Home
Unlabelled
vyama vya wafanyakazi vyatakiwa kutojihusisha na maswala ya kisiasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
nani kawadanganya kwamba vyama vya wafanyakazi haviruhusiwi kujiusisha na mambo ya siasa wakati wanasiasa ndio wanawapangia mishahara ya na maslahi yao?
ReplyDeletevyama vya wafanyakazi wana haki kujua ni mgombea gani atawafaa kwa maslahi yao na kila kitu.mekataa kura zao sasa mnataka kuwawaekea ubabe kwamba hawaruhusiwi kujihusisha na siasa kwani wao sio wananchi wa tanzania? mtu yoyote anayepiga kura anaruhusiwa kujihusisha kwenye siasa.
angalia nchi zingine unapokuta mwanasiasa anapata endorsement kutoka katika chama cha wafanyakazi fulani kwa vile anaendana na maslahi yao watu wame elimika na wanajua haki zao tusijaribu kunyanyasana.
Serikali inabidi ijue tanzania ya leo sio ya jana.
Kumpa 'pilau' Dr. Slaa ndio imekuwa kujihusisha na siasa?
ReplyDeleteBasi museme wafanyakazi hawana ruksa kupiga kura , ama kupiga kura sio kujihusisha na siasa?
(US Blogger)
Vyama vya wafanyakazi vina mchnago mkubwa sana katika kuchagua viongozi wataoweka maslahi ya wafanyakazi mbele. Sioni tatizo lolote kwa TUCTA kufanya hivyo. Kama vyama vya wafanyakzi wa nchi tajiri kama Marekani hufanya kampeni ya kumpigia kura mgombea wamtakaye, mfano walivyofanya kwa Obama uchaguzi uliopita. Na mara nyingi wanapendelea sera za Democrats katika chaguzi mbalimbali, wakiamini kuwa huwapendelea zaidi wafanyakzi wakiongoza nchi. Sisi ambao ni masikini ni kitu gani ambacho tunashindwa kufanya hivyo ? Au sababu inaelekea upepo safari hii hauvumi kule tunapopenda ?
ReplyDeleteVyama vya wafanyakazi ni moja ya interest groups katika nchi. Badala ya serikali kuogopa, inapaswa kupata changamoto zaidi, siyo kuboresha tu wafanyakazi, ila watanzania na nchi kwa ujumla.
Labda mimi sijaelewa vizuri, lakini inaonekana hafisa mkuu wa habari anaandika minute za kikao hicho. Ina maana alikuwa hana mpaka wakati huo taarifa kamili ambayo wizara ilikuwa inatoa kwa waandishi wa habari mpaka wakati huo ? Na yeye baada ya hapo waandishi wakimuuliza maswali zaidi kuhusu issue hiyo atawaambia nini ? Maana naye habari kwake ni mpya !! Kazi kweli kweli. Bado tuko mbali sana. Inawezekana tusijefika kabisa huko tuendako. Lakini hiyo picha hapo haijakaa vizuri kimaudhui.
Mwananchi.
Yeah I second you all up there...wamesahau kabisa Tanzania ya leo sio ya jana...
ReplyDeleteBongo bwana, kila kunapokucha kila afisa anaamka na yake mradi kuna vyombo vya habari kusikiliza kila upupu! nani kawaambia kuwa vyma vya wafanyakazi havina haki ya kujihusisha na siasa? Jiulize au rudi Mlimani mkajifunze "siasa ni nini?"
ReplyDeleteMimi ni mwanachama wa TUGHE sintakubali TUCTA inichagulie mgombea wanaomtaka wao. Kura yangu mimi nimeamua nitaendelea kumpa JK. Basi. Kwa nyinyi mlioko huko kwenye DIASPORA ambao mnamtaka huyo padre fu...ka shauri yenu.
ReplyDeletevyama vya wafanyakazi haviwezi kutenganishwa na siasa hata siku moja popote duniani....hata hapa kwetu watu mashuhuru kama HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA-SIMBA WAVITA alikuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi,vyama vya wafanyakazi vilishiriki siasa na harakati za kutafuta uhuru katika nchi nyingi tu duniana.
ReplyDeleteRais wa sasa wa afrika kusini Jacob Zuma ameshinda uraisi kutokana na support kubwa ya vyama vya wafanyakazi wa afrika kusini kupitia shirikisho la vyama vya wafanyakazi la COSATU.
WAZIRI MKUU WA ZIMBABWE AMETOKEA KWY VYAMA VYA WAFANYAZI NA KUINGIA KWY SIASA AMBAKO AMEPATA SUPPORT KUBWA KUTOKANA NA KUUNGWA MKONO NA VYAMA VYA WAFANYA KAZI.
CHAMA CHA LABOUR-HUKO UINGEREZA NI KUTOKANA NA KUUNGWA MKONO NA WAFANYAKAZI NDY MAANA VINASHINDA.
SERIKALI ISIWADANYE WALA KUWATISHA WAFANYAKAZI WA TANZANIA(TUKTA)-KAMA SERIKALI ILITELEZA KATIKA KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI IOMBE RADHI NA IJIPANGE UPYA.
VINGINEVYO TUTATUMA UJUMBE KUPITIA SANDUKU LA KURA MNAMO MWEZI OKTOBA.
Kwani serikali inachoogopa hasa ni nini? Enzi za nidhamu ya uoga zimekwisha mbona. Kila mtu si ana haki yakusema anachotaka ilimradi asivunje sheria hiyo ndio demokrasia. Mbona jumuiya ya wafanyakazi ilikua inajihusisha na siasa? Hizo sheria mpya zimeanza lini? Kama mtu unasimamia haki huwezi kuzuia watu kuwa na maamuzi yao.Msipoangalia watanzania nchi itageuzwa kuwa nyumba ya mtu unatunga sheria unapojisikia.
ReplyDeleteVyama vya wafanyakazi haviruhusiwi kama vyama vya wafanyakazi, kutaja jina la mgombea wa kumpigia kura. Pamoja na hayo wanaruhusiwa kutaja sifa za mgombea anayewafaa na sifa za mgombea asiyewafaa. Kwa mfano, wana haki ya kuambizana wasimpigie kura mgombea anayesema hazitaki kura zao, kama ambavyo kila mgombea ana haki ya kusema hataki kupigiwa kura na wafanyakazi.
ReplyDeleteMBONA CCM ILITOA FOMU ZA NAFASI ZA UBUNGE WANAWAKE VITI MAALUMU KWA VYAMA VYA WAFANYAKAZI? TANU ILIJIHUSISHA NA SIASA, NUTA NAYO ILIFUATA NYAYO NA TUCTA TANGU ILIPOANZA PIA ILIFUATA NYAO KUIPIGIA DEBE CCM SASA IMETOFAUTIANA NA CCM IMEKUWA KOSA! MBONA VYAMA VILIVYOKUWA VIKIIUNGA MKONO CCM HAVIKUONYWA? HUU NI UDIKITETA.
ReplyDelete