Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wahadhara wa kampeni, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini Musoma
Mgombea urais wa Tanzaia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akikumbatiana na mbunge wa zamani wa Musoma kupitia CCM, Paul Ndobo, mara baada ya mkutano wa kampeni za mgombea huyo mjini Musoma .Mgombea ubunge katika jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Vincent Nyerere, akihutubia katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini humo .Mgombea wa ubunge katika jimbo la Maswa Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Musoma, katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzaia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi MukendoVijana wa kikosi cha ulinzi cha Red Brigade wakisindikiza gari lililombeba mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya mkutano wake wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini Musoma .picha na Joseph Senga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ni bora angekuwa Rais kweli, lakini ndiyo hivyo tena, CCM lazima wataiba kura tu...Duuh bora ujitahidi upate angalau Wabunge wengi tu...CCM Kweli mngetuonea huruma mkapumzike tu, kweli hatuwataki...Hakuna jipya.

    ReplyDelete
  2. hakika oktoba 31 kila goti litapigwa.

    ReplyDelete
  3. CHADEMA IKIPATA KURA MOJA HIYO OCT 31 BASI ITAKUWA NI YA KWANGU, JAMANI TUJITOKEZE KUPIGA KURA UMEFIKA WAKATI WA KUTOA SAUTI ZETU KUPITIA MASANDUKU YA KURA.

    Ninakushangaa sana michuzi kila nitoapo comment zangu huzipost. hivi unajua dhana nzima ya uhuru wa kujieleza bila kuathiri haki ya mwingine?. ktk waandishi wa habari Wewe una athiri sana status yako kipindi hiki

    ReplyDelete
  4. ipo wapi habari ya watu waliopigwa risasi na polisi huko mwanzo nusura wafe?!? wamelazwa bugando hospitali? hizi habari za wagombea sio muhimu kuliko uhai wa raia wa tz

    ReplyDelete
  5. Haki ya nani Michuzi siku utakayo weka picha za kampeni za Lipumba wa CUF nitakupa zawadi! wewe ni Chadema na CCM tuu unaboa!

    ReplyDelete
  6. mbona hapa hakuna watoto wa shule kama kwenye kampeni za ccm? ninaona watu wazima tu.

    ReplyDelete
  7. yaani mwaka huu mpaka kieleweke, tumechokaaa!

    ReplyDelete
  8. kweli mwaka huu chadema watawatoa ulimi ccm kwa mpango huu unavyoonekana hali ni mbaya kwa upande wa ccm pamoja na kujaribu kumchafua huyu jamaa lkn bado anakubalika kwa watu sasa kazi kwa wananchi kuamua yupi mkweli yupi mwongo ila ukweli ni kwamba tumechoshwa na ahadi hewa za ccm bora tujaribu chadema mbona kenya waliweza baada ya kuwapa wapinzani hata sisi naamini tunaweza tuache woga watz lazima tuamue kutetea haki yetu ya msingi kwakuwachagua viongozi bora wanaojali maslai ya taifa kwanza

    ReplyDelete
  9. kampeni za CCM zimejaa kina mama, na hao ndio wapiga kura. Vijana mara nyingi wanakuaga mashabiki tuu, si mnakumbuka campeni za CUF za miaka ya nyuma!? Vijana kibao, lakini mwishowe hamna kitu

    ReplyDelete
  10. huyu jamaa anulizia watoto kwenye mkutano wa chadema ha!ha!ha!chadema tunawapa watu sera ndio maana wanaamua kuacha shughuli zao nakuja kusikiliza sera zetu

    ReplyDelete
  11. We anonymous hapo juu inaonekana hujamsoma bado michuzi, ukiweka jina anaminya, jana nilishangaa kuna habari imepita ya mgombea mmoja wa ubunge, nikasema anayofanya na kuweka jina yani nikaponda akaminya, nikatuma tena kivingine nikaweka jina akaminya ndio nikajua ahaa ukiweka jina la mtu anaminya

    ReplyDelete
  12. laiti mwaka huu ndio ungekuwa 2015 tayari slaa angekuwa rais wangu ila kwa sasa najua mkwere hata taka kukubali kukatisha kale katabia walikojiwekea ka vipindi viwili viwili na ukizingatia mkwere bado hajakamilisha recod yake ya kuzunguka dunia bado hajaenda brazil na canada kwa mujibu wa recod zangu

    ReplyDelete
  13. Hakuna kitu hapo, mnajidanganya na kujipa moyo, eti Chadema watashinda mawee! Watu wanafuata helikopta na wasanii basi. Kampeni zote huwa zinafanywa na wajumbe wa nyumba kumi kumi sio viongozi wakuu wanaopita mara moja. Tena huko Musoma ambako ndio ngome ya Chadema hakuna kitu kabisa mwaka huu mmeshemsha vibaya sana ubunge utakwenda kwa CUF na kura za urais namba 1 ni JK. Mkiambiwa ni ubishi mliambiwa zamani muimarishe chama kuanzia ngazi ya shina basi angalau ngazi ya Tawi wapii mmeng'ang'ania kula pesa na vimada kwenye mahoteli Dar, mtavuna mlichopanda.

    Wenzenu wana jumuia sijui ya kinamama, wazazi, vijana, sijui chipiukizi, wajumbe wa nyumba kumi kumi, mtashindana nao vipi? Kama mnataka kushinda shurti muache starehe mujiandae! eehee shauri yenu na ubishi wenu! Basi hapo mkiona picha mnajidanganya ooh tumeshinda, yote kutafuta sababu sizizo na msingi za kutaka kuleta fujo tu baada ya matokeo wakati ukweli ni kwamba HELIKOPTA ikiondoka watu wanatawanyika!

    ReplyDelete
  14. kwa hiyo helkopta ya ccm inakuwaje?

    ReplyDelete
  15. We unayejiita anonymous acha zako zipi huna hata aibu toa constructive ideas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...