HOTUBA YA MGENI RASMI, MHE. DKT. SALIM AHMED SALIM WAZIRI MKUU MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MJUMBE WA JOPO LA WATU WENYE BUSARA LA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UOMJA WA AFRIKA PIA MJUMBE WA BARAZA LA USHAURI LA UMOJA WA AFRIKA LA MWAKA WA AMANI NA USALAMA WAKATI WA MAADHIMISHO YA MWAKA WA AMANI NA USALAMA BARANI AFRIKA DAR ES SALAAM, TANZANIA
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
Mhe. Said Meck Sadiq, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Waheshimiwa Viongozi mbali mbali wa dini na serikali;
Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa;
Mabibi na Mabwana,
Nashukuru kwa fursa hii ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho haya ya mwaka wa Amani na Usalama barani Afrika. Maadhimisho ambayo yanafanyika katika nchi mbalimbali barani mwetu.
Kwa takriban miongo mitatu hivi sasa Umoja wa Mataifa umekuwa ukiadhimisha siku ya amani duniani. Hii inafuatia Azimio la Baraza Kuu la Umoja huo la mwaka 1981 ambalo liliamuru kuchaguliwa siku maalumu ya kuadhimisha juhudi za upatikanaji wa amani duniani kila mwaka na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1982. Afrika kama sehemu ya jamii ya kimataifa imekuwa ikiungana na Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku hii muhimu.
Amani ni msingi wa maendeleo na hivyo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani. Bila amani, nchi haiwezi kufanya shughuli za maendeleo. Hata pale ambapo maendeleo yameshapatikana, huweza kuvurugwa endapo amani itatoweka katika nchi.
Leo tunaadhimisha kilele cha Mwaka wa Amani Barani Afrika. Tunaadhimisha mwaka huu kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.
Tarehe 31 Agosti, 2009, Wakuu wa Nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mmoja wao, walikutana Tripoli, Libya, kwa Mkutano wao maalum ambao ulijadili agenda moja tu muhimu.
Nayo ni kuhusu Migogoro Barani Afrika. Viongozi wetu wakiwa na nia ya kutaka kuona watu wote barani Afrika wakiishi kwa amani na uslama, ikiwa ni pamoja na vizazi vinavyokuja, walipitisha Azimio la Tripoli lililoazimia kuwa mwaka 2010 uwe Mwaka wa Amani na Usalama Barani Afrika. Kauli mbiu ya mwaka huu wa amani barani Afrika ni “MAKE PEACE HAPPEN” au kwa lugha yetu ya Kiswahili, “Fanya Amani Iwepo”.
Lengo likiwa ni kuongeza msukumo katika jitihada za kuleta na kudumisha amani.
kwa muendelezo wa Hotuba hiii
BOFYA HAPA

Nasikitika sana kuhusu mtu huyu kaitumikia taifa letu miaka na miaka mtu mtiivu kwa nchi yake, huu uchaguzi na makampeni yote haya ya kufanya gasia na kupoteza pesa ni bure tu, wote ni waongo hao kila mmoja anataka kutajirika wanatoa ahadi wakishapata uraisi au ubunge hamna lolote wanalotufanyia sisi wananchi wanatusahau tunabaki na umasikini wetu, mimi kwa mtazamo wangu huyu ni katika watu best hapa TZ kuchaguliwa kuwa Raisi wa nchi yetu hii nzuri yenye amani na ukimya huyu ni mtu mwenye kumuogopa mungu wake, ataendesha nchi vizuri na kwa haki inavyotakiwa kwa wananchi wa TZ, swali langu kwa nini hachaguliwi kuwa Raisi..!!?? namuombea kila kheri na maisha mema daima.
ReplyDelete2 thumbs up kwa anon wa 07:08am. Dr. Salim angepewa nafasi ya kuongoza nchi hii tungewagalagaza hata wasausi afrika. You gotta love this man....his style, leadership, credentials. I tell you, mataifa kibao wange wish angekuwa raia wao ili agombee kuwaongoza.
ReplyDeleteGod Bless you Dr. S.A Salim, asante kwa kuitumikia Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.
PS. Gen. COLLIN POWELL GOT NOTHING ON YOU!
Namuunga mkono mdau aliyepita. Kuna haja ya Dr. Salim kugombe Urais wa Tanzania 2015. Nina amini zile fitina na mikasa ya 2000 zmeisha. Zanzibar kuna maelewano na mahusiano mazuri ya kisiasa hivyo hatuna budi kumpa Dr. nafasi ya kuongoza na hivyo tutafanya haki. Naamini JK akiamua kumuunga mkono atapita kwani yeye amaemaliza muda wake hivyo ni vyema akamuunga mkono Dk. Salim. 2015 ili tupate kiongozi saaafi.
ReplyDeleteDr. Salim apewe fursa mwaka 2015 agombee. JK muunge mkono kuondoa machungu ya 2000. Nani kama Salim kwa sasa?
ReplyDelete