semina ya mafunzo kwa wafanyabiashara ikiendelea katika ukumbi wa Nyumbani Hotel & Resort,jijini Mwanza.
Commercial Bank of Africa Tanzania mwishoni mwa wiki iliendesha semina ya mafunzo kwa wafanya biashara katika ukumbi wa Nyumbani Hotel & Resort jijini Mwanza.
Malengo ya semina hiyo ni pamoja na kuelezea huduma zitolewazo na CBAT, kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara, umuhimu wa kukatia BIMA biashara na mali.
Mambo mengine yaliyofundishwa katika semina hiyo ya siku moja ni pamoja na umuhimu wa kusajili biashara, matumizi ya mabenki na mahusiano kati ya familia na biashara.
Akizungumza katika semina hiyo Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi katika Benki hiyo David Shambwe alisema imefika wakati sasa wafanyabiashara kujifunza umuhimu wa kutumia huduma za kibenki na kauchana na tabia ya kuweka hela nyumbani.
Amesema hela ikiwa kwenye mzunguuko wa Benki na kutenganishwa katika matumizi ya binafsi na biashara itamjengea mfanyabiashara kuaminika na Benki na hivyo kumpatia moja ya sifa muhimu katika kupata mikopo.
Shwambwe aliwakumbusha wafanyabiashara umuhimu wa kutengeneza hati za nyumba na kusajili mali zao kwa kuwa pia nyaraka hizo ni muhimu katika kupata huduma mbalimbali za Benki na hasa mikopo.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya mia mbili iliendeshwa na Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali Fredereck Lutindi akishirikiana na Meneja wa uhusiano wa biashara kwa makampuni Beatrice Laizer iluhudhuriwa pia na wakurugenzi wa biashara na kufunguliwa na Mkurugenzi wa huduma za biashara za Makampuni na Taasisi Frank Nyabundege (Pichani).
Commercial Bank of Africa Tanzania inayoendesha shughuli zake kutokea jijini Dar es Salaam ina matawi matano nchini; matatu yakiwa jijini Dar es Salaam, tawi moja mjini Mbeya na tawi jingine katika jiji la Mwanza.
Nyabundege hubadiliki, yaani kabla sijasoma kujua kama ni wewe nilishaapata picha ya Usagara sec member wa 1995.
ReplyDeleteVipi bado unaendelea na ubishi wako kama wa kwenye discussion?, maana ulikuwa mgumu sana wa kukubali mpaka uelewe.
Hongera sana
Usagarani member aka mtoto wa Mudi au Shao