Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli akitoa heshima za mwisho wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Dk. Ernest Mashimba aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza kwa Mazishi katika Kijiji cha Ngudu wilayani Kwimba.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba nyumbani kwake mtaa wa Ursino, Regent Estate, Dar es Salaam.
Mke wa aliekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali Marehemu Ernest Mashimba mama Rose Ernest akisaidiwa na ndugu wakati alipopita mbele ya jeneza la marehemu mume wake wakati wa kuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake jijini Dar es salaam, mwili wa Marehemu mashimba umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Ngudu Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi. Marehemu Ernest Mashimba alifariki wki iliyopita Mkoani kwenye hoteli ya Executive Inn Lushoto mkoani Tanga alikokwenda kwenye mahafali ya mtoto wake Happy Ernest aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani humo.
Mtoto wa Marehemu aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani Tanga Happy Ernest Mashimba akiuaga mwili wa marehemu baba yake kwa majonzi makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Pole sana familia. Hasa binti yake. Mungu atawapa nguvu daima

    ReplyDelete
  2. Pole sana familia. Hasa binti yake. Mungu atawapa nguvu daima

    ReplyDelete
  3. We Michuzi Muislamu gani unaweka picha za maiti??? Kafiri mkubwaaaaaa!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. the last pic,namfeel huyo binti.i have been thru the same situation,sisi watoto wa kike tupo so close na baba zetu.masikini,pole sana familia ya Dr.Mashimba,may his soul RIP,pia mungu awape nguvu wanafamilia hasa watoto na mke wa marehemu.

    ReplyDelete
  5. Resptect the dead Michu! Sio vizuri kuweka picha za maiti! Privacy please!

    ReplyDelete
  6. wewe anonymous wa 3 wewe ndo kafiirrrii shetani kwani hii blog ni ya kiislamu....badala ata ya kutoa pole unaanza uuslamu wako apa....na ngoja yakukute yako tutaonaaa...

    ReplyDelete
  7. poleni sana jamani Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu sana, binti wa marehemu bado hajamaliza shule ndo wanafanya mtihani wa kumaliza shule mwezi kumi, unaposema binti yake aliyekuwa akisoma kifungilo na wakati bado yuko school haileti maana.

    ReplyDelete
  8. Mungu awape nguvu wafiwa katika kipindi hiki kigumu tuko pamoja nanyi katika maombolezo na majonzi haya , pia Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  9. kwa kweli inasikitisha sana jamani hasa kwa kabinti kake mungu amtie nguvu aweze fanya mitihani salama nahisi anapata maumivu makali sana moyoni coz anasema kama baba asingekuja kwenye graduation pengine asingefariki kazi za shetani hizi jamaniNa wewe mtoa maoni unayesema kaweka picha ya maiti hapo kama dini yako hairuhusu kaa kimya usilete mambo yako ya udinilisation kwenye mambo kama haya kama kwenu hairusu kwetu inakubalika

    ReplyDelete
  10. Mtu njinga utanjua katika kufikiri kwake,nyie waislaim wenye udini katika kazi za watu hebu tuondolee ujinga kafiri mwenyewe kafungue global ya waislam usionyeshe matukio.ningekuona wewe na kibalagashia chako nngekukwida hicho kichwa kisichokuwa na akili mwenzanu kabuni global yake mwataka kumtilia nuksi kafe mwenyewe

    ReplyDelete
  11. Kwa anonymous no.3 hapo juu, tofautisha Dini, Taaluma na Biashara. Mpe Mungu yaliyo ya Mungu na mpe Kaizari yaliyo ya Kaizari.

    ReplyDelete
  12. "USIHUKUMU NAWE UTAHUKUMIWA!" MUNGU PEKEE NDIE MWENYE MAMLAKA YA KUHUKUMU.

    ReplyDelete
  13. mnaona huyo wa juu alivyo anza, tukisema kwamba ustaarabu ni bora kuliko jazba wanasema, ooo sisi mnatubagua. kafiri?

    ReplyDelete
  14. we anonymous acha mambo ya kizamani ya udini kwani akiweka picha ni kitu gani mbona sisi waislam tunauridhia misiba ya wakristo,tuwe wamoja mambo ya ukafiri hapa sio mahali pake,elimika nyooo.....

    ReplyDelete
  15. Pole kwa familia ya marehemu. Mungu awape ujasiri kuipokea hali hii. Mungu ailaze pema roho ya marehemu.
    Mhh, ila wewe anonymous wa mwisho hapo juu utakuwa una matatizo na frustration zako. Kwani kila mtu anayeangalia hii blog ni Muislam? Michuzi anawakilisha ujumbe kwa jamii nzima sio waislamu tu. Mkubwa wewe...

    ReplyDelete
  16. Da wee michuzi kwanini umeweka hiyo kometi ya huyo kichaa wa sept 22, 09:27

    ReplyDelete
  17. Dah mungu amrehemu na abariki familia yake ipate nguvu.

    ReplyDelete
  18. we anonymous 09:27:00 kwani watu wanaosoma wote humu ni waislam, fikiria kabla ya kuandika acha kuleta mambo ya udini humu..

    ReplyDelete
  19. Wewe Wed Sep 22, 09:27:00 AM, marehemu jina lake ni Ernest, kwa hiyo ni clue kuwa hakuwa Mwislam, kama hurusiwi kuangalia maiti, endelea kuangalia picha nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...