Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashililah akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Fedha ya Bunge la Korea Kusini, Mhe. Joyoung Lee. Wabunge wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Korea Kusini wako nchini kujifunza namna Bunge linavyopitisha Bajeti na kusimamia matumizi ya Serikali ambapo pia wamewasilisha ombi rasmi la kuanzisha kwa mahusiano
ya kibunge. Kwa upande wake, Dr. Kashililah alishukuru hatua ya Bunge la Korea Kusini kuomba uhusiano na Bunge la Tanzania na kuahidi kuliwasilisha kwa wabunge wapya mnamo mwezi Novemba.Wa kwanza kulia ni Nd. Emmanuel Mpanda, Msaidizi wa Katibu wa Bunge na Nd. Siegfried Kuwite, Mkurugenzi wa Idara ya Mipandgo Bungeni.

Picha na Saidi Yakubu wa Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mmewaonyesha na kuwafagilia kuhusu zile kompyuta zao?

    ReplyDelete
  2. Swali kwa wote: Hizi zawadi zinazotolewa kwa viongozi wa government, ni for personal use au ni kwa ajili ya ofisi? Kwa sababu hawa viongozi wanaweza kwenda nazo nyumbani baada ya kazi, wakati inatakiwa zawadi zibakie kazini. Kitu kama hiki kilitokea hapa U.S. wakati Bill Clinton alipomaliza muda wake, ilidaiwa kuwa aliondoka na zawadi alizopewa akiwa rais, na wananchi walitegemea zawadi zibakie White House, kwa sababu kiongozi wa government akipokea zawadi, ni ya umma/government. Tubadilishane mawazo please.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...