Benki ya CRDB Tanzania Tawi la Zanzibar jana ilitoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi 3,400,000/- kwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Bwana Nassoro A. Uzigu, Meneja wa Benki hiyo Tawi la Zanzibar kwa Profesa Ali Seif A. Mshimba, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.


Shughuli hiyo ilifanyika katika Chumba cha Mikutano cha Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni ya Chuo Kikuu hicho.

Vifaa hivyo vinategemewa kutumika katika shughuli mbali mbali za kimichezo za Chuo yakiwemo mashindano ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki yanayotegemewa kufanyika baadae mwezi Disemba, 2010 huko Kenyatta University, Nairobi – Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...