Mgomea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Dr. Willblod Slaa akimpa baraka zote na kumnadi wanachama na wapenzi wa chama hicho Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika katika kampeni zake za Jimbo la Ubungo na kumhakikishia kuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha wanashinda.
Mpendazoe naye alikuwawepo kumnadi Mnyika kwa wananchi wa Ubungo katika ufunguzi wa kampeni za chama hicho Kimara Suca.
Wasanii wa muziki wa Bongo Freva wakiongonzwa na mgombea Ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II (SUGU) wakilishambulia jukwaa la ufunguzi wa kampeni za Mnyika Kimara Suca

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. ASANTE MICHU KWA KUSIKILIZA KILIO CHA SISI TULIOKUWA TUNAHITAJI HABARI ZA VYAMA VYOTE VYA SIASA.

    MIMI BINAFSI NILIKUAGA SIPIGAGI KURA KWASASA NITASHIRIKI KIKAMILIFU HATA NIKIWA TIGHT VIPI, HAKUNA HAJA YA KUONGOZWA NA WEZI NIMEGUNDUA KUKICHUKIA CHAMA FULANI TUU HAITOSHI MPAKA UKINYIME NA KURA KABISA

    ReplyDelete
  2. Go brother. naimani tutafika mbali.

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu umenifurahisha sana! Ni kweli kabisa tunatakiwa tubadilike kifikra Watanzania. Simaniishi kwamba wapinzani wote ni wasafi na ndio wanaotufaa sana, hapana! Namaanisha tuangalie wale viongozi wa majimbo yetu ambao tunaona kabisa wana mwelekeo na nia thabiti ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu.

    Tusitegemee miujiza ishuke kutoka mbinguni kuja kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania. Ni sisi wenyewe ndio wenye jukumu hilo. Tukiendelea kukaa kimya na kuwaachia hao mafisadi waitafune nchi, watoto wetu watakuja kutulaumu sana!

    Evil exist in our society not because of the actions of bad people, but because of the silence of good people!

    Lets raise our VOICES and say No to corrupt leaders, it is possible play your part.

    ReplyDelete
  4. nilikuaga sipigagi! teh! te! teee!

    ReplyDelete
  5. HII MICHU KAOMBWA HAJATAFUTA YEYE ZA CHAMA TWAWALA ANAKESHA NAZO JUZI ALIKUWA RUKWA NA KIKWETE, NILIFIKIRI WASANII TU MPAKA BRO MITHUPU!!!!!!!!!!!!!!njiiiiiiii

    ReplyDelete
  6. watabana weeeeee mwishoni wataachia tu!!Walikiona kimanumanu kilichowatembelea majirani zetu,Hata Bongo kitawadia tu.

    ReplyDelete
  7. YOU ARE RIGHT ANA 12:16PM. NJIA NI KURA YAKO. KUKAA NA KULALAMIKA HAKUTOSHI NJIA NI KURA YAKO TU.

    ReplyDelete
  8. ukiwanyima kura umewanyima ushindi wa kishindo tuu si ushindi woote.

    inaweza kukuuma ukiwakusudia na bado wakakushinda na dukuduku lako shingoni.

    ReplyDelete
  9. Yes. Kura yangu ninampa JK

    ReplyDelete
  10. John karibu utusindikize...

    ReplyDelete
  11. CHAMA TWAWALA tehe hehe he!!
    Ila Bro Michu tuonyeshe basi na kusanyiko/umati lilivo mbona unaonyesha mbele tu???!
    Ubungo kwa Myika tuuu

    ReplyDelete
  12. Hata mimi kura yangu nampa JK.

    ReplyDelete
  13. He...hivi Mbeya pia kuna Wachaga?

    ReplyDelete
  14. watanzania wenzangu tusidanganyike ccm ni chama bora kwani sera zake ziko wazi ukiangalia vyama vya siasa vya tanzania sito taja kwa majina kwani sisi wana ccm ni wastaarabu hakuna sera wanazonadi zaidi ya ufisadi hatukatai ila ufisadi sio sera msidanganyike wanadi ilani za vyama vyao na jinsi zitakavyo saidia kuboresha maisha ya watanzania kwa ujumla sera za ccm ziko wazi kwa manufaa ya kila mtanzania vijijini na mijini 2010 chagua kikwete chagua ccm

    ReplyDelete
  15. annons "mbeya kuna wachaga?" na "John karibu utusindikize" mbavu zangu uwiiiii

    ila jamani ivi hawa vijana ambao hata HAWAJAOA na wanakimbizana na siasa ivi wanatafuta nn hasa??angalau basi tuone japo wana watoto wa mazoezi mtaani lkn wapi!!vijana tulizeni kwaza bolu anzisheni familia ndo muingie izi siasa za kifo za bongo
    (njoni nyamagana muone vitisho)

    ReplyDelete
  16. HATA MIMI HUWA SIPIGAGI KULA ILA NAHISI MWAKA HUU UTAKUWA NI MWAKA WA HAKI KWA KIASI FULANI SIO CHANGA LA MACHO KAMA TULIVYO ZOEA KWA HAWA WEZI WA KURA NA WALIOBOBEA KUHONGA KILA KUNA A.K.A WACHAKACHUAJI this time nitapiga kura tu hata niwe nimebanwa kiasi gani na hata msululu uwe mrefu kiasi gani lazima nipige kura TUMECHOSHWA NA HAWA VIONGOZI MAJAMBAZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...