Mr. Michuzi,
Nimekuwa nikisafiri humu nchini, lakini siku ya Ijumaa niliishiwa nguvu baada ya kukutana na ajali zaidi ya nne kati ya Tanga na Dar. Chini ya umbali wa kilomita 330 kati ya masaa 5( Tanga-Dar) nilikutana na ajali zaidi ya 4 ambapo watu 9 walifariki papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa vibaya.
Nimekuwa nikisafiri humu nchini, lakini siku ya Ijumaa niliishiwa nguvu baada ya kukutana na ajali zaidi ya nne kati ya Tanga na Dar. Chini ya umbali wa kilomita 330 kati ya masaa 5( Tanga-Dar) nilikutana na ajali zaidi ya 4 ambapo watu 9 walifariki papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa vibaya.
Mbaya zaidi ni lile la mto WAMI ambapo lori la samaki lilivamia basi la abiria na kuua watu sita. Ya pili ni mzee aliyegongwa na lori la cementi na kufariki papo hapo. Cha ajabu ni kwamba, panapotokea ajali wanaokimbilia eneo la tukio badala ya kusaidia, kwanza wanakimbilia kupora majeruhi na waliofariki.
Hizi picha nilizuchukua mwenyewe maeneo ya tukio, zote zikiwa chini ya dakika tano baada ya ajali. Ajali zetu za aina hii zitaisha lini, chanzo ni nini? na wangapi wanakufa kila siku? Ufumbuzi utapatikanaje?
John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com
John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com
I really wonder what the leaders of our country are thinking when our poople are dying like animals and they are busy with the elections.It clears shows the leadership in tanzania. Why are we voting?
ReplyDeletewee anony wa kwanza, why are you blaming the leaders. Hao madereva wanaosababisha ajali sio kama hawana leseni au hawajui kuendesha hayo magari. Uzembe ni wa madereva na sio kiongozi wa Tanzania. Madereva wanaposababisha ajali, sheria inakuwepo na huwa wanasomewa mashtaka na mwisho kupewa kifungo. Sasa sijui hapo kiongozi anaingiaje. Tuache kulalamika kama wanawake bwana,cha msingi ni watu wenyewe yani madereva kuwa makini. Chanzo kikubwa cha ajali hizi ni madereva kuendesha magari kwa umbali mrefu bila kupumzika. By the time wanakaribia kufika wanapoenda huwa wamechoka sana. Tatizo ni kuwa nyie matajiri wenye magari mnaajiri dereva mmoja ili ubanie hela ya kumlipa. Wewe kama mtanzania umefanya nn kuzuia ajali hizi?
ReplyDeleteSalaamz wakuu.
ReplyDeleteKwanza kabisa bwana Mashaka asante kwa kutuletea picha hizi lakini ni wazi kuwa hukuwa kwenye ajali hizi baada ya dakika tano au kumi za mwanzo. Hii inaonesha una "Agenda" zako za siri different from just road accidents. Tuyaache hayo!!
Kuhusu hizi ajali kuna matatizo mengine makubwa sana ambayo yanachangia kutokea kwa hizi ajali. Hizi ajali ni "after the facts" au "majuto ni mjukuu".
Moja ya kazi za serikali ni kuangalia usalama wa raia wake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha barabara ni salama, vyombo vya usafiri ni salama, sheria na wasimamizi wa sheria wanafanya kazi zao, na pia watumiaji wa barabara wanajua haki na wajibu wao. Serikali ya Tanzania imeshindwa na kamwe haitaweza kufanya hili.
Leseni za kuendesha magari hazina maana yeyote kwa sababu kuna mamilioni ya watu ambao hawana sifa za kuwa na leseni, lakini wana class "C" na sio wale wachache ambao ni watoto wa vigogo, bali kila mwenye Shilingi 50,000 ya ziada.
Nini kifanyike:
Kwa sababu serikali imeshindwa kuwa-wajibisha madereva, basi wenye mabasi wawajibishwe.
Kwa mfano: Kama basi la Sai Baba likipata ajali, Kampuni ya Sai Baba inapigwa faini kubwa ikiwa ni pamoja na kulipia baadhi ya gharama za matibabu na fidia kwa wafiwa na majeruhi. Hii itawafanya wenye mabasi watafute madereva wa maana na kuaminika kwa sababu biashara zao ziko matatani.
Nna memngi ya kusema lakini naomba kuishia hapa...this is my two cents!!
Ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madreva wetu muda mwingi wanaongea na simu za mkononi akikaribia sehemu kuna trafiki ana kata simu akivuka hapo utasia oooh ukowapi?Pili wanamwendo wa kasi sana kupita kiasi sijui hizo speed gagana zimefia wapi?Labda ngoja tuone hizo leseni za kisasa zitasidiaje kupunguza ajali.Pia hizi Cheka na Jirushe ndo zinafanya madreva kuongea na simu sana...Kuwepo na adhabu kali kwa dreva akipatikana anaongea na simu ya mkoni
ReplyDeletewewe anony wa pili, fisadi mkubwa..unakandamiza wanawake, kama wewe ni mwanaume hufai kuwa mume mwema..usiwe unacoment kama unadiscriminate waliokuzaa na unaotegemea wakuzalie watoto. cha msingi hapo Madereva wawe makini, na wanaowachukulia hatua wafanye kweli. Serikali Corrupt
ReplyDeleteHuyu john mashaka kafanyiwa kitu mbaya bongo. Anadhani ujajnja wa kimarekani analeta DAR. Basi dogo karibia afe, motto wa mjini, mtoto wa mkubwa alimuagizia vitu vya mamillioni. Dola $6,000, sijui ma ipod, ipad, iphone na vingine vingi tu.akaambiwa akija dar atapewa hela cash. Alipofika dar, wajanja wakamwambia awape na baada ya siku mbili mshiko wake utakuwa tayari, basi hapo ndo machale yakamcheza kakataa. Jamaa kuona hivyo wakaishia mitini, basi mshikaji kaingia bonge la losi unaambiwa. Hawa ujanja wao wote kwa wabongo hawaoni ndani, wanaingizwa mkenge mchana
ReplyDeleteTatizo hakuna Law and Order mapka hiyo itakapokuwepo ajali zitapunguwa kiasi. Hazitaweza kupunguwa kabisa kwa sababu mbalia mabli, Akili za binadamu, magari mabovu, barabara zetu ni zinaitwa tiketi ya kifo, kwa sababu mmoja akiserereka tu kidogo anankugonga na na anweza kuwa ni dereva mzuri sana. Kwa undani zaidi kumbuka kila mwaka wanfunzi wanaandika reseach lakini huwa ni kwa ajili ya kupata vyeti na siyo kuangalia kwa undani ni jinsi gani ya kytatuwa matatizo ya barabrani au kwingine kokote. Nashukuru kwa kuzungumzia hili jambo ingekuwa vyema kama ungeanza kuwa kiongozi unatuma hizi information kila mahali ili walengwa waweze kuona kama kuna uwezekeano angalau wa kuweka matuta zaidi.
ReplyDeletenamuunga mkono mchangiaji wa pili anaewalaumu mataji kwa kuajili madereve wachache kwa umbali mrefu, dereva unkuta anachoka sana na anahitaji ajira afanyaje hilo ndio tatizo kubwa hasa linalochangia ajali nyingi sana za mabasi na malori ya mikoani
ReplyDeleteI think barabara mbovu ni chanzo kikubwa za hizi ajali, mfano wangeweza kujenga high way za two lanes each way hizi head on collisions ingekua ni historia. Mimi nimesafiri tz nilipokuwepo holiday from states nikapanda basi from Dar to Mwanza via Nairobi, trust me wakati wakurudi Dar ikabidi nipande ndege maana niliona mabasi yana overtake huku yamezima taa and i said that was it and i will never set my feet into those stupid Bus ever again.
ReplyDeleteJambo lingine wangeweka speed Camera kwenye hizo high way na kuweka penalty kubwa ya faini may be itasaidia otherwise God forbid tutaendelea kuzika ndugu zetu kila siku.
Mdau wa DMV
Mchangiaji wa pili mimi sikubaliani na kusema kuwa madereva wanaajiri dereva mmoja kwa safari ndefu. Sidhani kama cha msingi ni kuwa na madereva wengi unaweza ukawa na madereva wengi bado wakawa 'vishaa' vilevile. Kinachotakiwa na ambacho wenzetu wanafanya ni kuwa kuna masaa ambayo dereva anatakiwa aendeshe kwa siku bila kuzidisha kwani atachoka tuu. Mfano nchi kama Marekani dereva wa lori hatakiwi kuendesha zaidi ya masaa kumi kwa siku. Kwenye gari anakuwa na kitabu cha kuandika alianza kuendesha saa ngapi na tokea wapi, akisimamishwa lazima atoe hicho kwa polisi.Kama mtu ameamua kuajiri dereva mmoja basi amruhusu apumzike baada ya masaa kumi ya kendesha. Pia kuna jari nyingine zinatokea karibu kabisa na Dar sehemu kama kibaha tena mtu anatokea Dar utasema kachoka huyo? Nadhani pia elimu ndogo na kutokuwa makini 'mzaha mzaha' na kujiona una haki barabarani au kutaka kuwahi 'leo lazima nilale Dodoma kwa kimada wangu' hata kama itasababisha hatari kunachangia sana mambo haya kutokea.
ReplyDeleteMzozaji
Mimi nashangaa mnamlaumu aliyesema viongozi wa nchi wanatakiwa walaumiwe. Mimi namuunga mono kabisa kwani wao wana uwezo wa kulazimisha sheria zikasimiwa ipasavyo zaidi ya mambo ya kulaani tuu kwenye hotuba zao kuwa watu wanavunja sheria. Kiongozi wa nchi ana uwezo mkubwa sana wa kuwaita wakuu wa polisi na kuwaambia nataka muhakikishe hiki na hiki katika kupunguza ajili na awe anafuatilia. Haiwezekani leo kama kila mtu analalamika madereva wanatumia simu barabarani halafu hakuna hatua zozote zinachukuliwa. Viongozi wabebe lawama kwa wana uwezo mkubwa wa kutunga na kulazimisha sheria zifuatwe.
ReplyDeletesystem Tanzania haipo.viongozi ni matumbo yao wasimamia sheria ndo usiseme na watanzania wote ukikaa na sisi dakika mbili ndo utaamini kuwa duniani hatupo.inatia hasira inabidi ucomment kwa upole tu.
ReplyDeleteWEWE MASHAKA KAMA UNAUCHUNGU NA NCHI YETU MBONA USIRUDI NA KUGOMBEA KITI CHA URAIS AMA UBUNGE? UMEKAA HUKO USA SIJUI UNAPIGA DOMO AJARI AJARI MALA UCHUMI OH MADINI SIJIUI RUDI KWENU MSOMA USAIDIE WATU WANAKATA ROHO KILA SIKU! KAMA KWELI UNAUCHUNGU NA HII NCHI BASI GOMBEA HATA UDIWANI SIYO KUPIGA PIGA DOMO TU KAMA MAMA MJAMZITO, SAMAHANI MICHUZI KWA HII LUGHA YANGU LAKINI IMEBIDI NIMCHAMBE JOHN MASHAKA ANAKOSOA SANA WAKATI HANA SOLUTION YA HAYA MATATIZO! KWANI HUKO ULAYA HAKUNA AJARI KAMA HIZI? UNABOA SANA MASHAKA.
ReplyDelete