Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Muheza, Mh. Joseph Mnyema, akitangaza kukitosa chama hicho na kujiunga na CCM huku JK akimsikiliza.
JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM jimbo la Pangani, Tanga, Mh. Saleh Pamba

Mgombea Urais kupitia CCM,Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Muheza mkoani Tanga leo mchana huu.
Mgombea Urais kupitia CCM,Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wananchi wa Muheza baada ya kuhutubia Mkutano wa Kampeni leo mchana.
Dr. Kikwete akiwapungia wananchi wa wilaya ya Muheza wakati akiondoka mara baada ya kuwahutubia katika mkutano wa kampeni mchana huu

Na Selina Wilson.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, ambaye pia ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Kikwete, ameendelea kuvua wafuasi toka vyama shindani katika mikutano ya kampeni zake baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Muheza, Joseph Mnyema, kukitosa chama hicho na kujiunga na CCM.

Mbele ya mamia ya wakazi wa Muheza katika mkutano wa kampeni wa CCM, Mnyema alisema amehama CHADEMA kwa kuwa kimekosa sera zenye mwelekeo.

“Kukaa upinzani ni kupoteza muda, Chama chenye mwelekeo sahihi kwa maslahi ya Watanzania ni CCM,” alisema Mnyema aliyekabidhi kadi ya CHADEMA kwa Rais Kikwete.

Akasema zaidi kuwa viongozi wa CHADEMA hawajali utu na kwamba wengi wako kwa maslahi binafsi na si kwa faida ya wananchi.

Naye Raisi Kikwete alimfahamisha mwanachama huyo mpya kuwa mateso aliyoyapata akiwa CHADEMA hatayaona CCM kwani inajali na kuthamini kero za Watanzania. Akawaasa wananchi kuungana na Mnyema kutafuta kura za CCM kwani amejiunga kipindi muafaka, wakati CCM ikiwa kazini kutafuta ushindi kwa Urais, Ubunge na Udiwani.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwaonya wanaume wanaoshiriki mapenzi na wanafunzi kuacha kufanya hivyo kwani kunaongeza umasikini kwa wananchi kushindwa kupata elimu itakayowasaidia kupiga hatua kimaendeleo.

“Nina taarifa kuna tatizo kubwa la mimba kwa wanafunzi. Naomba muache, nendeni kwa wakubwa wenzenu, acheni wasichana wasome. Hakuna maendeleo bila elimu na ukimuelimisha mwanamke umeelimisha taifa,” alisema Raisi Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka uwe unaweka na za CUF,TLP na CHADEMA,TUMEMCHOKA KUMUONA HUYO KILA SIKU MGONJWA HUYO

    ReplyDelete
  2. Unaweza kuwa unaweka dondoo za kile anachokuwa anahutubia, au wanahutubia hawa wagombea??

    Maana picha pekee hazileti picha kamili ya kinachoendelea, ukizingatia baadhi ya vyama vinakataa kushiriki kwenye midahalo!!

    Au hizi ni kampeni bubu?? Wengine wakiongea wanakatazwa kuongea.

    Vidumu vyama vyote!!

    ReplyDelete
  3. Msimlaumu Ankal, ni mtumishi wa serikali ya CCM hivyo analalia kwenye ajira.

    NB: Hata usipo-post MESSAGE SENT!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...