Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mh. Joseph Kabila Kabange akiwa na ujumbe kutoka Tanzania baada ya Prof.Mark Mwandosya , Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania, kuwasilisha kwake ujumbe rasmi kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete shambani kwa Mhe Rais Kabila, Mekao km 150 kutoka mjini Kinshasa wikiendi ilopita. Kutoka kushoto ni Nd. Washington Mutayoba, Mkurugenzi wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya watu wa Congo(DRC), Mama Lucy mwandosya na Mhe. Gordon Ngilangwa, Balozi wa Tanzania DRC.
Alipokuwa Kinshasa Prof. Mark Mwandosya pia alimtembelea Mama Pauline Lumumba, mjane wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo, Marehemu Patrice Emery Lumumba,nyumbani kwake Gombe. Katika picha, waliokaa ni Mama Pauline Lumumba na Prof. Mark Mwandosya. Waliosimama kushoto ni Mama Lucy Mwandosya na kulia ni Juliana Lumumba, binti wa marehemu Patrice Lumumba, aliyekuwa waziri wa Habari na Utamaduni katika serikali ya Marehemu Laurent Kabila.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mark Mwandosya ( watatu kushoto) akipata maelezo kuhusu kituo kikubwa cha umeme kwenye Bwawa la Inga, mto Congo. Watano kushoto ni Mhe. Jose Endundo Bonange, Waziri wa Mazingira na Maliasili. Katika maporomoko ya Inga, yakiendelezwa, DRC ina uwezo wa kuzalisha MW 100,000 za umeme.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Duuh kumbe mawaziri bado wapo nilisikia kama jk amevunja baraza la mawaziri. labda siku sikia vizuri!




    Mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  2. Duuh watu wamejinyonga na matai na masuti halafu yanko yakupigia simpo tu kuonyesha huko kwenye ranch lake, good looking JOseph

    ReplyDelete
  3. Duh! Kumbe misopu fulanas umepata kongo? Kama yako vile

    ReplyDelete
  4. oh how nice kuona picha ya mke wa lumumba. LUMUMBA HEROES NATIONAL. history ya lumumba iandikwe na mke wake.

    ReplyDelete
  5. UKITAKA KUJUA HABARI ZA PATRICK LUMUMBA NENDA KATIKA YOU-TUBE UTAFUTE HABARI ZAKE ANDIKA TU CHIA LAKE KWENYE KISANDUKU CHA SEARCH UTAONA JINSI ALIVYOTESWA HADI ANAULIWA INATIA HURUMA. KUNA VIDEO KIBAO ZA LUMUMBA HUKO
    KWENYE YOU-TUBE INATIA HURUMA WAZUNGU SI WATU

    ReplyDelete
  6. ZEEEE FULANAz ini ze hausi!!!!Ankal kumbe Mjomba Joseph alikupigia pande kwenye ze fulana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2013

    Nimefurahi kumwona Mhe. Ngilangwa. Very respectful man, I salute you! ni kati ya watu wachache waliotumika kwa uadilifu wa kweli ktk Serikali ya Tanzania. Live long and remain blessed.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...