

Novatus Makunga,Karatu
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani hapa wamemlaki kwa maandamano makubwa pamoja na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Karatu kumlaki mgombea wa ubunge wa chama hicho katika jimbo la hili ambalo limeachwa na katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa
Slaa aliyeamua kujitosa katika urais ameliongoza jimbo hilo tangu mwaka 1995 baada ya kujiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na jina lake kuenguliwa baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge kabla yake Patrick Qorro.
Mgombea huyo ambaye ni mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini (KKKT) katika jimbo la Karatu mchungaji Israel Yohana Natse alisema kuwa amejitosa katika ubunge ili kuitumikia jamii kwa upana zaidi.
Alisema kuwa kutokana na kushirikiana na mbunge anayemaliza muda wake Dk Slaa katika miradi mbalimbali amejipima na kubaini kwamba ana uwezo mkubwa na kuwaongoza wananchi wa Karatu.
“Ninachoweza kukwambia ni kwamba viatu alivyoviacha Slaa nina uwezo mkubwa wa kuvivaa pengine hata zaidi ya Slaa kwa kuwa miradi mingi tumeisimamia pamoja,"alisema mgombea huyo.
Alileeza kwamba kipaumbele kwake kitakuwa ni elimu kuanzi ya ngazi ya chini mpaka elimu ya juu na hasa mchakato ulioanza wa kuanzisha Chuo kikuu cha Karatu ambapo yeye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya chuo hicho.
Alisma kuwa Chuo hicho kitachukuwa majengo ya shule ya sekondari ya Karatu huku shule hiyo ikiamishiwa eneo la Ganako.
Aidha alisema kuwa ataendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha Chuo cha uuguzi na uganga kilichopo katika hospitali ya serikali wilayani Karatu ambacho pia ni mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa chuo hicho.
Katibu wa CHADEMA wilayani Karatu Laurent Bother alisema kuwa kuwa katika kumchagua mgombea huyo walizingatia uwezo wake katika kutekeleza katika ngazi ya jimbo na taifa yote yaliyoachwa na mtangulizi wake jimboni humo.
“Hata ukiangalia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza ni uthibitisho wa kwamba hali hii inaondoa dhana ya wapinzani wetu kwamba mikutano yetu inajaza watu kwa ajili ya helikopta
Alisema kwa chaguo hilo jimbo hilo kuchukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ni ndoto.
Awali wanachama wa chadema katika jimbo hilo walipinga vikali uamuzi wa Slaa kuacha jimbo na kwenda kugomba urais kabla ya yeye mwenyewe Dk Slaa pamoja na viongozi mbalimbali kwenda jimboni humo na kutoa ufafanuzi wa uamuzi wake huo
HIVI NYIE CHADEMA HAKUNA WAGOMBEA ZAIDI YA EWACHUNGAJI,WEKENI VIJANA UIBADILISHE NCHI,NAWASHAURI WA TZ WAWACHAGUE VIJANA KWENYE MAJIMBO,WASIANGALIE CHAMA,HAWA WAZEE WASIGEUZE BUNGE SEHEMU YA PENSENI
ReplyDeleteCHADEMA WENDAWAZIMU,KARATU NDO SAHAUNI,HAPO NI CCM BILA WASIWASI.
ReplyDeleteDALILI ZA CCM HIZO KUCHUKUA JIMBO
ReplyDeleteHIVI HAWA WACHUNGAI WOTE WANAKIMBILIA CCM NA MAKANISA WANAWAACHIA NANI,UHUNI MTUPU
ReplyDeleteJamani msiwahukumu watanzania kwa dini zao. Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alishayasema haya. Tanzania haina dini bali watu wake wanayo dini.
ReplyDeleteKama ni suala la uzee, vipi utatatueleza nini kuhusu akina KINGUNGE NGOMBALE MWIRU?
kaka Michuzi hizo comment nne za mwanzo zote zimetolewa na mtu mmoja mwenye mlengo wa kidumu chama cha M. CHADEMA watashinda karatu kwani ni jimbo lao hakuna ubishi na umati wa watu hapo kwenye picha ni ushahidi tosha.
ReplyDeleteComments zinafurahisha!!!!!!!!!, Anko endelea kuzitoa.
ReplyDeleteCha ajabu, hili jimbo ambalo linashikiliwa na upinzani linampango wa kuanzisha chuo kikuu?? yaani Mlimani nyingine huko Karatu!!!!!!!!!
Nadhani CCM wataliogopa hilo jimbo. Hiyo kasi ya maendeleo iliyopo huko jimboni nadhani inatisha.
Watu wa Karatu na Moshi mjini wanajua umuhimu wa kuchagua wabunge kutoka CHADEMA,ni maendeleo kwa kwenda mbele.Toka vyama vingi vianze hakuna chama twawala. ndio TWAWALA.
ReplyDeleteSasa ukisikia mchungaji anazikimbia roho za kondoo wake anakimbilia kwenye siasa huko ndiko kuchakachua. Lo. Aondoke padri aingie mchungaji. CHADEMA in Karatu you are finished. CCM inachukua kiualaini. Huyo mchungaji sisi tunamjua na anazo kashfa kibao.
ReplyDeleteHawa wachungaji kukimbilia Siasa ndio nini? Je, wamestaafu uchungaji? Manake wasiingize Siasa kwenye Dini. Kuna yule mchungaji wa CCM kule mbeya, na kulikuwa na Mchungaji mwingine anagombea kule Dodoma mjini lakini ameanguka vibaya. Jamani bakini kwenye dini
ReplyDeleteMbona Menegoha Mkuu wa ELCT(Evangelic Lutheran Church of Tanzania) alipigania ubunge zaidi ya mara mbili hakupitishwa na CCM ingawa alikua anatoa michango mikubwa kwa kwenda mbele. Sasa hivi amerudi tena huko baada ya kustaafu kuomba CCM wampitishe sijui amepata. Kweli mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu. Mambo ya Karatu wanajua wanakaratu wenyewe wawo ndio wanalala na kuamka kuona maendeleo yao hizi kelele nyingine acheni chagueni watu watakaoendeleza majimbo yenu.Hizi propaganda hazitusaidii chagueni mtu kwa uwezo sio itikadi au anafananaje.
ReplyDeleteTuache kupingana kwa sababu ya dini na makabila ya watu.
ReplyDeleteMtu anayeweza kutuongoza hata kama hana dini tutaupima uwezo wake.
Naona hoja ya miradi aliyosimamia haiangaliwi tunaona tu udini.
HII ZAMBI YA UDINI HAITATUACHA SALAMA.
Viatu vya SLAH vimepata mvaaji.
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza anasema CHADEMA inaweka wazee?Ni chama kipi haswa hakina wazee?CCM?CUF?
ReplyDeleteACHA UJINGA.
Wazee tutawapinga tu kama hawatusaidii sio tuwapinge tu kwakuwa ni wazee.
Baba wa Taifa MWENYEHERI Nyerere bado kidogo atakuwa MTAKATIFU.
ReplyDeleteKaratu katoka Padri Slaa sasa anakuja mwingine.
CHADEMA mbona hamna aibu kabisa.
Kwa mwendo huu ni aheri ya CCM na rushwa yake kuliko nyinyi na UKABILA na UDINI.
Chama kinaendeshwa kama kampuni binafsi.
Mkutano mkuu haujaamua tayari Padri Slaa kesha anza kampeni kuwaiga CCM hivi wajumbe wakimkataa inakuwaje?
Leo wanawake nao wameanza kukataa kuburuzwa na kuwekewa watu na viongozi.
CHADENA kwa kutaka ukubwa sasa ndiyo mtadhihirika zaidi udhaifu wenu na hasa huo mpango wenu wa kuchukua makapi ya CCM mtaona maana ukiona mfupa umemshinda fisi ujue hakuna wa kuweza.
Au ndiyo staili yenu maana hata Padri Slaa si alikuja baada ya kufungiwa milango na CCM isije kuwa nyote ni maslahi tu haman chochote maana na ile kauli ya M bowe Jangwani kwamba lazima waingie ikulu hata kwa kuiba kula inatisha.
Jiandae ndiyo kwanza kazi inaanza.
MIMI NAFIKIRI SUALA LA UDINI HAPA TULIACHE MAANA HATA SII SII EMU WANAYE MCHUNGAJI LWAKATARE NA YULE WA MBEYA NA WENGINE KADHAA. CHA MUHIMU HAPA TUANGALIE SUALA LA MAENDELEO. MNACHOTAKA KUMAANISHA NI KUWA VIONGOZI WA DINI HAWAWEZI KULETA MAENDELEO? SIYO KWELI. TENA WANKUPA MAENDELEO YA KIROHO NA KIMWILI KWA MAANA YA HUDUMA ZA KIJAMII NA KIUCHUMI - MAJI, SHULE, BARABARA, HOSPITALI. ANGALIA SHULE NA HOSPITALI ZINAZOMILIKIWA NA TAASISI ZA KIDINI NI UBUNIFU WA NANI? NA PIA ANGALIA VYOMBO HIVYO (SHULE NA HOSPITALI) VINAVYOPERFORM VIZURI UKILINGANISHA NA VYA SERIKALI YA SII SII EMU. NAMALIZIA KWA KUSEMA KARATU MMELAMBA DUME HUYO MCHUNGAJI NDIYE RIGHT CANDIDATE KWA MAENDELEO YENU
ReplyDeleteWasichoelewa watu ni kwamba. Uchungaji ni moja ya elimu za juu sana. Uchungaji unahusisha elimu nyingi, utawala, falsafa, uchumi, saikolojia, uongozi na mambo mengine mengi. Ndiyo maana wachungaji wana uelewa mkubwa wa mambo mengi. Wanafaa sana kuongoza
ReplyDeleteWe Anon wa Tarehe Thu Aug 12, 08:43:00 AM. Mchungaji hatumpi kura yetu. No way. Huyo sisi wa Karatu tunamjua kimbelembele na kinyumenyume. Wana uswahiba na Slaa na wamefanya kashfa nyingi pamoja. Subirini tu mtasikia. CHADEMA in Karatu is finished. C'est fini mon ami.
ReplyDeleteHuyu anon wa Thu Aug 12, 08:25:00 AM,sijui anatumia sehemu gani ya mwili wake kufikiri.
ReplyDeleteAmeanza kwa kusema Nyerere ataitwa mtakatifu,akarukia kusema dr.SLAH alikuwa padre,anamalizia kwa kusema hii niaibu kwa CHADEMA.
Anataka kutuambia upadre wa slah, na nyerere kuitwa mwenyeheri ni mambo ya aibu na yamesababishwa na CHADEMA.
Iko wapi mantiki.
ACHA UPIM
Anon wa Thu Aug 12, 08:25:00 AM,ametawaliwa na udini sana.Eti ni heri tuchague CCM na rushwa yake kuliko CHADEMA kisa SLAH ni padre.
ReplyDeleteTukianza kuchambua wagombea kwa misingi ya dini unadhani CUF na CCM watabaki salama?Umewaona wagombea wao wa urais wa muungano na visiwani?
Angalia hoja zako we PIMBI.