Na Woinde Shizza,Arusha
Kocha mkuu wa Tanzania wa timu ya riadha ,Endro Boro amelalamikia uchache wa siku za mazoezi kwa timu ya taifa ambayo anaiandaa kwenda kwenye mashindano nchi india .
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii ndani ya kiwanja cha Sheikh Amri Abeid kocha huyo amesema kuwa anasikitishwa sana na uchache wa siku ambazo amepangiwa kuiandaa timu hiyo ambayo inatarajiwa kuondoka mjini hapa Septembar 24 kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya safari yao ya kwenda nchini India.
Alisema kuwa amepewa wiki tatu tu kuiandaa timu hiyo ambayo inaenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya riadha ambapo ni siku chache sana walizonazo kulingana na wachezaji wenyewe wanavyofanya mazoezi.
"Unajua kuna mazoezi mengi sana vijana hawa walitakiwa wafanye kama kufanya mazoezi ya mikuki, kufanya mazoezi ya misuli,kwenda gym na hata kukimbia na kutengeneza spidi sasa mpaka sasa wamefanya moja la kukimbi kimbia na bado hawajawa kama nilivyotaka yaani nasikitika sana "alisema Boro
Alisema kuwa anaimani kabisa kama wangekuwa wamepata muda mrefu basi wangeweza kufanya vizuri zaidi na kufanya mazoezi yao vyema kwani wachezaji wake ni wazuri .
Alisema kuwa timu yake inajumla ya wachezaji tisa ambao wametoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo manyara ,Kilimanjaro,Dodoma,Singida pamoja na mkoa wa Arusha.
Kwa upande wa Rais wa Chama cha riadha Tanzania, France John alisema kuwa vijana hawa wamejiandaa vizuri licha ya kuwa kocha wao ameulalamikia muda wa mazoezi.
"Vijana wamejianda vyema sababu kabla ya kocha huyu anaewafundisha wa taifa kuanza kuwafundishi wachezaji hawa walikuwa wameshaanza kufanya mazoezi katika vilabu vyao hivyo nasema wako vyema kabisa kama ni mapungufu ni madogo tu nanathani katika siku hizi watakuwa wamerekebika na watafanya vyema"alisema john
Alibainisha kuwa mashindano ambayo timu hii inaenda kushishiriki ni magumu sana kwani wamekutana na watu mbalimbali na wengi ila wamejiaanda vya kutosha.
Aliishukuru serekali kwa kuisaidia mchezo huu haswa katika safari hii kwani imeigaramikia wachezaji mambo mengi ikiwemo usafiri na hata malazi .
Alibainisha kuwa mashindano haya yanatarajiwa kuanza kutimua vimbi October 3 mwaka huu.
HIYO NI KINGA YA KURUDI BILA MEDALI
ReplyDeleteHtuwezi kushinda kwa kutegemea wanariadha wanaojianda kambini, wenzao wa nchi nyingine hujiandaa makwao kambini ni kwa ajili ya kurekebishana tu. Waende tu wakafanye shopingi.
ReplyDeleteHaya ndo mambo yanaongelewa kila siku kuhusu nchi yetu. Kwa nini tunaingia gharama za kupeleka watu kwenye mashindano wakati hawako tayari? Nini dhumuni la ushindani huo. Na maskini kocha mwenyewe kawambia mapema, hii si kumtaka ubaya kwamba si kocha mzuri?. Hata kama tukichukulia kuwa ni udhamini uliotumika kushiriki mashindano hayo, bado mtu mwenye mtazamo wa uharisi wa mambo, angeweza kukubaliana na offer hiyo, isipokuwa vile vile kuweza kuonyesha kuwa kutokana na muda na viwango vya wanamichezo wa fani hiyo kwa muda uliobaki usingeweza kuleta mafanikio ya matarajio yetu, na hii ni assumption tu kama kuna msamalia mwema aliyeamua kutoa mchango wake, otherwise, don't you think that we have other areas we could put this money into? Nafikiri wakati mwingine tusionyeshe kuwa tunatenda kazi kutokana na nafasi tulizonazo ilimradi tu, bila kuonyesha watu ni kwa kiwango gani cha ufanisi. Ningekuwa Mwalimu, mthibiti wa mashindano hayo ningempa "F" na ningekuwa boss wake angekabidhi ufunguo wa ofisi, maana si kingine kinachoendelea licha ya kuiabisha nchi ktk upeo wa kimataifa.
ReplyDeleteBack 2 U. Mdau skyway.
TUPO HAPA INDIA LAKINI NAONA WAMESHINDWA KUMALIZA MIUUNDO MBINU YA MICHEZO HIYO. HIVYO NI VYEMA KUTOPOTEZA PESA KUJA HAPA MAANDALIZI YAKIWA MABOVU. RUSHWA KATIKA KUTOA MIKATABA YA UJENZI IMEWANGUSHA. HAYO HAYO YAWAKINA ROSTAMISM!!!!
ReplyDelete