Mkurugenzi wa Masoko wa Precision Air Bw. Emillian Rweijuna (shoto) akitangaza ujio wa ndege mpya ya kampuni hiyo inayotarajiwa kutua nchini Agosti 26, mwaka huuu kutokea kiwandani Toulouse, Ufaransa. Ndege hiyo aina ya ATR72-500, itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 48 na ni ndege ya sita kati ya saba za aina hiyo ambayo Precision Air imeingia mkataba na kiwanda hicho kuwatengenezea. Na itapewa jina la 'Bukoba' kuwaenzi wananchi wa eneo hilo kwa kuwa pamoja na shirika tokea mqwanzo kabisa. Ndege hii itaifanya Precision air kuwa na ndege tisa za ATR na Boeing moja.
Precision Air Tanzania's leading airline in the country will take delivery of its sixth brand new ATR on 26th August 2010 in Toulous France.

The announcement was made by Precision Air’s Group Managing Director and CEO Mr. Alfonse Kioko at a press conference in Dar Es Salaam today.

"Preparations are underway to ensure all the necessary documentation is in place to enable the smooth delivery of the aircraft on 26th August and the ferry flight to Dar Es Salaam to commence the next day," Said Mr. Kioko.
The new aircraft- an ATR42-500 which will bear the registration 5H-PWF and the name Bukoba is scheduled to arrive at JNIA by the end of August 2010.
Like its predecessor, it will feature state-of-the-art inflight entertainment allowing the passenger to watch movies and listen to music during flight. The aircraft has the capacity to carry 48 passengers.

“This aircraft is named Bukoba in recognition of the business support we enjoy from the people from that region. In the recent past we have launched aircraft named; Kigoma, Zanzibar, Mwanza, Musoma to mention but a few.” He added.
PWF will be the sixth in seven brand new aircraft that Precision Air has ordered from ATR of France.
In 2006 PW and ATR signed a US $129 million deal to deliver seven brand new aircraft. The first aircraft (PWA) was delivered in March 2008 and the second (PWB) in November of the same year.
The third - PWC and fourth- PWD were delivered in April 2009 and July 2009 respectively while PWE was launched in March 2010. Under the terms of the deal ATR is required to deliver two aircraft each for the first two years and three in the final year. The final aircraft will arrive in September this year.

The financing deal of the seven aircraft (2 ATR 42-500s and 5 ATR 72-500s) has attracted two international awards. On April 20th 2009, Airfinance Journal awarded the US$ 129 million structured finance lease 'African Deal of the Year 2008' at the 10th Annual Deals of the Year Awards Dinner ceremony, held in New York.
The financing of the ATR fleet was already awarded last December, by Jane's Transport Finance magazine, as the "2008 Aircraft Leasing Deal of the Year in Africa".

The new ATR brings the total number of fleet to nine, six of which are brand new. Precision Air also operates a Boeing 737.

The delivery of the seven new aircraft has continued unabated and gone hand in hand with the increase in passenger uplift. The airline has the largest local network comprising; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Regionally Precision Air flies to Nairobi, Mombasa and Entebbe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. big up precision air...kwa kweli hii kampuni inastahili sifa inafanya kitu ambacho serikali imeshindwa hapo na ndege zake...hapo ndipo utajua ufisadi upo kiasi gani tanzania...watu wanakula tu mali ya taifa.

    ReplyDelete
  2. Heri ndege hiyo ingepewa jina jingine badala ya hilo la BUKOBA. Kwa vile ni chombo cha usafiri kama ilivyokuwa MV. BUKOBA iliyozama 1996, inaweza kuwatia hofu abiria wake kwa kukumbuka yale yaliyotokea kwenye MV.BUKOBA.

    ReplyDelete
  3. pelekeni zote bukoba na mkipata ndege ingine iiteni katerero!!!sisi wa kusini mnatuona hatuna nauli za kupandia ndege zenu.shame on you.

    ReplyDelete
  4. Aika Shirima. aika mmeku'a kwaka. Unaiweka Tanzania katika ramani ya aviation. Je ungekuwa haupo mambo yangekwendaje? KILA LAHERI. Ombi moja. Tafuta ndege moja ndogo ya kutupeleka nyumbani ROMBO. TUNAWEZA KUTENGENEZA RUNNING STREAP PALE MKUU. THINK ABOUT IT.

    ReplyDelete
  5. Jamanii Precision Kigoma vipi and congrates

    ReplyDelete
  6. Hongera PrecisionAir kwa kutoa huduma kwa vitendo na inshallah mtazidi kujitanua na kuizidi Ethiopian Airlines hapa barani Afrika, ndiyo inawezekana.
    Mdau
    Arusha.

    ReplyDelete
  7. Chaula, IpogoroAugust 11, 2010

    Nyie Precision mmetusahau sisi wa Iringa? Au mnatuona tumezidisha majungu? Basi siku hizi wenye majungu wote tumewaangusha katika kura za maoni, tuleteeni angalau ka-Twin Otter.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana kwa huduma yenu wakazi wa Bukoba tunawapongeza tangu kufa kwa ATC mmetusaidia sana kwani hata hilo jina la ndege hiyo mnajua Bukoba tulivyochangia, kwahiyo mchangiaji aliyesema watu wataogopa kupada tukikumbuka MV Bukoba ni mvivu wa kufikiria kwani bado Jina Bukoba lipo na sisi wakoba tunajivunia ukoo wetu, na meli bado tunapanda bila wasiwasi wowote,wenyeji wa Bukoba hatuwezi kumsahau agent wa shirika lenu marehemu Kajirita au binti yake Rose wamefanyakazi kubwa sana, ila tunaomba ndege kubwa zaidi sababu uwanja wetu umepanuliwa.
    Tunawashukuru sana .BUKOBA OYEEEEEEE.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  9. we rwejuna viwanja vya ndege viko wapi hapo bongo,unatangaza shirika linakua kivipi,
    mdau schoolmate shycom

    ReplyDelete
  10. Lakini huyu jamaa emilian anafanya kazi/anajitahidi.

    ReplyDelete
  11. WE MDAU UNAYE ISEMA SERIKALI KWAMBA IMESHINDWA NA PRECISION INABIDI UFAFANUE VIZURI KWASABABU SERIKALI HAIJASHINDWA NA PRECISION WALIOSHINDWA NI WATU WALIOKABIDHIWA KAZI YA KULIENDESHA SHIRIKA LA NDEGE, NA WASIPOANGALIA SHIRIKA LITAZIKWA MDA SI MREFU.

    ReplyDelete
  12. Precision Air ni 'national flag carrier' by their own standards. Ni aibu sana kwa taifa kutokuwa na chombo kinachomilikiwa japo kwa sehemu na serikali kinachoongoza shughuli za anga. Hawa jamaa wanauza shares, ni bora serikali kuondoa aibu inunue hisa nyingi tu ili nayo iwe na umiliki kwenye kampuni hii ambayo ndio inayotawala anga la Tanzania, sio kung'ang'ania ATC ambayo haina namna ya kujitoa ICU pamoja na maruzuku yote ya serikali!. Sio salama hata kwa usalama wa taifa. Imagine viongozi wangapi wa serikali wanalazimika kutumia chombo hiki kila siku? Je adui akijipenyeza humo ndani tutapona kweli? Mungu apishilie mbali. Wenye akili wanasema IF YOU CANT BEAT THEM, JOIN(BUY) THEM!!

    ReplyDelete
  13. Where is ATC??? shame on the TZ government kwa weli. Huyo anayesema ni watu walopewa majukumu to run ATC anasahau kuwa wanapewa kazi na serikali..that was a paraststal and the DG was a presidential apointee[tena wa mwisho[sijui kama mpaka sasa ndio huyo] if i remember correctly alishaharibu sehemu ingine nyeti pia! To add insult to injury nyie mnaowauliza Precision kwanini hawafiki maeneo yote, je ATC walikua wanaenda? Na je kuna viwanja? nadhani viwanja sio jukumu la Precision. Watanzania tujifunze ku appreciate efforts za wenzetu pale wanapofanikiwa roho za korosho ndio zimefanya nchi hii ifike hapa ilipo: PABAYA.

    ReplyDelete
  14. heee bukoba tena?kwani kanda ya ziwa ni wahaya tu?washashi na getegete mbona aka ndo kausafiri kao au mnawabagua?tena uwanja uko mwanza...mweeee
    ni kweli iringa imesahaulika kabisaaa na ule uwanja ushakuwa machunga ya mbuzi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...