Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mtunza Hazina wa Duka la Dawa la Lumumba Abdallah Jamal (kulia) jinsi wanavyotoa vyandarua kwa mama wajawazito chini ya mpango wa hati punguzo. Duka hilo ni miongoni mwa maduka ya dawa yalisajiliwa na serikali ya kutoa vyandarua vya hati punguzo.
Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian (kulia) akimwangalia mtoto mchanga na mama yake leo jijini Dar es salaam wakiwa katika Kituo cha Afya cha Manazi Mmoja wakisubiri kuandikishwa kwa ajili ya kupata vyandarua vinavyotolewa chini ya utaratibu wa Hati Punguzo kwa mama wajawazito na watoto.
Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian (kushoto) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Asha Mahita(kulia) na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja Dkt Felister Kwayu(katikati) leo jijini Dar es salaam . Naibu Waziri huyo alitembelea Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja kujionea utaratibu wa utoaji wa vyandarua kwa Mama wajawazito chini ya Mpango wa Hati punguzo.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Vyandarua hivi feki ndicho chanzo cha ongezeko la mbu, wataalamu tunaowategemea wanasemea chinichini kuhusu utata wa biashara hii ya vyandarua feki.

    ReplyDelete
  2. Mmmh na hilo pazia hapo ofisini? hakuna utaratibu wa kuangalia maofisini pazia mpaka linataka kuachia?!

    ReplyDelete
  3. kazi nzuri kaka ila anaitwa Stephen O'Brien. Wewe utajisikiaje ukiitwa Muhidin Makande ilhali jina lako ni Misupu oh sorry Michuzi?

    ReplyDelete
  4. dili la malari

    ReplyDelete
  5. tuangamize mazalia ya umbu jamani acheni kupoteza pesa kwenye vyandarua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...