Mgombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Mh. John Mnyika akipokea fomu za kugombea Ubunge kwa jimbo hilo kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi jimbo la Ubungo,Bw. Gaudence Nyamwihura katika ofisi za Manispaa ya Kinondoni leo.
Mh. Mnyika akionyesha Fomu alizozichukua leo.
Mgomea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh. John Mnyika akiwa ameshikilia fomu alizozichukua mchana huu katika ofisi za Manispaa ya Kinondoni huku akiwa amezungukwa na wajumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kijana huyu hata angekuwa mgombea binafsi mimi na familia yangu tungempigia ata kama imefutwa!yani, uwezo anao, nafasi anayo na moyo anao. tuliokuwa nae mbuyuni primary, tambaza na UDSM twamjua fika hy kijana. Go brother. huu ni wakati wako JJ. May God be with you wezi wa kura wasifanye mambo ths time!

    ReplyDelete
  2. heeee!huyu kijana kumbe ni handsome hv!Mungu akubariki

    ReplyDelete
  3. MZEE WA BUNJUAugust 13, 2010

    HUYU NDIO RAISI WANGU AJAYE INSHAALLAH, KIJANA MAKINI SANA HUYU, SAFU YANGU ITAKUA KAMA HIVI

    RAISI - JOHN MNYIKA
    WARIRI MKUU- MAKAMBA JNR
    UCHUMI- ZITTO KABWE
    MAKAMU WA RAISI- HALIMA MDEE

    NISAIDIENI NIMUWEKE WAPI NAPE MNAUYE

    ReplyDelete
  4. KAKA MICHUZI UNABOA NA HABARI ZAKO ZA CHADEMA KILA SIKU. TOKA WAMEKUTISHA BASI UNA BEND TO THEIR PRESSURE. MBONA CUF HABARI ZAO HUWEKI? AU NDIO UNAOGOPA KUITWA MDINI? HAO HATA UKIWAFANYIA VIPI HAWATAACHA KUSEMA. NI USHAURI WA BURE TU UKITAKA CHAPISHA HUTAKI FICHA

    ReplyDelete
  5. songa kaka, bila shaka umekomaa sasa, na kilichokuangusha 2005 umeshakiona, kwa hiyo safari hii kifanyie kazi.

    ReplyDelete
  6. Vaa magwanda dogo, CHADEMA hakuna ubrazameni.

    ReplyDelete
  7. Nilichokupendea Michuzi ni kuwa umeona mbali, baada ya kuchungulia umeona kuwa CHADEMA wanaenda kuchukua ikulu mwezi wa Oktoba. na wewe kibarua chako cha Usa---- unaweza kukikosa na vijisafari vya hapa na pale utavikosa na vitakuwa kwishne. sasa unaanza kutupamba,hahahahahah kaza buti ndugu yangu tunaweza kukupa kazi ya ukatibu kata wa CHADEMA tawi la kunduchi.
    mdau Paka la jikoni.

    ReplyDelete
  8. Good luck John Myika.

    Uwezo unao, nia unayo na sababu unayo ya kuwa mbunge.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  9. Kijana. Kura yangu ya ubunge nitakupa lakini urais nampa mkuu ambaye ni handsome kama wewe na si mwingine bali JK. Nyote wawili mna mvuto. Siwezi kumpa kura yangu FREEMASON. No.

    ReplyDelete
  10. Tuweke pembeni ushabiki wa vyama tuangalie watu wanaoweza kule changamoto mpya kwa maendeleo ya jiji la Dar es salaam, kijana huyu anastahili kuwa mbunge, msikilize anavyojieleza kwa kujiamini, anvyosimama na kusema bila woga kero zilizopo, wabunge wengi wa Dar waliopita hawajaweza kupambana na kutafuta ufumbuzi wa kero nyingi hapa Dar, mfano mkubwa pale Ubungo, mabilioni ya shilingi yanavunwa kwenye kodi za mabasi, magari binafsi, taxi, abiria na wasindikizaji kila siku ya Mungu lakini sio mbunge wala diwani au kiongozi yoyote aliyekuwa anajaribu kufungua domo kuulizia hilo mpaka PM alipoenda mwenyewe!!!! Tunahitaji mtu kama huyu jamani!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Kama ana mvuto na unampenda sana kanywe nae chai. Uongozi sio sura

    ReplyDelete
  12. jj kaza buti tupo nyuma yako kura utapata labda waziibe km walivyofanya 2005 na siku zote mafuta hujitenga na maji,uongozi unauweza na hakuna kuangalia nyuma,tunahiaji mabadiliko ubungo!unakumbuka enzi za Yuna,Fhi?
    go mazee!


    zawadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...