Tume ya Mawasiliano kwa ung'eng'e Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) linavyoonekana toka Chuo Kikuu cha University of Dar es salaam. Jengo hili ambalo lipo pembeni ya barabara ya Sam Nujoma road itokayo Ubungo kuelekea Mwenge jijini Dar ni mojawapo ya majengo marefu yaliyojengwa nje ya kati ya jiji na kuwa mfano mmojawapo bora wa kupunguza msongamano wa watu na magari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hivi jamani hilo ni vumbi, moshi au type nyingine ya pollution iliyotanda juu ya jiji la Dar...something need to be done! Yani kijani haionekani kabisa ni moshi moshi tu umetanda angani watu wataanza kuugua kifaduro sasa hivi!

    ReplyDelete
  2. We wa kwanza hapo juu acha ushangingi maneno mengi badala ya kusifia kilichofanywa unatafuta jambo tu...Stop being negative for everything......Wee hujaishi Dar ndio maana ...kwani hujui humidity hiyo...Hiyo ni kwa vile wako karibu na bahari..Mbona Minnesota sehemu nyingi kunaoneka hivyo hivyo ukipiga picha wakati wa summer na haufungui mdoomo...Kaa kimya kama hujui jambo

    I like the building na ni mfano mzuri uliofanywa kujenga nje ya city center.....

    ReplyDelete
  3. Mbona jengo lenyewe limelala kidogo kama leaning tower of Pizza? Au ndiyo camera angle hiyo?

    ReplyDelete
  4. Anon..comment ya kwanza lazima tu uwe mbeyaaa wewe..maaana kila kitu kifanyikacho Bongo wewe unaweka comments za kukiground as if huku uliko utumwani (US/UK) nchi ilijengwa siku moja...Elewa geographic climate..siyo kila kitu unacompare bongo na ughaibuni..we osha tu mavi huku..tuachie siye na kifaduru chetu kituuwe...we si unadhani bongo kila kitu kibaya..pole sana..we are having thrills here in bongo daily....

    ReplyDelete
  5. Anon 01:38, hiyo ndio bongo. Matatizo kila nyanja ihali wanasihasa wanatuambia maisha bora kwa ---------------

    ReplyDelete
  6. Kaka kuna makosa mawili matatu kwa kuwa ni blog yetu ya wanajamii hatuna budi kuyarekebisha. Moja umeandika CHUO KIKUU CHA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM na pili umeandika BARABARA YA SAM NUJOMA ROAD

    ReplyDelete
  7. wewe kessy kwani hujapata ujumbe? au wewe ni mwalimu ???
    nenda pale kwenye daraja la salenda bridge ukaote manyoya

    ReplyDelete
  8. Hapo wamepunguza foleni ya kutoka wapi? maana kama unatokea Kibaha, foleni inaanzia mbezi mwisho. Ukitoka pugu, inaanzia Gongolamboto. Ukitoka Bagamoyo, inaanzia Kabla ya Tegeta, Ukitoka Mbagala, inaanzia mbagala hukohuko!

    ReplyDelete
  9. Haki ya Mungu kuna watu wana majibu! Wee acha tu eti nenda pale salenda bridge akaote manyoya mwee! you have made my day, big up mdau!

    ReplyDelete
  10. Majengo MAREFUU, ... we mama mbavu zanguuuu!!

    Afu kuna mwengine anasema "... kwani hujapata ujumbe ..."). Mbavu zanguu tena! LMAO!

    Hayo ndiyo yafanyayo nchi iliyotakiwa kuwa yetu ipige hatua za kasi ya ajabu kurudi kinyumenyume! Ni kwa kuwa tu wengi wamewekewa mapazia katika majicho yao. Ndio, narudia kuwa wabongo wenti majicho yao yako TINTED ndio maana hawaoni mbali.

    Ebu sikiza, watu wanaoonekana kama 'wanakashifu' kila kinachoonekana chema, kwa mawazo yangu wana mchango muhimu sana katika maendeleo. Inabidi kuwashukuru.

    §Toeni vibanzz kwenye majicho wabongooo, serikali yenu ilitakiwa kuyafanya mengi zaidi ya hayo tokea siku nyingi. Ni sawa na mzazi ambaye kwa makusudi kabisa anaamua kutelekeza familia na kuendekeza ulevi, ulafi, na choyo iliyokithiri - kisha kufanya familia iishi kwa mlo mmoja kwa siku, na wanafamilia wakaona kuwa ni kawaida.

    Basi baada ya wachache katika familia hiyo kuonahali ilivyo kwa familia nyingine na kuanza kuwatonya mabroda na masista wao, mzee anaamua kuongeza chips dume kwa mlo wa mchana mbali na ile dina waliyozoea siku zote.

    Sasa wapiga boksi wanazidi kupiga kelele kwamba hiyo tu haitoshi, ndipo wanajitokeza wajuaji na kuunguruma, ' ... ooh, baba anajitahidi kutuhudumia, zamani tulikuwa na mlo mmoja lakini sasa kaongeza chipsi dume, angalia foleni kibao - sijui inaonyesha utajiri (LMAO!), ... n.k. mama mbavu zangu weeee! duh, n'sije n'kapelekwa MOI ya kiboxini babake!
    nt'akatwa masaa (yes, huku ni haqi bin haqi).

    oke, nisingependa kutia maneno mengi, zaidi ya kuwasihi wabongo washushe vioo (zile tinted) ili wapate kuona! Watu twaishi mara moja tu katika maisha. Ni vema basi tukaishi kwa raha, hakuna aliyezaliwa ili apate shida. Serikali za nchi zote zinawajibika kuwafanza wananchi wake waishi kwa raha. Nchi yenye neema kama Bongo inapaswa kupunguza adha ya maisha kwa kutumia neema hiyo ya utajiri wa asili.

    Muhusika wa hii bugolu, naomba uiweke hewani hii ndude, usiwe 'uza samaki' (seli fishi) ili unufaike nayo wewe peke yako!

    Japokuwa nimedhamiria kutorudi, bado nawapenda na nitaendelea kuwapa ushauri wa bureeee!

    Mdau kiboxinii!

    ReplyDelete
  11. "Kessy" lazima atakuwa ni mgeni wa hii blog au huwa akiingia humu haisomi vyema, maana hizo lugha za hii blog ni chachu za hii blog, ndo moja ya vitu vingi vinavyoiweka hii blog kuwa kubwa so far!

    ReplyDelete
  12. Nawewe nawe, maneno mengi eti tinted sijui nini, sijui sirudi, niko ughaibuni havihusiani na mada iliyowekwa hapa.

    Tunajua huwezi kurudi kwa sababu huna makaratasi na tupesa twako twa ku clean na kuwa security gadi huko uliko hujaweza hata kununua kiwanja bongo, na kila ukicheki vijana wenzio uliowaacha wanakimbikiza!!

    Kaa huko huko ufanye security gadi na uklina kwa sababu ukija bongo hutajua pakuanzia na hutaweza tena kurudi ughaibuni!

    ReplyDelete
  13. Wewe Anonym wa Tarehe Sat Aug 14, 06:00:00 PM, wewe ndio haswaa mlengwa. Macho yako yamekuwa TINTED na si siyeem mpaka umekuwa mpweef. Hiyo ni fakti. Ubaki na hizo asampsheni zako, eti kukosa nauli - sijui nini! Mimi na wengineo walioshusha vioo na kupata kuona mbele 'tunapeta' kwa ulaiiiin! Ni kaushauri tu kutaka kukutoa wewe na wengineo katika upweeef uliokithiri.

    ONDOA 'TINTED' kwenye majicho mwanangu.

    ReplyDelete
  14. Huna makaratasi wewe mzee wa tinted, eti wewe ndiye unayeona kuliko wote, si urudi basi kama kweli papers zimekaa sawa? Kama vipi tukuchangie nauli wangu uje japo kuwasalimia wazazi wako kule kijijini.

    Mimi nina uwezo wa kukulipia nauli uje na kupiga kura kabisa. Ntakusubiri Uwanja wa JKN nikupokee maana waweza kupotea mjini tangu ulivyopelekwa nje kusoma Masters yako miaka mitatu iliyopita tena kutokea bara na sio DSM basi unajiona umefika. Sijui umekwisdhajilipua au bado unaishi kwa kubangaiza maana student visa yako imeisha tangu mwaka jana.

    Wakorea na Waasia wengine wangekuwa na mtazamo kama wako nchi zao zisingeendelea. Kisha nyie mnaozamia student visa zenu zikiisha ndio mnawaponza wenzenu wawekewe masharti magumu ya Visa.

    Na kadegree kako ka master bado unaishia kufanya kazi za hovyo hovyo, mzungu gani atakupa kazi ya maana? Unalipwa kima cha chini, bills kibao mwishoe unakuja malizia frustrastion zako kwenye blogu.

    Eti sirudi, sirudi, kumbuka iko siku utarudi tu tena bila passport!

    Hebu mie nikawachukue wanangu beach walikokwenda kupunga upepo weekend hii! Salaam kwa vizee shift ya usiku!

    Bongo Tambarare

    ReplyDelete
  15. KionaMbaliAugust 16, 2010

    Bradha.

    Hapa kuna kuhamia DODOMA tena kweli hapa!?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...