Joyce ni mtoto wa miaka 7,ambaye ana matatizo ya kichwa kujaa maji(hydrocephalus),ambayo imemsababisha asiweze kutembea kwani kichwa ni kizito.

Mtoto Joyce George anaomba msaada wa kununuliwa baiskeli ya walemavu na pia anahitaji kusaidiwa ada ya shule maalum,kwani mama yake hana uwezo wa kifedha.mtoto huyu kwa sasa anakaa Tabora na anategemea kuingia shule endapo atapata ada wakati wowote kuanzia sasa katika shule maalum ya jeshi la wokovu hapo Dar
Kwa sasa hivi mama yake mtoto Joyce anambeba mgongoni popote pale wanapokwenda,kwa hiyo angepata kwanza baiskeli itawasaidia sana, pia akiwa shule kwani atakuwa anakaa shule hadi wakati wa likizo,hii itampa mama huyu unafuu wa kuwatunza watoto wake wengine alionao wakubwa kuliko Joyce na pia kupata kupumzika kwani kazi anayofanya kwa kweli sio rahisi.
kwa maelezo zaidi mnaweza kuwasiliana na mama wa mtoto huyu ,anaitwa Flora Athumani kwa simu namba
0783607345 au 0755983262.
Mtoto Joyce anatafuta msaada kwa mtu mmoja mmoja au wafadhili kutoka vikundi na makampuni mbalimbali.ametoa bank details zake kama ifuatavyo Acc No. 2112501328,
bank ya NMB
CHALINZE BRANCH, PWANI.
jina lake kamili ni
FLORA ATHUMANI SAOKE.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mtoto Joyce anahitaji msaada, sio anatafuta msaada. Anayetafuta msaada (kwa ajili ya Joyce) ni mama yake au huyu msamaria mwema aliye leta hili Tangazo. Juhudi ilengwe kwenye matibabu pia, ili mtoto aweze kupona. Hima wana blog ya jamii, hayo ndiyo mambo muhimu ya kuchangia, sio kuchangia CCM!!

    ReplyDelete
  2. Salaam uncle Michu,
    Kwa nijuavyo mimi watoto wenye matatizo kama la huyu wanapatiwa matibabu bila malipo hospitali ya CCBRT Msasani Dar es salaam, hivyo kama hajapata matibabu ni vizuri akapata.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha kuona mama(familia) inaangaika kutafuta msaada kwa ajili ya mlemavu, kwa nchi za wenzetu hawa wenye matatizo maalumu kama haya ya ulemavu(disabled/phyisically handicapped)ni vulnerable group ambalo serikali kupitia social service inawapa kipaumbele kuwasaidia kupunguza ugumu wa tatizo walilonalo. FAMILIA HAIHITAJI KUTOA BAISKELI, au kugaramia gharama nyingine za matibabu, bali ni serikali ndiyo inayowahudumia. Nchi yetu imekwisha kazi ilipaswa ichukue jukumu la kuhudumia watu kama huyu kwa kumnunulia hiyo baiskeli na huduma nyingine kama kumpeleka shule maalumu, kumu entertain, nk. Ndio maana CCM tunaipiga chini mwaka huu, CHAGUA CHADEMA

    ReplyDelete
  4. This is sad, watanzania inabidi tujumuike na kusaidiana , huyu mtoto yupo bright na anaweza kujenga taifa na pia akaleta changamoto kwa sisi wote, naomba isiwe ni comment tuu, ila tuwajibike katika kumsaidia huyu mtanzania mwenzetu.

    ReplyDelete
  5. Jamani shule ya jeshi la wokovu ni bure pale kilwa road kama ninavyojuwa miaka ya 90. Na walimu walikuwa wa serikali, ninachojuwa ni kwamba misaada ni mingi sana wanapata lakini haiwafikii walengwa kama ipaswavyo. Hili ni tatizo la jamii yetu. Pole sana mpenzi jibu litapatikana mungu mkubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...