Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa Dodoma Fatma Tawfiq alipowasili katika uwanja wa ndege Mkoa wa Dodoma jana.katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. James Msekela.
Kikundi cha ngoma ya asili cha wakina mama mkoani Dodoma kikitumbuiza mbele ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kushoto) alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Dodoma katika muendelezo wa ziara zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
(Picha na Mwanakombo Jumaa-Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hi, Mkurugenzi wa Blog ya Jamii, mtandao wako umekuwa wa mhimu sana katika kuihabarisha jamii kwa kuwa na habari za kila namna hata za siku za kuzaliwa za watu, huu ni mfano mzuri kwa kuwa unajaribu kukidhi na kuipa nafasi ya kila mwanajamii. Mi kama mwanajamii nimekuwa nikipitia katika media yako kupata habari kila mara na kwa kuwa Blog yako imeweza kuleta habari mbalimbali basi kila mara mtu hupenda kupitia na kuona wapi kutakuwa kumetokea nini.

    Utakubaliana na mimi pia kuwa kwa sasa maendeleo ya kampeni za uchaguzi ndo zinachukua nafasi kubwa katika vyombo karibu vyote vya habari. Kuna hali naiona katika Blog ya Jamii ambayo siyakawaida sana na tafsiri ya haraka ninayopata ni kama vile wahusika wake wanamlengo wa chama fulani au wameelekezwa kufanya hivyo kwa sbb pengine Blog hii inasomwa na watu wengi. Samahani Mkurugenzi mimi si mtu ninaye keti mahala pa juu zaidi ya mmiliki wa chombo hiki isipokuwa ni msomaji tu wa Blog yako. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa umeweza kutuhabarisha matukio kutoka kila kona ya TZ hata Nachingwea kwetu ambako umeme na internet ni shida lakini matukio mengine kama hayo imekuwa agharabu kuonekana hapa, kulikoni Mkururgenzi?!

    Naomba kuwasilisha

    Msomaji wako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...