Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mh. Joseph Kabila Kabange akiwa na ujumbe kutoka Tanzania baada ya Prof.Mark Mwandosya , Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania, kuwasilisha kwake ujumbe rasmi kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete shambani kwa Mhe Rais Kabila, Mekao km 150 kutoka mjini Kinshasa wikiendi ilopita. Kutoka kushoto ni Nd. Washington Mutayoba, Mkurugenzi wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya watu wa Congo(DRC), Mama Lucy mwandosya na Mhe. Gordon Ngilangwa, Balozi wa Tanzania DRC.
Alipokuwa Kinshasa Prof. Mark Mwandosya pia alimtembelea Mama Pauline Lumumba, mjane wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo, Marehemu Patrice Emery Lumumba,nyumbani kwake Gombe. Katika picha, waliokaa ni Mama Pauline Lumumba na Prof. Mark Mwandosya. Waliosimama kushoto ni Mama Lucy Mwandosya na kulia ni Juliana Lumumba, binti wa marehemu Patrice Lumumba, aliyekuwa waziri wa Habari na Utamaduni katika serikali ya Marehemu Laurent Kabila.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mark Mwandosya ( watatu kushoto) akipata maelezo kuhusu kituo kikubwa cha umeme kwenye Bwawa la Inga, mto Congo. Watano kushoto ni Mhe. Jose Endundo Bonange, Waziri wa Mazingira na Maliasili. Katika maporomoko ya Inga, yakiendelezwa, DRC ina uwezo wa kuzalisha MW 100,000 za umeme.

Duuh kumbe mawaziri bado wapo nilisikia kama jk amevunja baraza la mawaziri. labda siku sikia vizuri!
ReplyDeleteMdau
kisiju pwani
Duuh watu wamejinyonga na matai na masuti halafu yanko yakupigia simpo tu kuonyesha huko kwenye ranch lake, good looking JOseph
ReplyDeleteDuh! Kumbe misopu fulanas umepata kongo? Kama yako vile
ReplyDeleteoh how nice kuona picha ya mke wa lumumba. LUMUMBA HEROES NATIONAL. history ya lumumba iandikwe na mke wake.
ReplyDeleteUKITAKA KUJUA HABARI ZA PATRICK LUMUMBA NENDA KATIKA YOU-TUBE UTAFUTE HABARI ZAKE ANDIKA TU CHIA LAKE KWENYE KISANDUKU CHA SEARCH UTAONA JINSI ALIVYOTESWA HADI ANAULIWA INATIA HURUMA. KUNA VIDEO KIBAO ZA LUMUMBA HUKO
ReplyDeleteKWENYE YOU-TUBE INATIA HURUMA WAZUNGU SI WATU
ZEEEE FULANAz ini ze hausi!!!!Ankal kumbe Mjomba Joseph alikupigia pande kwenye ze fulana
ReplyDeleteNimefurahi kumwona Mhe. Ngilangwa. Very respectful man, I salute you! ni kati ya watu wachache waliotumika kwa uadilifu wa kweli ktk Serikali ya Tanzania. Live long and remain blessed.
ReplyDelete