Kikosi cha Wichita
Kikosi cha Houston
Houston wakifurahia bao la kufutia machozi

Ni wakati wa mapumziko ambapo mshambuliaji hatari wa Wichita Iddi Ligongo (kati) na wenzie wakionekana kutafakari namna ya kupata ushindi

Timu ya Watanzania wanaoishi Wichita, Kansas, imetoa kipigo kikali kwa timu ya Watanzania wanaoishi Houston, Texas, kwa jumla ya magoli 4-1, katika mchezo uliochezwa Wichita, Kansas Jumamosi ya 7/8/2010.

Kwa ufundi mkubwa timu ya Houston ilitawala kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo, na kufanikiwa kujipatia goli la kwanza na la kuongoza katika dk ya 32 ya mchezo, mfungaji akiwa mshambuliaji wake hatari Peter Bategeki, goli hilo lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Wakati wa mapumziko, timu ya Wichita ilionesha kuchanganyikiwa na hali ya mchezo na kulazimika kufanya mabadiliko, ambapo yalibadilisha hali ya mchezo na kuifanya timu ya Houston kuanza kuonekana mdebwedo.

Mwiba kwa timu ya Houston alikuwa ni mshambuliaji hatari Idd Ligongo, ambaye alikuwa akiwasumbua walinzi wa Houston na kuwafanya washike kiuno kila mara, hali inayoashiria walikuwa hoi.
Katika dk ya 60 Idd Ligongo aliifungia timu yake ya Wichita goli la kusawazisha, dk 68 mshambuliaji huyo akafunga tena goli la pili. Dk ya 75 Musa Mbongo aliipatia timu ya Wichita goli la tatu baada ya kuitumia pasi safi toka kwa Idd, huku mshambuliaji Denis Mbelwa Rweikiza akiimaliza shughuli kwa kuandika goli la nne katika dk ya 82.
Kwa habari na picha zaidi tembelea
ama
www.tawichita.net.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. wichita wakija DC tutawapiga bao kama wamesimama.tatizo lao wanataka kuchezea kwao tu.

    ReplyDelete
  2. Shaali, Saidi na Diwani naona Mmemtesa Twailu, Du.





    Sandaly

    ReplyDelete
  3. huyu ni yulle Idi mtangazaji wa ITV...du kakimbia Tanzania..aisiii..kweli Tanzania shida sana ..sasa kwa nini watu wanakimbia...OK karibu USA kaka...fani yako ya utangazaji hapa sahau..hapa ni kuosha vizee mavi tu..na kuuza sandwiches Subway au kubeba box,...Whole Food,walMart nk...

    ReplyDelete
  4. mdau wa tatu hapo juu umeniua nimecheka weee, kweli we umepinda

    ReplyDelete
  5. du bulu nyani nakuona hapo, upo maboksi yamekubali hivyo naona siha unayohaswa,

    ReplyDelete
  6. Mdau wa aug9 04:43am.acha majungu sasa huku ULAYA kama tunaosha vizee sijui mavi,kupiga box,wewe kinachookuuma ni nini?sasa kwa taarifa yako hao watu unaowadharau MUNGU anawasaidia kuwapa kipato kizuri sana na wanaweza kufanya mambo makubwa sana huko nyumbanikuwasaidia familia zao na kuweka maisha yao vizuri kwa ujumla.Au walikunyima VISA nini ndo mana unachonga?acha hizo bwana wewe endelea kuchonga lakini tambua kwamba sisi tunasonga mbele na hatuna habari na habari za majungu hatupendi.Behave your self please!!!
    Mdau-Mji wa kusoma!!!

    ReplyDelete
  7. Wacha wafanye wanavyoweza Angalau Hawauzi Unga au Kukaa tu Majungu kama wewe. Mwenyezi mungu kaumba Dunia kwa Wote kachanganya watu kwa sababu zake, Riziki kwenye kila dini imeandikwa Tafuta kokote saidia wenzako kama alivyosema mdau mmoja angalau anasaidia kwao wewe una type majungu. Mungu azidi kuwafungulia Ndugu zangu huko Nje na Awalinde vizuri. Mkirudi mrudi Salama. MZ Iringa.

    ReplyDelete
  8. mdau wa aug9 02:01:00pm...Asante sana.ujumbe wako umesomeka vizuri mnooo.Bless!!!
    Mdau-Mji wa Kusoma!!!

    ReplyDelete
  9. mbona mnamlaumu mchangiaji hapo juu yeye anajaribu kumkaribisha mshikaji na kumueleza ukweli kama hapo alipo maisha yanakwenda kwa kuosha vizee na wewe unamlaumu kwani kasema kazi ya kuosha vizee ni mbaya ama anamueleza ukweli wa maisha ya ughaibuni nadhani kama nimemuelewa yaelekea na yeye ni moja ya wafanyakazi wa hiyo kazi sidhani kama ni muuza unga...

    Muosha vizee mzoefu

    ReplyDelete
  10. Safi sana Wichita! Lunda umenifurahisha na vuvuzela!!

    ReplyDelete
  11. naomba saana huu mjadala wa uoshaji vibibi uendeleee kwi kwiiiiiii

    ReplyDelete
  12. Timu ya Wichita hawana nauli,watafikaje Houston au DC ? Siku zote wanashindia uwanja wa home kwa kubebwa,tokeni tuone.Nyoooo !!!!!!

    ReplyDelete
  13. Muache Idd,haja leta u star wowote,Idd ni mtu mwenye determination,kama alicheza maigizo miaka hiyo,sasa hivi si Idd yule mcheza maigizo .Idd ana "determination ktk maisha" tatizo wabongo hawapendi kumuona mtu kaendeleea wanataka kila siku awe pale pale anacheza maigizo.Idd high five ,you are the man,you are the acheiver,usiwasiskile kuna watu mika kumi wapo kiwanja hawajaenda shule wala nini,halafu kuna ma haters sana

    ReplyDelete
  14. Wichita wameshinda kwa sababu walikuwa wanacheza watu 12, wichita acheni ujanja wa nyani, mlisubstitute timu nzima wakati Hoston hakuna substitutes. halafu kwenye timu ya Wichita kuna wapopo kibao,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...