MAZIWA FEKI YA WATOTO!
Kwanza kabisa lazima nikiri kuwa ninaandika walaka huu nikiwa na masikitiko makubwa sana pengine kuliko yote kwa mwaka huu kwasababu nami pia ni mwathirika wa taarifa zilizotolewa leo na TFDA kuhusiana na maziwa ya NAN 2.
Kwanza kabisa lazima nikiri kuwa ninaandika walaka huu nikiwa na masikitiko makubwa sana pengine kuliko yote kwa mwaka huu kwasababu nami pia ni mwathirika wa taarifa zilizotolewa leo na TFDA kuhusiana na maziwa ya NAN 2.
Nikiwa kama raia ambaye nyumbani kwangu sina maabara wala kifaa chochote kinachoweza kunionyesha maziwa haya ni sahihi au ni feki nimekuwa nikimnunulia mwanangu maziwa hayo tangu mwezi January baada ya tangazo kama hilo kutolewa likisema kuwa maziwa kadhaa yakiwemo S26 GOLD na mengineyo kuwa hayafai kwa matumizi ya watoto kwakuwa kuna watu wameyafoji nakusisitiza kuwa maziwa ya NAN na mengine kadhaa ambayo siyakumbuki ndio yanafaa kwa matumizi ya watoto.
Swali langu kwa wanaohusika ni kwamba hivi haya maziwa huwa yanaingilia wapi? Je, TFDA na TBS wana ofisi bandarini na kama wanazo huwa wanaaga familia zao wanaenda kazini kufanya nini?
Endapo haya maziwa feki yanasumu yoyote yenye madhara kwa watoto serikali imejipanga kufanya nini na kuwafanya nini walio yaagiza na kuyaingiza maziwa haya nchini huku wakitambua kuwa ni sumu?
Ninavyofahamu mimi serikali yetu ni moja ya kati ya serikali kadhaa duniani zinazotumia fedha nyingi sana katika masuala ya usalama mfano mzuri mnao kwamba kuna watu special kufuatilia Mtikila kasema nini ili ashitakiwe wakati bandarini kunaingizwa uozo ambao ni hatari zaidi kuliko maneno ya Mtikila!
Sina pa kusemea Michuzi ila roho imeniuma sana maana nchi yetu imegeuzwa dampo na wajanja wachache wenye roho za kifisadi na wasiotosheka na mali hata ukiwamilikisha bahari ya fedha. Mr President please do something for this, nchi inamalizwa na walafi wachache kwa tamaa ya pesa.
Ingawa hatuombei madhara, hebu fikiria watoto hawa waliotumia maziwa haya wakiharibikiwa mafigo na maini atakuwaje? INAUMA SANA!
Ni mimi MWATHIRIKA
Ni mimi MWATHIRIKA
brother Michuzi kwanza kabisa naomba nikupe hongera kwa kuweka hii taarifa kwa uma. mie binafsi nina mtoto mdogo nafikiri kama sio leo basi hata kesho yanaweza kunikuta na mie pia. Hizi athari mbazo wahusika wakuu TFDA na TBS wanazipuuzia zitaleta madhara kwa hiki kizazi "cha kesho" tunaweza kutengeneza vijana wenye matatizo ya akili ukuachilia mbali vifo. Nimesikitishwa saaana ni hili tukio. Jamani "serikali" niulize kitu, hivi unafikiri serikali kama ya china inaona raha kuweka adhabu kali kama ya kifo? Inafanya hivi ili watu kama hawa wanoingiza bidhaa hizi feki wasiweze kuthubutu. Nasikitika kusema serikali yetu inalea uozo huu na madhara yake ni makubwa sio kwa waathirika wanafamilia bali hata kwa taifa lote. Mwisho ningekuomba brother Michuzi na wadau wote tulisemee hili suala ikiwezekana tuweke sahihi ya adhabu ya kifo kwa watu wote watakaopatikana na hatia.
ReplyDeletendugu mwandika wakala, inaniuma mie pia kama wewe. Naona hawa TFDA, ni kama wale wanaosubiri mafuriko yatokee, ndo watoe utabiri wa hali ya hewa. Wameshatuumiza saana na hili swala la maziwa ya watoto, mpaka mimi nimeamua kumtafuta mtu mwaminifu kuliko TDFA anayefuga ng'ombe ndo maziwa yake nampa mwanangu. Nafikiri maziwa haya hutambulika kuwa feki baada ya kutumika, jamani! ni kwamba staff hawatoshi huko TDFA au ni vichwa maji ndo wamejaa huko? Hayo maziwa huwa yanatokea hewani na kuingia madukani? Kweli Kikwete ana kazi, kazi kubwa! inabidi iwekwe sheria kuwa zikikutwa bidhaa feki za vyakula madukani, basi waanze kuadhibiwa staff wa TDFA kabla ya wenye maduka, kwani ndo wanatakiwa kuchukua action first before wenye maduka.Ndio maana maduka makubwa (Supermarkets) wameamua kuacha kabisa kuuza maziwa ya watoto, kwa sababu ya longolongo hizi. TDFA fanyeni kazi bwana,mtachuma dhambi kibao kwa kutuharibia watoto wetu buree!
ReplyDeleteNAFIKIRI KUNA MAPUNGUFU YA KIMSINGI YA KIUTENDAJI WA TAASISI ZETU NAKUMBUKA WAKATI FULANI WALISITISHA MATUMIZI YA DAWA FULANI YA BINADAMU BAADA YA DAWA HIYO KUPIGWA MARUFUKU NA MAMLAKA YA CHAKULA YA NCHI JIRANI.PENGINE NI WAKATI MUAFAKA KWA TAASISI HIZI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA NA WATAMBUE UMUHIMU WA KAZI YAO. SERIKALI IMEWAAMINI NA KUWAKABIDHI KUSIMAMIA USALAMA WA AFYA ZETU WATEKELEZE WAJIBU WAO SAWASAWA SIO WASUBIRI KUPATA TAARIFA KUTOKA NCHI ZINGINE NDIPO WACHUKUE HATUA, HUO NI WIZI WA KITAALUMA NA KUKOSA UWAJIBIKAJI.
ReplyDeleteAssalaam Alaykum,
ReplyDeleteNdugu Michuzi , tunashukuru kwa kututumia vitu kama hivi, mimi naweza kusema ni muathirika au sivyo kwa kuwa sijui nini kilimsibu mtoto wangu wa kike ambae alikuwa na miaka 9. Mtoto aliumwa figo likatolewa na bahati mbaya sana akaambiwa ana cancer na very unfortunate mwaka huu mtoto alifariki. kwa kweli wakati mtoto wangu amelazwa pale Ocean Road case kama za mwanangu zilikuwa nyingi mno! kila mtoto aloletwa pale either amekuja moja kwa moja ocean Road ana matatizo ya figo , au ametokea Muhimbili ameshachnwa mwanzo wa tumbo mpaka mwisho ameshatolewa figo, au amekuja OCean Road kupunguzwa uvimbe akatolewe Figo, kwa kweli ni watoto wengi sana sana sana idadi yake siijui na sijui Khatma zao zilikuwaje ila kuna mmojaambae nilisikia nae amefariki. Nilipokuwa nauliza uliza manurse kwanini cancer za watoto ni nyingi hivi na hasa mafigo ! nurse alinijibu huenda maziwa na vyakula !!! jamani mie naandika hii msg naumia sana ! nadhani serikali yetu inatakiwa iwe serious au sivyo kizazi cha kesho chote kitaangamia na cancer kwa ajili ya maziwa na vyakula vya hovyo! Dah! yaani hata sijui nieleze vipi hisia cangu ! jamani Serikali wabunge ! badala ya kujali maslahi yenu tafuteni ufumbuzi kwenye hili , tomorrow it might be you !!!!
Mungu wabariki na walinde watoto wa TAnzania...Amin
Pole sana mwathirika. Kwa bahati mbaya sana mambo kama hayo yapo kwenye kila idara ya Serikali yetu. watu hawako makini, au wanafanya makusudi ili wajitajirishe. Suluhisho lake ni ngongojea Mh. Rais aingilie kati ili vyombo vya habari vitangaze kuwa " JK NI KIBOKO". Hapo ndipo tulipofikia kwa sasa. Maana yake ni kuwa wale wote waliopewa dhamana ya kufanya kazi kwa ajili ya Taifa hili na kumsaidia Rais kutekeleza majumuku wameshindwa kazi. Mbaya zaidi ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa juu yao. Wanaishia kuhamishwa na kubadilishwa.
ReplyDeleteHuo ndiyo ukweli wenyewe, inabidi tuishi nao tu.
Hivi ni vipi kitu kimeshatumika ndo wanagundua wakati watu wameshahathirika, Je hivi vyombo vya ukaguzi vinafanya kazi yake sawasawa? Kuna sehemu kazi hazifanyiki sawasawa. Wahusika wanachukua rushwa huku raia wakiumia? au wanaopewa kazi elimu yao haitoshi kugundua hitilafu kama hizi.
ReplyDeleteMdau,
ReplyDeletePole sana.
Tanzania mteja hana HAKI YOYOTE yaani hata akiuziwa maziwa feki au dawa feki za binadamu.!!!
Hapa ndipo mimi ninapowashangaa Wanasheria wetu (binafsi na serikali) kwa nini wasiwe na mwamko wa kukusanya waathirika na kufungua mashitaka dhidi ya serikali na waagizaji kwa niaba yao?
This is madnes.
NB: Mdau iwapo mtoto wako bado anatumia maziwa, weka e-mail yako hapa nikupe mwanga wa namna ya kupata maziwa safi na salama.
Mdau umeleta hoja ya muhimu sana. Nashangaa hao wanaojiita TFF ya mdawa eti wakiona wanamekaa sana kimya wanatafuta waandishi wa habari wanaenda kwenye maduka ya vyakula, na madawa wanajifanya wamekamata madawa feki. Foolish!! Walikuwa wapi hadi vikaingia wakati wanajua kabisa vinapoingilia. Pili wanaishia tu kusema wamakamata vitu na sio watu walioviingiza. Ukikamata vitu, alaf mtu hujamkamata ataendelea kuleta vingine. Come-on msiwe wanasiasa nyie TFF ya madawa. Najua nyie mna nafasi kubwa sana ya kulinda afya zenu kwa kuvileta maabara yeny hapo vile vitu mlivyonunua kwa matumizi yenu ili mvipime kama haviaadhiri afya. Mnavipima kwa gharama yetu sisi wananchi alaf mnaa Khrrrrrrrrrrrr, sitaki kuongea tena mnaniuzi
ReplyDeleteNakuunga sana mkono mtoa mada. Mimi pia imenikera mno mpaka kwenye gazeti la Daily News ambalo lili-report nimeweka comments zangu. Ni hatari sana kwa kweli hasa kwa watoto wadogo ambao nchi zingine wanathaminiwa sana sana kama nguvu kazi ya kesho. Miaka ya nyuma wanangu watatu wametumia sana S 26 na zingine kwa muda wote mpaka wameacha wenyewe. Huyu wa nne ana mwaka mmoja sasa na ilipoanza ile mwaka jana mambo ya fake fake, mara moja nilimwachisha maziwa ya kopo na akaanza ya ng'ombe. Baada ya muda kidogo nikapiga marufuku any tinned (parkaged) materials nyumbani. Sitaki tomato sources, species, juices wala hata chochote. Tunanunua sokoni vikiwa fresh na ku-blend wenyewe.
ReplyDeleteTunajua kuna fake items kibao madukani,ila linapokuj suala la vyakula vya watoto, kwa kweli tunapoteza matumaini kabisa maisha. Tusaidieni wakubwa
NI KWELI KABISA HIVI HAO TFDA NA TBS,WAFANYE UCHUNGUZI KWANI TANZANIAIMEKUWA DAMPO LA NCHI ZINGINE KULETA BIDHAA FEKI,MKO WAPI? MADUKANI NA MASOKONI KUNA BIDHAA FEKI KIBAO ZA KICHINA NA NCHI ZINGINE AMBAVYO ZINA VIAMBATA VYA SUMU KWA AFYA NA MWILI WA MWADADAMU,OKOENI TAIFA JAMANI,TUNAANGAMIA!!!
ReplyDeletembaya zaidi madhara kwa mtumiaji huonekana muda mrefu baada ya matumizi.
ReplyDeleteI feel you brother. This is more serious than maneno ya Mch. Mtikila. Someone must do something really.
ReplyDeleteTATIZO HILOSI LA TANANIA PEK YAKE NI NCHI ZOTE ZA KIAFRICA NA HASA BAADA YA KUWAKARIBISHA WACHINA NAKUMBUKA MWAKA JANA WATENGENEZAJI WA MAZIWA HAYO FEKI WALIHUKUMIWA KIFO CHINA,LAKINI WENGI BADO WAKO HUWEZI AMINI KUNA MCHELE FEKI,KETCHUP FEKI MAYAI FEKI TOKA CHINA.DAWA NI KURUDI KWENYE VYAKULA ASILIA MAZIWA YA MAMA YA NG'OMBE YA KUKAMUA NI BORA NA AFYA KWA WATOTO HAWA JAMAA WATATUMALIZA.
ReplyDeleteyaa inauma sana na poleni sana kwa wote ambao mmepatwa na janga hili hasa kwa watoto wenu. Juzi hapa sweden walikuwa wanonesha tatizo kama hilo ambalo limetokea huko china kuwa watu walikuwa wakinunua maziwa kwa ajili ya watoto wao na kumbe maziwa hayo yalikuwa na sumu na madhara yake ni kuwa watoto wanaanza kuota matiti wakiwa bado wadogo kwa hiyo inasikitisha sana pale mtoto wako anapokuwa na matiti wakati hata bado hajavunja ungo. kwa kweli tanzania inabidi viongozi wetu waache ujinga wafuatilie mambo muhimu hasa kama haya ambayo kwa vizazi vijavyo itakuwa hasara kubwa. Kwani kama maziwa hayo yameuzwa kwa mda na hadi sasa ndio wanagundua madhara yake unadhani ni watoto wangapi watakuwa wameyatumia? inabidi watanzania tuamke na tusimame kutetea haki zetu na kufanya mabadiliko.
ReplyDeletemdau sweden
WATANZANIA WATAENDELEA KULIA TU, HAO HAO WANAINGIZA HAYA MAZIWA NDIO WACHANGIAJI WAKUBWA WA CHAMA CHA KIDUMU. HIVYO USITEGEMEA WATAGUZWA NA WENYE SIRIKALI.
ReplyDeleteMdau unaharibu unapoingiza politikk ndani ya mada nyeti na kuharibu kila kila kitu. Masuala ya kufuatilia mtikila kasema nini (hata kama yapo) hayana uhusiano kabisa na ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kwetu. Tuache kulalama ovyo tukitegemea serikali itatufanyia kila kitu. Chukua hayo maziwa feki na mfungulie mashtaka huyo aliyekuuzia, huo ndiyo uzalendo!
ReplyDeleteMacho, masikio, mioyo na mawazo yote ya viongozi sasa yameelekwezwa kwenye uchaguzi wa Oktoba. Hakuna msaada wowote wa maana kutoka kwa serikali hii unless watu wenye watoto waseme hawataipa kura mpaka wahusika wa haya maziwa wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa kwa haki.
ReplyDeleteNchi kama China hapa ni kunyongwa tu. Hakuna huruma kwa watu kama hawa. Lakini hapa Tanzania blaa blaa ni nyingi sana hivyo wanapeta tu. Ikitokea wakipatikana wanalipa tu gharama za kuharibu hayo maziwa basi. Halafu wanaagiza tena bidhaa nyingine feki
ReplyDeleteNdugu mwathirika, sijui ya kwamba idara husika zinafanya nini? Na je mpaka hivi sasa kuna mtu yeyote anayeshikiliwa/kushtakiwa kwa huu udhalimu zidi ya watoto wasio na hatia? Na kama hakuna mtu anayeshikiliwa walijuaje ya kuwa kuna tatizo hilo? Hivi hapo TFDA kuna wataalaam wa vyakula kweli? Wizara ya afya mpo wapi? Mama Blandina mbona upo kimya kwa hili lakini ingekuwa suala la 'publicist' basi tungekusoma blog zote! We kazi yako kujifagilia tu, lakini suala kama hili upo kimya!!! Prof Mwainkyusia vp baba? Upo kwenye kampeni au? Maana suala hili wapinzani makini wakilipata latosha kabisa kukuangusha baba, maana ofisi yako imelala na watoto wa wadanganyika wanakufa taratibu... JK hawa jamaa zako wa wizari hii tafadhali mwezi wa kumi watafutie kazi nyingine maana hii wizara imeoza.
ReplyDeletePole sana dada yangu. Tatizo ni kwamba Tanzania sasa hivi imekuwa kama law of the jungle "Struggle for existence, survival of the fittest". Yaani ni kama baharini vile big fish eats small and then he's going to be eaten by larger that him.
ReplyDeleteHuu ni mwaka wa uchaguzi. Mojawapo ya issue ilitakiwa kuwa consumer protection. Nchi yoyote ile yenye serikali makini huweka usalama wa raia wake kama primary responsibility (Including protection from fake products).
Tatizo la nchi yetu ni moja, wafanyabiashara ndiyo wanaotutungia sera. Matokeo yake ni kulinda masilahi yao kwanza mengineyo baadae. Kama ingekuwa ni nchi za watu walikuwa na elimu ya uraia ya kutosha mnawatosa wale wasio wajali katika nafasi za uongozi. Unakuta mtu kakamatwa na mafuta chakachua mnamchekea kumwambia ayafanyie refining badala ya kumnyang'anya leseni na kumpiga mvua kumi jela.
Nyerere aliishasema kuwa nchi yoyote corrupt utaijua kwa viongozi wake kuacha kuangalia jinsi ya kuwainua masikini na kuwalinda badala yake kukumbatia matajiri, ambao hutumia nafasi hiyo kuwanyonya masikini kila kona.
Ingekuwa inawekwa wazi kuwa bidhaa yoyote fake ikikamatwa nchini, mkuu wa TBS, TRA, Polisi na waziri mwenye dhamana wanajiuzulu mara moja na kupisha wengine wafanye kazi. Unakuta mtu anakamatwa na ofisa wa ngazi ya chini, baada ya muda kinakuja kimemo toka ngazi ya juu kuwa aachiwe ana uhusiano na mkubwa fulani. Hapa ndipo kwenye uoza. Tunahitaji Raisi ajaye awe dictator kwenye kulinda masilahi ya wananchi na nchi (Siyo chama, maana chama kinaweza kuwa kiko chini ya wafanyabiashara, kulinda masilahi yake ni kulinda masilahi ya wafanyabiashara)
jamani wa kina mama wenzangu hasa so called wasomi ndiyo wenye kupenda mavyakula ya madukani kama frozen foodstuffs, fizzy drinks na chips kwa watoto, unaweza kuwa una elimu kumbe huja elimika. Kama huna kizuizi kama maambukizi ya HIV, nyonyesha, nyonyesha, nyonyesha maziwa ya Mama ni bora kuliko chochote. Kisingizio eti hayatoshi hakuna kitu kama hicho. God created for purpose. Kama unasafiri kikazi ndani ya nchi basi nenda na Yaya na mtoto ili mtoto anyonye. Huu ukisasa utatumaliza. Wazazi wetu walitulisha vyakula vya asili na tumekua. Sasa tumejaza vyakula kwenye freezers vitaliwa hata miezi 3.
ReplyDeletemambo ya formula tuwaachie wenye nchi zinazotetea maslahi ya wananchi wakiumia. Imekuaje maziwa ya ng'ombe siku hizi hayatumiki tena? Tulivyokua tunakua maziwa ya kopo yalikua hata huyaoni. Ni cerelac tu nayo unampa mtoto kama a treat. Siku hizi kila mtu ni maziwa ya kopo. Maziwa ya ng'ombe hamna anayetaka tena. Akitumia anaonekana kama hajaendelea...Faida ndio hii...watu siku hizi hata hawataki kunyonyesha watoto wao tena. Niko huku cousin wangu ananiambia anataka nimtumie formula. I was really shocked nilivyosikia hivyo?
ReplyDeleteWenzetu wameamka na kufanya maresearch na kuona waototo wanaotumia haya maziwa ndio wanapata childhood cancer kuliko wanaonyonyeshwa. Kwa wenzetu cancer wanatibu na asilimia 80% wanapona. Sisi kwetu tuna %? ya success? Tukishaanza kutumia haya maziwa miaka 10 kila mtoto akija kupata cancer kuna mtu atabakia kweli? Hospital ya cancer si zitakua overwhelmed tu? Tuache kuiga haya mambo ya kutmtumia haya maziwa sio kuonekana kuwa umeendelea au unahela ni ufinyu wa akili. lakini wenye hela ndio wanatumia haya maziwa hivyo watoto wao wakiugua wataweza kuwapeleka huko nje kutibiwa. Kama huna hela ndugu yangu stay away from these formulated and process foods...Trend imerudi kila mtu anataka kula organic siye ndio tunatupiwa hayo mavitu yasiyopata wateja tena. Tutakuja kumlaumu nani baadaye...Let go back to out tradition. Mtoto anyonyeshwe mpaka miaka miwili unless una matatizo au immune system iko compromised.
to all mothers,
ReplyDeleteplease breast feed your child they will get good health and get good brains and be like you.
IF WE FEED FACTORY MILK, OUR CHILDREN WILL BE LIKE THE WORKERS OF THE FACTORY.
Jibu ni moja, nalo ni kumpa 'pilau' Dr. Slaa katika Muungano na Maalim Seif Zanzibar.
ReplyDeleteBila ya hivyo mutapiga kelele weeeeeeeeeeeee mpaka mutachoka , ndio maana mimi nimeacha kutumia degree yangu ya Oxford kuandika makala za uchumi wa Tanzania.
natumikia wazungu mpaka Dr. Slaa na Maalim Seif watakapokabidhiwa nchi ndio niakuwa kusaidia.
(US Blogger)
Je ni nani aliwaambia kwamba kuna wakaguzi bandarini au kokote kule, kama wapo ni wanfanya kazi ambayo kuna maslahi mfano kuna pesa imetolewa ili waweze kukamata kitu fulani. Kama unataka kujuwa kwamba hakuna wakaguzi popote pale do anything wewe weka tu pesa yako mfukoni utafanikiwa. Kama vile EPA n.k. Ukiona wakaguzi wewe waangalie usoni tu wamejaa njaa wanfikiria jinsi gani atapata pesa yako apeleke mtoto shule ya private kama ya yule jirani yangu, au nitapata pesa tu nikanunuwe gari kama ya rafiki yangu. Ukaguzi sahau kama upo ukikaguliwa tu ni pesa yako wantaka lakini siyo kujali eti taifa na kizazi kijacho kitapata chochote.
ReplyDeleteKwa ufupi ni kwamba kuelimisha wananchi ni vyema kabisa. Taifa bila elimu si taifa. KUmbuka enzi za elimu ya watu wazima chini ya mti, je kunae aliyeshiriki kufundisha wazee wakati huo? hiyo ndiyo ilikuwa elimu kwa umma kwani watu walijuwa kinachoendelea na wakjuwa kusoma magazeti.
Ni vyema kujulisha familia kwamba chochote unchonunuwa dukani kimefunikwa kwenye kopo au plastic unawapa familia yako wale kina madhara. Na hili ni tatizo kubwa kwa wasomi Tanzania kwani mkulima ni saa ngapi atahangaika na vitu kwenye makopo wakati anvyokula vingi vipo shambani. Watu wanaancha nyanya safi sokoni, wankwenda kununuwa supper markert, vitu ambavyo vimeshaisha wakatiwake.
Kama kweli tuna wakaguzi basi wangeingia kwenye hizo supper makert na kuondowa mashelf ya vitu vyote vilivyopitwa na wakati.
Poleni sana mlioathirika na ili. Mimi mwanangu ana miezi miwili hivi. Bahati mbaya mama yake hana Martenity leave kwani alianza kazi akiwa tayari mjamzito. Hivyo nategemea maziwa haya kwani mtoto kakataa maziwa ya ng'ombe.
ReplyDeleteNaangaika sana kutafuta maziwa yasiyo feki. Watu wanasema ninunue Lactogen 1 pale Namamnga. Nimekuwa nafanya hivyo. Lakini nimestuka sana kwani mara ya kwanza mwezi jana nilinunua kopo lenye maandishi kwenye karatasi iliyobandikwa huku nikihakikishiwa kuwa sioy Feki.
Wiki juzi nilinunua duka jirani lakini maandishi yapo kwenye kopo.
Hivyo naomba mdau hapo juu anielekeze sehemu ya kupata maziwa yasiyo feki.
Email: nyati04@yahoo.com
Vile vile kama kuna jinsi ya kumfanya mtoto anywe maziwa ya ng'ombe basi naomba nielekezwe
Natanguliza shukrani za dhati
Nasikitika kuona kwamba ni wazazi wengi tuna matatizo kuhusu maziwa ya kopo, tunapenda sana kunyonyesha watoto wetu lakini kuna matatizo mbali mbali yanayotufanya tusiwanyonyeshe watoto. Maziwa ya ng'ombe siyo yote ni mazuri na kupatikana kwake ni kwa shida. Hivyo naomba wizara inahohusika itueleweshe kuhusu hayo maziwa. Nimekuwa natumia Lactogen 1 yenye maandishi kwenye mfuniko. baadaye nikaambiwa siyo mazuri. Nitumie yenye maandishi kwenye kopo. JAMANI TUSAIDIWE NA HILI JANGA.
ReplyDeletepole waliopatwa na shida hii. mimi ninamtazamo tofauti kidogo, naona tuna wabebesha sana lawama hawa jamaa wa TFDA nafikiri tuanze na sisi wenyewe kwanza wananchi kwa ujumla wetu tunasaidiaje hili? watu wa TFDA ni wachache kulinganisha njia nyingi za panya zilizopo watu wanapitisha kwenye njia za vichochoro iliyo karibu na mipaka ya nchi yetu, tuanze kabisa kwa kuwalaumu wafanya bihashara wanao jifikiria wao tu bila kujua madhara ya watumiaji ambao wanaweza kuwa hata wajukuu wao. TFDA wanajitahidi sana tuwape moyo ili waendelee watanzania wanapenda rushwa sasa ebu tujiulize yule mama aliyekuwa mkurugenzi wa TFDA yuko wapi leo? ameacha kazi kwa kuwaogopa watu wa nchii hii. tuanza na sisi wenyewe na si TFDA watanzania yumekuwa walafi sana.
ReplyDelete