Tanzania imepewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Millenium Development Goals (MDGs) 2010 : The Global Heabeat kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika maendeleo ya Elimu katika sherehe zilizofanyiaka kwenye ukumbi wa Waldorf Astoria Grand Ballroom jijini New York Septemba 19, 2010. Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea tuzo hiyo na kutoka kwa Mmoja wa wasimamizo wa shughuli hiyo na Msanii maarufu , John Schneder.
Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa, Ombeni Sefue wakiwa wameshika tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Naibu Katibu Mkua Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Intercontinental jijini New York Septemba 19, 2010. Mheshimiwa Pinda yuko New York kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalojali Maendeleo ya Millenia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Labda sijaelewa, kidedea kivipi wakati report inasema tuko nyuma, au ndio propaganda hata kama watu wanalala njaa jamani? Usibania naomba kuelimishwa tafadhali

    ReplyDelete
  2. Asante Dakta Rose kwa mitindo kutoka Afrika. Unajua kuyapangilia mapigo ya kibantu.Tanzania inawakawaka ndani ya Waldorf Astoria, sio mchezo. Sifa za kweli au mnatupaka mafuta ili mtuchune vizuri?

    ReplyDelete
  3. Michuzi nani anakutumia hizi picha za NY haraka namna hiyo?
    Mi nadhani uko kwenye kampeni mikoani kule kwenye kuku kapanda baiskeli bata kavaa raizoni,ahahaha! Au PInda mwenyewe anakutumia? LOL!

    ReplyDelete
  4. Kaka hii si zarau hii jamani? enhe? Si zarau.

    Yaani Waziri Mkuu mzima anakabiziwa zawadi na MSANII? kiprotokali iko sawa hii?

    Angekuwa Waziri Mkuu wa nchi zilizoendelea angekabiziwa zawadi na Msanii?

    Aaa jamani!?

    ReplyDelete
  5. NI KWELI DR ROSE HUWA ANAPENDEZA SANA NA NGOU ZAKE I HOPE MAMA PINDA ANGETAFUTA FUNDI MZURI WA NGUO ZAKE NAYE HUWA ANAPENDA KUVAA NGUA ZA KIAFRIKA LAKINI NAONA FUNDI WAKE ANAMWANGUSHA

    ReplyDelete
  6. KIDETEMELABUPILESeptember 21, 2010

    Hii inaitwa INFIRIORITY COMPLEX kwa waafrika wengi Wasanii ndiyo watu muhimu kwenye campaign kama hizi na zingine kama malaria na HIV PM umependeza sana kula kuku baba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...