
Mkurugenzi wa huduma kwa mlipa kodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Protas Mmanda, akionyesha mfano wa leseni mpya za udereva, makao makuu ya TRA jijini Dar. Shoto ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa usalama barabarani, Johansen Kahatano. Habari na www.wavuti.com
Picha na Chachandu Daily blog.
Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wameanza utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji leseni za udereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kudhibiti ajali za barabarani na utoaji holela wa leseni na kudhibiti mapato ya Serikali.
Kadhalika, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani, Johansen Katahano, amesema kuwa madaraja ya leseni hizo yameongezwa kutoka 8 hadi 14. Madaraja hayo yameongezwa katika daraja A na C na yameongezwa kutokanana na uwezo wa vyombo vya moto vya madaraja husika na idadi ya abiria watakaobebwa na vyombo hivyo.
Uzinduzi wa matumizi wa leseni hiyo yatafanyika
kesho Jumatano jijini Dar.
Leseni hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za kielektroniki za mtumiaji ikiwemo idadi ya makosa aliyoyafanya akiendesha chombo cha moto, gari na pikipiki.
Leseni hizi mpya zitahitimisha matumizi ya leseni za zamani.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Protas Mmanda amewataka madereva wanaotumia leseni zao za kawaida kutokuwa na wasiwasi kwani kwa muda huu wataendelea kutumia leseni hizo kihalali na watapewa leseni mpya watakapokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuzihaishi. Watu wenye leseni za Daraja C wataanza kupata leseni hizo mara moja lakini watahitajika kupata mafunzo maalumu kwanza.
Leseni hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za kielektroniki za mtumiaji ikiwemo idadi ya makosa aliyoyafanya akiendesha chombo cha moto, gari na pikipiki.
Leseni hizi mpya zitahitimisha matumizi ya leseni za zamani.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Protas Mmanda amewataka madereva wanaotumia leseni zao za kawaida kutokuwa na wasiwasi kwani kwa muda huu wataendelea kutumia leseni hizo kihalali na watapewa leseni mpya watakapokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuzihaishi. Watu wenye leseni za Daraja C wataanza kupata leseni hizo mara moja lakini watahitajika kupata mafunzo maalumu kwanza.
ankal ungekipiga kwa karibu tukione kilivyo kama ni cha kisasa ua ndio kama kawaida mtu anaweza kutengeza feki.asante mdau wa texas
ReplyDeleteKilichonifurahisha ni kuona kijana mdogo na magorofa, atakuwa kasoma au siku hizi polisi kuna katiba maalum na majungu yameisha.
ReplyDeletemadaraja 8 hadi 15 ya nini? ndio kuengeza bureaucracy na rushwa tu. Watu watachukua leseni zisizo wafaa kwa vile either zitakua cheap au easy to get na kuzitumia kwa mambo mengine. kwanini msifanye chache tu muweze kuzicontrol na watu waweze kuspecialize vizuri?
ReplyDeleteHao wafanyakazi mlionao wa kuweza kusimamia masection yote hayo ni wapi?
GOOD NA BIG UP SANA KAMANDA MPINGA NA TRA.
ReplyDeleteKUWA NA MADARAJA NI VYEMA, KWA MFANO PIKIPIKI NA BAJAJI ZA KUBEBEA ABIRIA, JE MADEREVA WAKE WANGEPEWA LESENI CLASS "C"?
TANZANIA SASA TUNAANZA KUWA NA ELECTRONIC DATA BASE SYSTEM. BAADA YA HAPA TUHAMISHIE YALE MAFAILI YETU KULE POLISI YA MAKOSA YA JINAI NA RB KIELETRONIC PIA.
WASIWASI WANGU NI KWENYE GHARAMA ZA KUPATA LESENI . HAMJAWEKA WAZI HATUA ZA KUWEZA KUPATA LESSENI ILI KUEPUKA NA CHANGA LA MACHO NA VISHOKA.
NI MIMI KONDA MWENYE SHAHADA YA UDSM.
Engineer Afande Kahatano hongera sana kaka!
ReplyDeleteulaji mwingine kwa trafiki polisi huo umewadia.
ReplyDeletemdau wa TX kwani kuna kitu kisichoweza kufanywa feki?Bidhaa kibao unazozinunua ni feki(Bootleg)Marekani kuna Driver license fake kibao,Passport fake lukuki.Hii ni dunia ya computer kila kitu kinaweza kuwa forged.Kwa TZ itakuwa ndo balaa.
ReplyDeleteNilimsikiliza/ kumtazama huyo kamanda via itv jana- i was dissapointed kwa jinsi alivyo na kigugumizi. Sijui alipenya vipi na kuwa officer kwani hastaili. Officer, ni lazima awe na sauti kakamavu na dhabiti- not kigugumizi please. Hii ina maana kubwa; anapotoa amri na miongozo lazima isikike kwa ufasaha ili kusiwe na utata & confusion ktk utekelezaji wake.
ReplyDeleteBongo bana,tuna leseni hadi class 8
ReplyDeletewakati barabara zenyewe zinatupiga mitama.
Haya sasa nimesikia raisi ametuahidi eti atatuwekea bara bara zajuu na chini.
Nafikiri class 8 ni kwa wapita juu
tu,
ukitaka uone uhondo,
kuwa mitaa ya kimarabaruti mida
ya saa12 jioni,
alafu angalia utafika ubungosaa ngapi?.
LENGO NI NIDHAMU YA UENDESHAJI(HASWA DALADALA) NA HATIMAYE KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI ZINAZOSABABISHA VIFO VY WATANZANIA WASIO NA HATIA .wote mliotoa mawazo mko sawa eng/ kamanda naona hii itakuwa njia muafaka ya kuchuja madereva wenye rafu haswa wa daladala.kosa la kwanza faini la pili mahakamani la tatu funga leseni akatafute fani/kazi nyingine kama kweli leseni zote zitakua computerized hakuna jinsi kwa dreva asiye na nidhamu ya kuendesha atanusurika.TUNATAKA SALAMU YA OFISA WA USALAMA BARABARANI KWA DRIVER WA DALADALA IWE NIPATIE LESENI YAKO KAMA HANA YA KISASA WEKA NDANI SIKU 14 THEN MAHAKAMANI KWANI HAO NDIO WASIOKUWA NA LESENI NA WASABABISHAJI AJALI.
ReplyDeletekumbe afande ni mhandisi/engineer, ndo maana ana maua mengi mazuri begani ni vijiwe.
ReplyDeletebado mdogo utaula ulimwengu hasa.
BORA HATA MVIBADILISHE HIVYO VI DRIVING LICENCE VYENU VILIKUWA VINATIA AIBU HAKI YA MUNGU,NAKUMBUKA MARA YA KWANZA NAKUJA UK,NILIKUWA NATUMIA DRIVINGI LICENCE YA KIBONGO WAZEE WAKANIDANDIA WAKAOMBA LESENI NIKAWATOLEA LILE KARATASI LENU LA MWANZO WAKACHEKA WAKANIULIZA HII NI NINI,BILA WOGA NIKASEMA NI DRIVING LICENCE YA TANZANIA,WAKAIGEUZA MPAKA NIKACHUKIA,UZURI NILIKUWA SINA KOSA ILA NILIONDOKA NA AIBU YA KUWA NA DRVING LICENCE MBOVU DUNIANI...NAHISI HATA MALAWI WAMETUSHINDA.
ReplyDeleteHata wakikuponda kamanda, wao au baba zao hajapata ukamisha wakiwa miaka ya salasini ya umri wao.
ReplyDeletewakale chakula walale.
Mi nakufagilia afande kijana. hamna majungu wala nini.
yani nyie mnazindua wakati tayari watu weshazipata zamaniii kwa njia yetu ile ile ya mlungula dot com
ReplyDeletewee wa UK acha umbeya utaendeshaje nchi nyingine na driver license ya nchi nyingine. Hata hao waliokushika walikuonea huruma tu au walikua hawaelewi ni nini unacho....International driver license ndio unaweza kuendesha nchi nyingine na sio nchi zote ulimwengini zinazotambua hiyo leseni
ReplyDeletehata pasi za mwanzi=oni zilikuz karatasi ...kila kitu ni maendeleo na pole pole tutafika tu huko walikofika
Wameshaanza mradi huo vibaya wapi na wapi mamlaka ya mapato inasimamia usalama wa jamii kwa kutoa vitambulisho???? I just do not get it, ilitakiwa wizara ya mambo ya ndani ndio isimamie na kutoa vitambulisha na sio vinginevyo.
ReplyDelete