RATIBA YA VODACOM MISS TANZANIA 2010
Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, leo wameingia kambini kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumrithi mrembo anayemaliza muda wake, Miriam Gerald.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo mchana kabla ya warembo hao kuelekea Kambini, Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema kuwa “Warembo hao Wakiwa kambini watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii”
Alizitaja sehemu hizo kuwa siku ya Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.
Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010
Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajiri ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu.
Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.
Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.
Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

Imetolewa na Hashim Lundenga
Mwenyekiti
Kamati ya Miss Tanzania
kila siku umiss tu akuna lingine !!
ReplyDeleteHivi watu weusi hatuwezi kuwa wazuri mpaka tuvae nywele za kubandika?
ReplyDeleteWasichana wazuri wa kiafrika lakini vichwani ni nywele za weupe.
WHEN ARE WE GOING TO BE PROUD OF OUR OWN BODIES WE BLACK PEOPLE
SUBHAANAL LAH
ReplyDeleteDALILI INGINE YA MAANGAMIZI, DADA NA BINTI ZETU, WENGINE BILA KUJUA WALIFANYALO, WANATUMBUKIZWA KATIKA VISHAWISHI VYA NGONO ZEMBE NA UFUSKA!
MWANZO WA FUTURE YAO KUHARIBIKA, LAKINI SI HIVYO TU, BALI NI MWANZO MWENGINE WA JAMII KUPOTEZA NGUVU KAZI NA HATIMAYE KUPOTOKA!
MUNGU ATUSAIDIE, SABABU TUNAKOKWENDA KUNATISHA. TUMESHASHUHUDIA SI MARA MOJA WALA TANO, MATOKEO YA U MISS, UASHERATI, TABIA MBOVU NA KWA UJUMLA KUPOROMOKA KWA MAADILI, HESHIMA NA FOCUS.
SAMBAMBA NA PROMOTION INAYOFANYWA KATIKA KUUPIGIA DEBE HUU UITWAO ULIMBWENDE, WAZAZI, WALIMU NA WOTE WANAOHUSIKA NA MALEZI YA WATOTO WAENDELEZE JITIHADA KATIKA KUVIELIMISHA VIZAZI VYETU MADHARA YA MCHEZO HUU. KWA KIFUPI HAUIFAI JAMII YETU NA HAUNA HERI YOYOTE, LAKINI ZAIDI NI KICHOCHEO CHA ZINAA NA MAAMBUKIZI YA MARADHI.
LAKINI KWA MASTAAJABU, SHETANI AMEKAMATA BANGO MBELE KUONGOZA UCHAFU HUU, NA MPAKA SASA NDANI YA NYOYO ZA WATANZANIA WENGINE MARADHI YAMESHAINGIA NA KUOTA MIZIZI, NA LINAPOKUJA SUALA LA ULIMBWENDE HUNA CHA KUWAAMBIA WAKAKUSIKILIZA.
KULIKO MICHEZO MINGINE YOTE, MCHEZO HUU NDIO KWA SASA WENYE KUPIGIWA MBIU ZAIDI NA WENYE KUFANYIWA KAZI ZAIDI.
KAMA NI YA KWELI YALE YALIYOIGIZWA KATIKA FILAMU YA MISS BONGO, NA KAMA NI YA KWELI YALE TUNAYOYASOMA KUTOKA GAZETI LA IJUMAA KUPITIA MTANDAONI, NENO MOJA TU LINAWEZA KUFAA KUIELEZEA JAMII YA KITANZANIA YA LEO: TUMEKWISHA! TANZANIA YA SASA BILA UKIMWI NI NDOTO ZA ALINACHA!
NANI WA KUMLAUMU?
WA KWANZA, KWA MTAZAMO WANGU, NI KIONGOZI WA JUU ZAIDI MADARAKANI, KISHA WATENDAJI WAKE WOOOTE, AMBAO NDIO TUWAONAO MAGAZETINI NA KTK TV WAKIWAPEPERUSHIA BENDERA YA NCHI HAWA MAMISS ETI WAKAIWAKILISHE NCHI YETU.
NI LAZIMA WENYE MSIMAMO KAMA WANGU TUSIMAME KIDETE JAPO TU KUKEMEA BALAA HILI, NAAMINI SHETANI NI DHAIFU KULIKO MUNGU MUUMBA, NA TUTAWEZA KULETA JAPO MABADILIKO KIDOGO.
Mndengereko, Ukerewe
Ankal Hasheem Lundenga
ReplyDeleteKwahisani yako naomba hii kambi muifanye kabla au baada ya mfungo, kumbukumbu zangu zaonesha hii ni awamu ya tatu kambi ya Miss Tz inafanywa kipindi cha mfungo, sikinzani ni mipango yenu, lkn itawapa fursa mabinti wenye imani waweze kutekeleza nguzo hii bila vikwazo.
Ni hayo tu,.kwani anaekukosoa bila kukuonea haya huyo ndo rafiki wa kweli.
wow! i cant wait for Miss Tanzania!! this year, wazuri wengi!!!
ReplyDeleteDont forget to go by laprincessaworld.blogspot.com
Loh huyo mlimbwende aliyevaa blauzi ya bluu amenigusa moyo na ninamwombea apite apate taji - ana amvuto wa aina yake.
ReplyDeleteNdugu unayelalamikia maadali: ukweli ni huu: kama madume wanavyotumia udume wao (masculinity) kucheza mchezo wa ngumi (ambao nina uhakika utakuwa unaushabikia sana) ndivyo majike wanavyotumia ujike (femininity)wao kucheza mchezo wa ulimbwende. Ni maumbile tofauti na yanatumiwa kwa lengo lile lile - usanii ili kuburudisha na hivyo kujipatia kipato.
Michuzi usibanie hii, Naomba sana wewe ni mwandishi wa habari mwenye heshima nyingi na tunapenda sana unachokifanya. Nikiwa kama binti kuyumbishwa namna hii, sidhani kama kuna baba ambae yupo Proud kutangaza kwamba binti yangu ni anakazi ya kupigania umiss, badala ya kuhamuwa kumpatia kitu cha kusimama mwenyewe na kujenge taifa letu, kuna mabinti hapo sidhani kama wanakwenda majumbani wakishamaliza shunguli hapo, nadhani wengi wao wanaishia kwenye mahoteli na kulala na hoa hao wanojiita wasimamisiUnakuta libaba na wake zake na watoto kila kona ni bado ananisamamia Umiss Its shame. Ukiangalia mila zetu za kitanzania hazina hii jadi ambayo haina maana, ni vyema hao mabinti wakeleza hadharani ni kitu gani kinawasibu, Just victim kama vile House girls tu. Kaka Michuzi sidhani kama unaweza kumruhusu binti yako azungushwe namna hii.Tafadhali kama utatusaidia na kutotowa hili jmabo kama vile unavyotowa kila kitongoji, unatudhalilisha sana sisis wakina mama. Ingawa tunajuwa kwamba baadhi yao ni wafadhili wako, lakini tumia utu wa kutokudhalilisha namna hii. Nashukuru kaka Michuzi.
ReplyDeletehuyo mdada mwenye blue ndio mshindi tuuu, wengine hayaaa na sie tulikuwepo hata ankal anampa kipaumbele cha photo mee!!
ReplyDeleteDUH!
ReplyDeleteMSIMU WETU UMEFIKA...KAMA KAWAIDA NAHAMIA MITAA ILEILE....MNAONGELEA MAADILI NI WANAFIKI TU HAMNA LOLOTE...KILA KIUMBE KINA RIZIKI YAKE HAPA DUNIANI ..WE ANGALIA WANYAMA ,NDEGE NK HUWA WANAWEZAJE KUISHI ?? HATUWEZI WOTE TUKAWA WANARIADHA AU MABONDIA AU WANAMUZIKI....ACHA WALIOJALIWA UREMBO WAUTUMIE,HIYO NDIYO KARAMA YAO!!!I LOVE U BEAUTIES....UFUSKA,MISBEHAVING NI MAMBO YATOKANAYO... NI TABIA YA MTU ..WAPO WAREMBO WENYE TABIA NZURI NA WANAJIHESHIMU TU MPAKA LEO..
Chaos JM
Said, Mndengereko Ukerewe!! So nice Nimependa Saana Hiyo. Hata mie hua najiuliza Hivi Mbona maovu ni mengi saana katika mchezo huo! Na watu wanaushabikia utadhani kitu gani!! Kuna Huyo anyetetea ngono zembe hapo chini eti kama mieleka mieleka we umeambiwa kuna kambi gani wanakaa wakarubuniwa kama hawa vibint!! Maana Binti akienda Huko ajiandae kujitoa kwa kila kitu ili eti anaweza akawa miss!! Lakini zaidi ya yote wanaishia kudhalilika Hii Inaniuma saana ningekua na uwezo ningepiga stop!! Full Mazingira ya ngono!! Hyu mwinginw eti baada au kabla ya Ramadhani NOP Haina baada wala Kabla!! Huu mchezo ni ngono tu humo!! Big up Dada unaesema hakuna baba anaefurahia huu mchezo na kama yupo basi Naye ana mchezo mchafu kwa vibinti vya wenzie!! Mniwie radhi Ila huu mchezo haufaiiii TZ!!!.... Lundenga Unafunga Kweli wewe!!!!!!..... Mungu Akusamehe
ReplyDelete........Haya sasa Ma PDG(pedeshee)nyama haina mfupa hiyo.....kitu lainiii!!!!!!! Ankal Hashim jitengenezee tu pepo yako.
ReplyDeleteMnoko.
Mambo ma-miss!! mimi ni supa staa wa bongo. Ntawatembelea huko kambini hivi karibuni kuonja mmoja wenu...nisubirini. Mimi supa staa hamwezi kataa...
ReplyDelete