Timu ya Watanzania wanaoishi Wichita, Kansas, imetoa kipigo kikali kwa timu ya Watanzania wanaoishi Houston, Texas, kwa jumla ya magoli 4-1, katika mchezo uliochezwa Wichita, Kansas Jumamosi ya 7/8/2010.
Kwa ufundi mkubwa timu ya Houston ilitawala kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo, na kufanikiwa kujipatia goli la kwanza na la kuongoza katika dk ya 32 ya mchezo, mfungaji akiwa mshambuliaji wake hatari Peter Bategeki, goli hilo lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Wakati wa mapumziko, timu ya Wichita ilionesha kuchanganyikiwa na hali ya mchezo na kulazimika kufanya mabadiliko, ambapo yalibadilisha hali ya mchezo na kuifanya timu ya Houston kuanza kuonekana mdebwedo.
Mwiba kwa timu ya Houston alikuwa ni mshambuliaji hatari Idd Ligongo, ambaye alikuwa akiwasumbua walinzi wa Houston na kuwafanya washike kiuno kila mara, hali inayoashiria walikuwa hoi.
Katika dk ya 60 Idd Ligongo aliifungia timu yake ya Wichita goli la kusawazisha, dk 68 mshambuliaji huyo akafunga tena goli la pili. Dk ya 75 Musa Mbongo aliipatia timu ya Wichita goli la tatu baada ya kuitumia pasi safi toka kwa Idd, huku mshambuliaji Denis Mbelwa Rweikiza akiimaliza shughuli kwa kuandika goli la nne katika dk ya 82.
Kwa habari na picha zaidi tembelea
Kwa habari na picha zaidi tembelea
ama
www.tawichita.net.
wichita wakija DC tutawapiga bao kama wamesimama.tatizo lao wanataka kuchezea kwao tu.
ReplyDeleteShaali, Saidi na Diwani naona Mmemtesa Twailu, Du.
ReplyDeleteSandaly
huyu ni yulle Idi mtangazaji wa ITV...du kakimbia Tanzania..aisiii..kweli Tanzania shida sana ..sasa kwa nini watu wanakimbia...OK karibu USA kaka...fani yako ya utangazaji hapa sahau..hapa ni kuosha vizee mavi tu..na kuuza sandwiches Subway au kubeba box,...Whole Food,walMart nk...
ReplyDeletemdau wa tatu hapo juu umeniua nimecheka weee, kweli we umepinda
ReplyDeletedu bulu nyani nakuona hapo, upo maboksi yamekubali hivyo naona siha unayohaswa,
ReplyDeleteMdau wa aug9 04:43am.acha majungu sasa huku ULAYA kama tunaosha vizee sijui mavi,kupiga box,wewe kinachookuuma ni nini?sasa kwa taarifa yako hao watu unaowadharau MUNGU anawasaidia kuwapa kipato kizuri sana na wanaweza kufanya mambo makubwa sana huko nyumbanikuwasaidia familia zao na kuweka maisha yao vizuri kwa ujumla.Au walikunyima VISA nini ndo mana unachonga?acha hizo bwana wewe endelea kuchonga lakini tambua kwamba sisi tunasonga mbele na hatuna habari na habari za majungu hatupendi.Behave your self please!!!
ReplyDeleteMdau-Mji wa kusoma!!!
Wacha wafanye wanavyoweza Angalau Hawauzi Unga au Kukaa tu Majungu kama wewe. Mwenyezi mungu kaumba Dunia kwa Wote kachanganya watu kwa sababu zake, Riziki kwenye kila dini imeandikwa Tafuta kokote saidia wenzako kama alivyosema mdau mmoja angalau anasaidia kwao wewe una type majungu. Mungu azidi kuwafungulia Ndugu zangu huko Nje na Awalinde vizuri. Mkirudi mrudi Salama. MZ Iringa.
ReplyDeletemdau wa aug9 02:01:00pm...Asante sana.ujumbe wako umesomeka vizuri mnooo.Bless!!!
ReplyDeleteMdau-Mji wa Kusoma!!!
mbona mnamlaumu mchangiaji hapo juu yeye anajaribu kumkaribisha mshikaji na kumueleza ukweli kama hapo alipo maisha yanakwenda kwa kuosha vizee na wewe unamlaumu kwani kasema kazi ya kuosha vizee ni mbaya ama anamueleza ukweli wa maisha ya ughaibuni nadhani kama nimemuelewa yaelekea na yeye ni moja ya wafanyakazi wa hiyo kazi sidhani kama ni muuza unga...
ReplyDeleteMuosha vizee mzoefu
Safi sana Wichita! Lunda umenifurahisha na vuvuzela!!
ReplyDeletenaomba saana huu mjadala wa uoshaji vibibi uendeleee kwi kwiiiiiii
ReplyDeleteTimu ya Wichita hawana nauli,watafikaje Houston au DC ? Siku zote wanashindia uwanja wa home kwa kubebwa,tokeni tuone.Nyoooo !!!!!!
ReplyDeleteMuache Idd,haja leta u star wowote,Idd ni mtu mwenye determination,kama alicheza maigizo miaka hiyo,sasa hivi si Idd yule mcheza maigizo .Idd ana "determination ktk maisha" tatizo wabongo hawapendi kumuona mtu kaendeleea wanataka kila siku awe pale pale anacheza maigizo.Idd high five ,you are the man,you are the acheiver,usiwasiskile kuna watu mika kumi wapo kiwanja hawajaenda shule wala nini,halafu kuna ma haters sana
ReplyDeleteWichita wameshinda kwa sababu walikuwa wanacheza watu 12, wichita acheni ujanja wa nyani, mlisubstitute timu nzima wakati Hoston hakuna substitutes. halafu kwenye timu ya Wichita kuna wapopo kibao,
ReplyDelete