Sandu Mpanga a.k.a Kid Bway
Hali ya mtangazji wa Redio Free Africa ya jijini Mwanza ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio za Tetemesha Records,Sandu Mpanda almaarufu kwa jina la Kid Bway, ambaye alipoteza fahamu tangu waki iliyopita ( jumnanne) baada ya kupigwa na msanii na chuma kizito kichwani (rejea hapa ), inaanza kuimarika kiasi baada ya kuzinduka na kuanza kutambua ndugu zake.

Kidbway aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando, Mwanza baada ya uchunguzi wa madaktari ilibainika kwamba fuvu lake eneo la nyuma limepasuka hivyo kusababisha kuvuja kwa damu nyingi katika ubongo na nyingine kwenye uti wa mgongo. Kulingana na hali hiyo bado madaktari wanaendelea na matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. habarii ya kusikitisha sana...

    pole sana mate...tupo pamoja kwenye sala na mwenyezi mungu atakusaidia kupona haraka.

    ni matumaini yangu aliyehusika sheria itachukua mkondo wake.

    ReplyDelete
  2. Huyo mvuta bangi aliyefanya huu unyama yuko chini ya ulinzi? Au ndo 'uchunguzi na msako mkali' unafanyika? Bwana Sandu amshukuru Mungu aliyempa uzima hata sasa, jeraha hilo ni la hali ya hatari sana katika hali ya kawaida.

    ReplyDelete
  3. Kuvuja kwa damu nyingi katika ubongo???angekufa bana,.acheni kupotosha alaiki...toeni maelezo ya kueleweka.
    GeT Well Soon Sandu!

    ReplyDelete
  4. Namwomba Mungu apone. Lakini huyo aliyempiga na chuma anastahili kushtikiwa for ATTEMPTED MURDER!

    ReplyDelete
  5. ni vile hii ni africa tu.... kama ni ulaya jamaa aliyefanya hivyo angechukua mvua kadhaa lakini utashangaa tutapigana vikumbo mtaani... mtu kama huyu hahitaji kabisa kuwa na sie he/she is a threat to the society, achukuliwe hatua awe mfano kusudi isirudiwe tena.

    Pole mgonjwa samahani nimekasirishwa tu na huyu aliyekutenda hivi manake najua bado una njia refu ya kutibiwa.

    ReplyDelete
  6. pole sana kaka, ple kwa uhasama ulofanyiwa. mungu na akupe nguvu wa huu.
    tuko pamoja sana japo tupo mbali nawe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...