NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
KAMPUNI ya Borodino kutoka nchini Urusi ya uwekezaji wa umeme imetia saini na Serikali ya Tanzania mkataba wa mradi wa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji wenye uwezo wa kuzalisha 222 MV wenye thamani ya dola za Marekani milioni 700.
Makubaliano ya mkataba huo, yalitiwa saini jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Razmik Tarverdyan katika ukumbi wa mkukutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Mradi huo unaojengwa katika eneo la Rumakali ,mkoani Iringa unatarajiwa kukamilika mwaka 2018.Akizungumzia kuhusu jijitahada za Serikali katika masuala ya umeme, Katibu Mkuu huyo, Jairo alisema wizara yake itahakikisha kuwa Tanzania haitarudi nyuma katika masuala ya nishati hiyo ili iweze kuwa chanzo kikuu cha usambazaji wa umeme kwa Afrika Mashariki na ya Kati.
“Tunataka tuondokane na mgawo wa umeme na kuwa na umeme wa kutosha ambao hutasafirishwa nchi za jirani,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo Jairo. Huku akiongeza kuwa hawatarajii kuwa na mgawo wa umeme wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Katibu Mkuu huyo alisema vyanzo vya umeme vitaendelezwa mfano vya maji ili kuifanya Tanzania iwe na umeme wa uhakika, tulivu na safi wenye bei nafuu.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Tarverdyan alisema mradi huo ni mkubwa katika uwekezaji wa nishati hiyo katika Afrika Mashariki, hivyo wamewekeza fedha hizo ili kubadilisha maisha ya Watanzania hususan walio kwenye eneo hilo .
Mahitaji halisi ya umeme nchini ni MW 897 wakati uzalishaji wa sasa ni zaidi ya MW 600.

Jamani hebu mnijuze pengine ufundi mchundo niliousomea mwaka 47 umepitwa na wakati!!!
ReplyDeleteHapo juu twasoma wawekezaji wanajenga mtambo utakaotoa umeme wa nguvu ya 222MV, hivyo ni vipimo gani?
Au mwandishi akimaanisha 222MW(Mega watts)?
Kulingana na ukweli wa kubadilika kwa hali ya anga, bado tunawekeza kwenye hiyo mitambo ya maji!
ReplyDeleteKwa nini tusiwekeze kwenye nuklia (serikali tayari imekubali matumizi ya uranium kwa amani), mionzi ya jua au upepo?
tanzania bwana project kama hizi ndogo sana na i am sure tuna ma engineer wengi sana wanaoweza kufanya vitu kama hivi,umeme wa maji pia mnawaita watu wa nje shame on u,there's none special hapo umeme wa maji ni kama dynamo ya baiskeli tu,cement mnayo nunueni turbines na vitu vingine tu hapo muwaite vijana wenye ujuzi muone kama kazi haitafanyika hata walioko nje wakisikia kuna mpango kama huo wa kujenga kituo cha umeme watu watakuja wenye uchungu na nchi na kupenda maendeleo.huo mkataba kuna mkono wa mtu hapo hata hivyo isitoshe tumetumia umeme wa maji toka enzi hizo na hatukuona manufaa yeyote zaidi ya maumivu,haki ya Mungu bora unyimwe yote kuliko akili,tuna uwezo wa kuzalisha umeme wenyewe bila hata kumuita mtu yeyote,hembu fikirieni jua tulilobarikiwa,upepo wa kutosha yaani mmeshindwa kuvitumia vyoote hivyo...haya kuleni tu maana hapo baadae utasikia sijui hilo jina la kampuni ni la mtoto sijui wa kingu...sijui lowa...,tanzania nimeichoka na sirudi ng'ooo huko,kaeni na giza lenu.
ReplyDeleteNakubaliana na wadau wote hapo juu hii ni aibu kubwa sana kwa serikali yetu hatuwezi kuwa tunarudi nyuma kila siku wakati wenzetu wanakwenda mbele ukiangalia vizuri miradi kama hii inakuwa haina masoko kwenye dunia za kwanza na pili ila sis ndio wa kwanza kuchukua huu utalaamu uliopitwa na wakati kweli hata ukiwachukua vijana wa cSido watakutengenezea huo umeme.Mimi sielewi hii mikataba inagawiwa tu bila ya kungalia wapi tunakwenda jamani inatia aibu hata huyo mzungu anacheka tui kwani akimaliza yeye kula pesa yetu anamleta ndugu yake. Mimi naona sasa inabidi serikali iwajibishwe kwa kuwapa wananci sauti ya kuamua tunavyotaka tuondokane na ukoloni mambo leo.
ReplyDeleteUmm. Hii kampuni mbona siipati kwenye Google? Au ndio mambo yale yale ya fly by night power companies (i.e. Richmond)?
ReplyDeleteNimekupata Magreth Kinabo.
ReplyDelete