JK akimnadi mgombea ubunge jimbo la Isimani ambaye kapita baada ya kukosa mpinzani Mh. William Lukuvi huko Isimani leo
JK akiondoka Isimani baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni
JK akihutubia wananchi wa Isimani

Wasanii wa Tip Top Family na TMK family walikuwepo Isimani leo
Mgombea ubunge Iringa Mjini Mh. Monica Mbega akikumbatiana kwa furaha na Frederick Mwakalebela ambaye alikuwa mpinzani wake kwenye kura za maoni
Mwanasiasa mkongwe Mh. Paul Kimiti akiwa na mgombea Ubunge Iringa mjini na Frederick Mwakalebela uwanja wa Samora mjini Iringa leo. Wahasimu hao katika kura za maoni walitangaza kuvunja makundi na kumpigia upatu mama Mbega pamoja na wagombea udiwani
Pamoja na kutopitishwa katika kura za maoni Frederick Mwakalebela na wagombea wengine wa ubunge na udiwani Iringa mjini walikuwepo uwanja wa Samora kukiunga mkono CCM
Sehemu ya umati uliojitokeza Uwanja wa Samora leo kumsikiliza JK akimwaga sera
Wageni wa mataifa mbalimbali walikuwepo pia
Nyomi uwanja wa Samora
Uwanja wa Samora ulifurika
Wananchi kibao wa Iringa walijitokeza wananchi wa Iringa wakimsikiliza JK uwanja wa SamoraJK akiwasili katika kijiji cha Kilolo tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni
JK akiwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Iringa mjini Bw. Frederick Mwakalebela kwa pamoja wakiwasalimia wananchi waliofika kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa. Mwakalebela, huku akishangiliwa na maelfu ya wakazi wa mji huo, aliweka historia ya kuwa mwana CCM aliyenadiwa hadharani pamoja na kushindwa katika kura za maoni ambapo alipopanda jukwaani sio tu alitangaza kuvunja makundi bali pia kuomba wananchi wa Iringa kumpa kura mshindani wake Mh. Monica Mbega na madiwani pamoja na Rais kwenye uchaguzi mkuu Octoba 31.

JK akikumbatiana na Mwakalebela leo uwanja wa samora
Mgombea Urais chama cha CCMMh Jakaya Kikwete na Frederick Mwakalebela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. hivi huyu mwanajeshi kwenye hii misafasa ya kikwete ni nani na kwa nini anakuwepo?au jeshi nalo ni la ccm?na analipwa per diem au?na kama analipwa pesa ni za nani? ccm au serikali? mie sielewi kabisa hebu wenye majibu watuambie.

    ReplyDelete
  2. Swali la kizushi. Huyu mwanajeshi anafanya nini kwenye kampeni za CCM? I thought Army wanatakiwa wawe neutral kwenye maswala ya kama haya especially sasa hivi kwenye kampeni, au basi at least angevua uniform zake kwenye hiyo misafara. Wanaoelewa kazi ya huyu mwanajeshi, please feel us in.

    ReplyDelete
  3. CANDIDATES WAMEKUWA WAKIAHIDI WAKICHAGULIWA WATAFANYA HILI NA LILE LAKINI HAWASEMI PESA ZITATOKA WAPI KUFANYA HAYO YOTE. MBONA HAWA ZUNGUMZII HILI JAMBO LA WAWEKEZAJI KWENYE MADINI WANATUPA ONLY SIJUI 5 PERCENT AU 15 PERCENT YA FAIDA WANAYOIPATA KUTOKA MADINI YETU. NINASHANGAA KUSOMA NCHI KAMA ERITREA, BOTSWANA NA HATA CONGO KWENYE FUJO WANAPATA 40 PERCENT. TANZANIA KUNA UZEMBE GANI. JANA TU NINASOMA ETI SERIKALI INA LIFT BAN ON EXPORTS OF RAW GEMS ETI WAWAPE WAWEKEZAJI MUDA. MBONA SISI NI WARAHISI KUSHAWISHIWA NA WAZUNGU KUFANYA LOLOTE WATAKALO. TUACHE HUU UJINGA AMA TUTAKUA MASKINI MILELE. VYAMA VYA UPINZANI KWANINI PIA HAWALI ZUNGUMZII HILI ISSUE LA MADINI NA KUWAAMBIA WANANCHI WATAFANYA NINI JUU YA HUU UIZI WAKITEULIWA. DOES IT MAKE SENSE KUPELEKA VIBAKULI VYA KUOMBA KILA SIKU KWA WALE WANAOTUIBIA. HAYA MADINI TULIONAYO TANZANIA YANAWEZA KUTU PUNGUZIA OMBA OMBA.

    ReplyDelete
  4. nyie washamba unaodandia treni kwa mbele huyo ni bodyguard wa rais,sema akiwa kwenye sehemu za harakati ndo anazaa hizo uniform,akiwa sehemu nyeti ndo anavaa suti ya jeshi,na mkumbuke bodyguard wa rais ni lazima awe kanal

    ReplyDelete
  5. HIYO NYOMI siyo kumsikiliza mama mbega au JK..hiyo nyomi imeenda pale kuangalia Bongo Flava..POLE JK na CCM yako mnatumia Bunduki kumpiga inzi...du madaraka bwana...poleni sana..Ila kaa mkijua hata Zambia Kaunda ..kenya..Moi waliondolewa madarakani..SIKU ZENU ZINAHESABIKA

    ReplyDelete
  6. Huyo Mwakalebela si walidai ni mtoa rushwa? Kumbe walikuwa wanamsingizia tu. Watu bwana...

    ReplyDelete
  7. Sasa ndugu yetu Kikwete, huyu Mwakalebela ambaye mnakumbatiana kama kuku na kifaranga chake, si ndiye anashtakiwa kwa rushwa huyu? Halafu ukiambiwa unakumbatia watoaji na wala rushwa unakataa, sasa una mwenyewe uthibitisho huo.

    ReplyDelete
  8. Wewe unaowaita wenzio washamba wao wameuliza swali wape majibu basi, Watu mliosoma shule za kata mtawajua tu

    ReplyDelete
  9. Mbega hakunandiwa na kikwete au ndo unazi wa Michuzi? mbona hakuna picha akinadiwa? tumekusoma michuzi na unazi!

    ReplyDelete
  10. Tuone pia picha za mbunge wa sasa akinadiwa au makundi bado yapo japo mnaimab mmevunja.

    ReplyDelete
  11. Mume Wangu, Mikanjuni TangaSeptember 22, 2010

    Mwakalebela kuwa mvumilivu tu, JK anakutafutia WILAYA ukaongoze lakini hataki kukupeleka vijijini kwa kuwa hataweza kuonana na wewe kila mara. Subiri hapo Dar, Mbeya, Tanga au Arusha utapelekwa hivi karibuni.

    ReplyDelete
  12. wewe mchangiaji ambae unasema bodyguard wa rais ni lazima awe kanal unaongopa sio kweli bodyguard wa rais sio lazima awe kanal inatemea pia ktk kampeni sio lazima bodyguard avae uniform pia ni maamuzi tu ya muheshimiwa mwenyewe na washauri wake ila inakuwaje jk amemkumbatia mwakalebela wakati anatumuma za kuhonga pesa bana? huyo jamaa ni aje?

    ReplyDelete
  13. Personal Body Guard au Mpambe wa Rais, kwa mujibu wa taratibu na Protocal au Itifaki ikizingatiwa anatakiwa wakati wote awe nyuma ya rais na ni mtu anae mhudumia karibu...kama kubeba mkoba, makabrasha na pengine kumuekea kiti vizuri mweshimiwa akae. Pia usisahau Rais ambaye ni mgombea Urais bado ni Rais na Amir Jeshi Mkuu(Commander in Chief). Nchi zilizo endelea wameona hilo jambo sio muhimu na wameliondoa. Nchi nyingi za kiafrika wanapenda sana Itifaki hiyo, Gaddafi yeye kaweka akina mama kabisa!
    Mgosi Shemboza. Tanga.

    ReplyDelete
  14. Usijali mwakalebela kwa jinsi ninavyoona mkubwa atakusqueeze somewhere haswa kwenye vijiwilaya vipya vipya hivi

    ReplyDelete
  15. Anony 22.09 12:47 am
    Hata wewe pia hujui. Huyo jamaa kwa lugha fupi na rahisi ni ADC wa rais na sii lazima awe Colnel wa jeshi japo hicho ndio cheo cha mwisho kwa wasaidizi wa rais. Mara nyingi huanzia Meja na kuendelea mpaka colnel. Hapo alipo hana hata WEMBE. Wenye kazi zao huwa wamevaa kiraiya. Na ndio maana mara nyingi yeye huwa nyuma ya rais kwa kumbebea makabrasha na vitu vingine. Wazee wa kazi huwa pembeni kidooogo. Yeye ni nembo ya taifa kama rais anapokuwa akipeperusha bendera awapo garini. Kwa kifupi kwakuwa Rais bado yupo madarakani kwa mujibu wa katiba, nihaki yake bado kulindwa na kuwa na nyenzo zote za kirais akiwepo huyo bwana.

    ReplyDelete
  16. Ndugu zetu Rais JK na W Lukuvi, Sisi wana-Isimani tutaendelea na kampeni ya kuhakikisha kuwa kila mwana-Isimani anajitokeza kuwapigia kura siku ya uchaguzi Oktoba mwaka huu hasa tukizingatia kuwa ni CCM pekee ndicho chama kinachoweza kuwaunganisha Watanzania wa makabila, rangi na dini zote TZ. Wana-CCM tusilegeze kamba, umoja wa TZ ni muhimu sana sana. Kidumu CCM. Mungu ibariki Isimani, Iringa, Tanzania na CCM. Amen. J. Mtasiwa.

    ReplyDelete
  17. KUMBUKENI KIKWETE NI RAISI WA TANZANIA NA HUYO MWANAJESHI NI YULE YULE MNAEMUONAGA AKIWANAE HATA NEW YORK AMA KOKOTE DUNIANI RAISI ANAPOKWENDA KWA ZIARA ZAKE ZA KIKAZI, AMEVAA MAGWANDA KWAKUWA YUKO KAZINI KWENYE KAZI YA KULITUMIKIA TAIFA(KUMLINDA RAISI WETU)NI KAMA YUKO VITANI.

    ReplyDelete
  18. KUULIZA SI UJINGA....Hivi NYOMI manake nini?

    ReplyDelete
  19. UCHAMBUZI WA PICHA,
    Mwakalebela & JK ameonekana mara 3
    Mwakalebela & Monica.............2
    Kuwasili JK......................2
    Kunadi Mgombea JK&Lukuvi.........1
    Mwakalebela & Wife wake..........1
    Mahudhuria ya watu(Crowd)........7
    Waburudishaji (Wanamuziki).......1
    Mwakalebela appeared 6 times 35%, Mahudhurio appeared 7 times 41%, Other Pictures 4 times 24%, Hakuna picha ya kumnadi Monica Mbega! Mahudhurio na Mwakalebela ndio wamechukua nafasi kubwa. Unaweza ukatafsiri kadri upendavyo kwa mchanganuo huo!
    Guluguja.

    ReplyDelete
  20. NA yule mwenye tumbo kama pakacha ni nani

    ReplyDelete
  21. nshimimana aka dumisaneSeptember 22, 2010

    watu wa CHADEMA bwana, yaani badala ya kusikiliza policies wao wanangalia nani amekuja mkutanoni!?

    yuko mjeshi hapo, anadili na maslahi ya Taifa tu, ndio maana siku ya kuapishwa rais Mpya, huyo jamaa anahama kutoka nyuma ya rais wa zamani kwenda kwa Rais mpya.

    habari ndo iyo, sijui mnataka nini tena!?

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  22. Wewe any.wa 22/09/ 12:47 unamkosoa mwenzio kwamba hajui kumbe wewe ndio hujui,ni kweli huyo ni mwanajeshi ni mpambe wa Rais na ADC ni huyo bwana mwenye kaunda suti.

    ReplyDelete
  23. Jamni huyo sio Bodigadi wa Raisi. Huyu anaitwa Mpambe wa Raisi au kwa kiingereza ni Aide de camp (ADC). Yaani kazi yake ni kumsaidia Raisi kushika vitu vyake, kwa mfano hotuba, zawadi anazopewa Raisi etc. Baiscally ni messenger wa Raisi, hana kazi ingine yeyote zaidi ya hiyo.

    ReplyDelete
  24. Mimi nina swali: Hivi kuwa mwana CCM lazima uvae haya mavazi ya KIJANI na NJANO? Sikumbuki wakati wa TANU na AFRO SHIRAZI na hata mwanzoni mwa CCM kama hiyo ilikuwa njia ya kuonyesha UZALENDO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...