari wawe makini, barabara sio kwa ajili ya magari peke yake, kuna wanyama nao pia wana haki ya kutumia.

    ReplyDelete
  20. sheria mkononi si kitendo kizuri kwa namna moja au nyingine, lakini kitu cha kujiuliza kwa nini watu wamefikia hapo?

    hawa jamaa zetu wanajiita usalama wa barabarani hawana jipya, kwa mnyonge subiri kilio, huyo mama kwa kuwa ana hiyo gari basi akaona huyu mwenye baiskeli hana lolote, kwanza kwa dereva ambaye anatambua sheria za barabarani, waweza kuta mtu ambaye wewe wategemea ni mzima kumbe anamatatizo ya kimwili, aidha kiziwi na kuna matatizo mengi ambayo tunatakiwa kwa wale wanaoendesha magari wawe makini, barabara sio kwa ajili ya magari peke yake, kuna wanyama nao pia wana haki ya kutumia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...