Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mtera, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Zakia Bilal, wakipunga mikono kuwaaga wananchi wa Jimbo la Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika jana eneo la Stendi ya Mabasi na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo George Simba Chawene.
Wananchi wa Kijiji cha Mloa Barabarani, Jimbo la Mtera, wakiwa na mabango wakati wakimsubiri Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuingia eneo hilo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni jana,ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Livingstone Joseph Lusinde, ambaye ni mrithi wa Malecela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Bro Michuzi nasikia Dr Bilali kuna mahali last week or this week alikosa watu wa kuwahutubia kwenye mkutano wake. Hivi ilikuaje? mbona hutuhabarishi kuhusu hilo? Tuna hamu ya kujua nini chanzo.Msaada tutani tafadhali

    Mdau Mbezi Loius

    ReplyDelete
  2. hiyo picha ya mwisho sina mbavu

    ReplyDelete
  3. Picha ya mwisho hao ndio wanaotambulisha "mtanzania wa kawaida". Shida kwao ni kama ukoo, pigia kura CCM wazidi kuwa na shida. Kama kumburuza mlevi vile.

    ReplyDelete
  4. Check walivyo simama na mbango..then mtapata nini?
    Nina uhakika hapo kama hawajapewa buku buku tu, basi ubwabwa wa bure tu,

    RIP Tsnzania

    ReplyDelete
  5. We anym wa kwnza mbona unambeep michuzi.
    Michuzi hawezi toa hizo weweeee , humjui ankal ana damu ya kijani nini!

    ReplyDelete
  6. Hivi jamani Mhe. Balali mimi naona bora tu asingingia kwenye huu uchaguzi, umri wake umeenda sana jamani....angepumzika tu. Hata hivyo namtakia kila la heri ila tu namuonea huruma umri wake umeenda sana. Hivi CCM ni chama cha Wazee tu?

    ReplyDelete
  7. mbona jamaa wakati wote yuko FULL TINTED !? tutapataje hisia zake!? huyu bwana bila shaka hii post kaburuzwa tu, mwenyewe alikua napo anapotaka. Ankal nistiri hii moja tu uitoe basi ! au?
    Mzee wa Kengeja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...