Kaka Issa,
EID MUBARAQ,
Hivi karibuni wananchi wa Taifa la Zanzibar walipiga kura kwa umoja wao na kukubali kuwa taifa lao limeridhia serikali ya muungano wa vyama tofauti kwa kifupi (serikali ya mseto). Ni hatua ya kupongezwa sana na ya kijasiri sana kwa Taifa hilo la watu wa Zanzibar.
Mimi kwa upande wangu nina swali moja ama maswali kidogo kwenye kichwa changu na ningeomba Jamii inasaidie kunielimisha kidogo.
Uelewa wangu mdogo ni kuwa Rais Wa serikali ya mapinduzi Zanzibar au wa Taifa la Zanzibar huwa anakuwa ni Waziri ama anajumuishwa kama Waziri kwenye serikali ya muungano Hivyo kupata fursa ya kushiriki kama mjumbe wa baraza la mawaziri la Serikali ya muungano Chini ya Mkuu wa Serikali ya Muungano Ambaye ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar yaani Tanzania.
Kwa hostoria fupi tu ni kuwa hadi sasa hivi utawala wa Nchi hizi mbili yaani Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) zimekuwa zikitawaliwa na chama kimoja nikiwa na maana CCM kwa pande zote mbili za muungano
Swali langu linakuja hapa;
Je kama CUF ikishinda uchaguzi kule Zanzibar Mwaka huu 2010 na kushika hatamu za uongozi na huku Tanganyika CCM ikashinda kwa kishindo hatamu za uongozi ni sheria gani au katiba inasemaje juu ya utawala wa vyama tofauti katika muungano wa mataifa yetu haya mawili ndani ya serikali ya muungano?
kwa wenzetu wa Taifa la Zanzibar Wameshabadilisha katiba ili Serikali ya mseto inawezekana Je kwenye Katiba ya Muungano nayo inasemaje? au upande wa Tanganyika unasemaje?
Nafasi ya Rais wa Zanzibar inakuwa ipi kwenye serikali ya muungano tukizingatia kuwa Kila upande wa Muungano kuna chama tofauti kilichopewa dhamana ya kuongoza Dola kwa umri wa miaka 5. Je ataweza kukaimu Urais wa muungano pale ambapo imebidi ilhali yeye ni wa chama kingine na sio chama kilichopewa dhamana kubwa? Katiba yetu ya muungano inasemaje hapa? au Sheria gani itatumika?
na Mwisho kabisa ni je, haki waliyoipata wenzetu wa Taifa la Zanzibar na sie wa Taifa la Tanganyika tunakuwa tumeipata Sawa (lakini bila ya kupiga kura) au la?.
Wadau wazingatie kuwa nimetumia maneno Taifa sana maana hivi karibuni ndugu Zetu Wamesisitiza Juu ya UTAIFA wao ndani ya muungano.
Nawakilisha kaka Issa nipate majibu Ili tuendeleze muungano wa nchi zetu na taifa Letu kwa ujumla.
Mungu ibariki Tanganyika & Zanzibir (TANZANIA)
wako:
BOSS

Tanzania haikuongozwa na chama kimoja tu toka iundwe. Toka mwaka 1964 Tanzania ilikuwa na vymama tawala viwili, yaani TANU kwa Tanzania bara (Tanganyika) na ASP (kwa Zanzibar) hadi hapo mwaka 1977 vymama hivi viwili vilipounganishwa kuwa CCM.
ReplyDeleteKwa muhtasari huo hapo juu katiba ya Tanzania tayari imeishatumiwa bila ya matataizo wakati utawala wa vyama tofauti (siyo vingi!) na vilivile wakati wa chama kimoja.
Swalio lako ni zuri ila inatisha kuona vijana jinsi ambavyo elimu ya utaifa na ya kimsingi kabisa inavyopiga chenga. Hili lilitakiwa ni jambo linaloeleweka kwa kila mzalendo..
Kwanini tusiwe na serikali tatu, yaani ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano Tanzania?, kwanini Wazanzibari wawe na serikali yao tofauti na sisi watanganyika tusiwe nayetu?.
ReplyDeleteHii ishu mpaka leo mie sijaelewa imekaaje.
Swali lako zuri sana.na wewe uliyetoa maoni umechemsha hujajibu swali.muuliza anataka afahamishe muundo wa serikali utakavyokuwa..wewe unamwambia TANU na ASP. ziliendeshaje serikali hujafafanua..kama huwezi kujibu kaa kimya
ReplyDeleteAsalaam!
ReplyDeleteKwanza tumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujalia uhai na hadi sasa tunaweza kutoa hoja mbalimbali zinazoakisi mustakabali wetu.
Pili, Mtoa mada umechagiza kuleta mkanganganyiko wa kimawazo na kitaaluma ya sheria kwa sisi wote, mimi binafsi nakupongeza.
Tatu: Mjibu Mada wa Kwanza kabisa, sijui jinsia yako lakini kama niseme hivi, hapo kaka/dada yangu umepotea na upeo wako wa kutathmini swali na uelewa wa ujumla wa mambo ya "uraia" kama ulivyosherehesha wewe mwenyewe bado unakupiga chenga, tafadhali ebu chukua muda na jaribu kupitia hoja ya ndugu yetu kwa kusoma between lines.
Nne; hoja hii ni pevu na imekuwa ikileta mijadala mingi. Ukweli wa jambo hili ni kwamba kwa vyovyote vile mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar yameleta uhalisia wa namna tunavyoweza sasa kuwa na muungano mzuri na wenye Hadidu za rejea Shirikishi. Kwa Mtazamo huu, bado Katiba yetu ya JMT haiwezi ku-accomodate mabadiliko ya kimsingi na makubwa yaliyotokea Zanzibar hivi karibuni. Hapo siku za usoni kama hali ikiwa hivi tutazamie mkanganyiko wa tafsiri na maamuzi yenye kukinzana kimuundo na kimantiki.
Tano: Nadhani kwa Mtazamo wangu, inawezekana wanazuoni wakasema kwamba sio rahisi kwa Katiba kubeba kila chembe ya hoja na hisia, na Ndio maana kama tunakumuka hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema( katika moja ya hotuba zake za mwishomwisho) kwamba,Rais atakayechagulia ataapishwa( kwa mujibu wa katiba) kwa kufuatana na dini yake...kama mkristo atapewa Biblia..na kama Muislam basi atakamata Quran... na akasema haijawahi kutokea mtu asiye na imani kati ya hizi ( ambazo ndizo zimo kwenye katiba) akawa raisi. Kwahiyo Nyerere alisema hivi, Ikitokea tukapata mtu/Rais wa namna hiyo, basi TUTATAFUTA UTARATIBU wa kumuapisha kwa mujibu wa imani yake...
Hapa nachotaka kueleza ni kwamba, hoja zako zote zina mantiki na ukweli, njia pekee ya kuaccomodate hoja hizi ni kwa kubadilisha Katiba. Lakini hili si jambo jepesi hasa kwa kuzingatia political will ya viongozi wetu na woga uliojengeka...lakini kama ikitokea Zanzibar kukawa na chama Pinzani(CUF) basi inshaalah kwa maneno na busara za mwalimu...UTARATIBU UTATAFUTWA ili rais huyo aweze kuaccomodate priviledges zote na fursa zilizopo kwa yeye kuwa kiongozi halali wa upande mwingine wa Muungano.
Saba: Kwa kweli TUNAHITAJI KUBADILIKA na Hatuna namna nyingine ya sasa KUKUBALI YAISHE na tusonge mbele.. MABADILIKO YA KATIBA ya aidha utambuzi wa uwepo wa Tanganyika ama mfumo shirikishi wa Muungano ni Lazima na hatuna cha kusubiri..wakati ulishafika tokea mwanzoni mwa miaka ya 90'. Tumechelewa na watanzania hatuwezi tena kusubiri. TUSONGE MBELE.
Nane: Mjibu Mada wa kwanza..Acha UTOTO na Eurocentrism......
Asalaam!

Tulikuwa katika moja ya mafunzo yetu ya kiskauti msituni. Kukaletwa na kamba ambayo ilikuwa na kifundo ambacho kwa weli kwa jinsi kilivyofdungwa ilikuwa vigumu mnno kkukifungua. Na tuliambiwa tufungue kupitia kifundo. Mwenzetu mmoja alijaribu sana kukifungua baada ya kila mmoja wetu kujaribu kufungua bila mafanikio. Ilipomshinda, aliamua kukata kile kifundo kwa kisu.
ReplyDeleteMimi nadhani ugumu ulioko katika swali lako, ni kwa vile umeona hatari iliyowekwa kwenye kifundo, isije ikawa umewekwa mtego ili hatimaye kitumike kisu kukata kamba ili kuweza kuifungua.
Wewe unahisi nini?????
Mtoa maoni.
swali limejibiwa muundo kama huwo wa ASP na viongozi wa Zanzibar tayari wameshaelekea mafunzoni UK kuangalia jinsi gani serikali ya mseto itaendeshwa.UK serikali imeundwa na Torres Na Conservative na uk pia ni muungano ikiwemo Nothern ireland na wales,Ijapo kua isiyokua na elimu itaibuka tu humu ndani kusema usifananishe UK NA TANZANIA sasa UK WANA MIGUU MITATU MITATU?
ReplyDelete