Habari kaka Michuzi,

Naomba uwahabarishe wadau ,Kuna matapeli wameingia nchini Tanzania ( Dar es Salaam) wanadai wao ni representatives wa T.B. Joshua wa SCOAN na Emmanueli TV. SCOAN wamekanusha kutuma representative nchini, hivyo kuweni makini. Matapeli wa aina hii wameenea duniani ambao hujipatia mali kwa jina la T.B.Joshua na Emmanuel TV.

Kwa habari zaidi angalieni Emmanuel TV au someni kwenye mtandao www.emmanueltv.com.

Asanteni na tuwe makini na hawa matapeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hao matapeli wapo wengi tu tangu maika ya 80 na 90 wazaliwa wa hapa hapa nyumbani, wewe waone tu wao wenyewe ulinganishe na waumini wao. Wengi wanatoka hata Europe wanasema wanakuja kufanya mikutani. Tafadhali Google kwanza kabla hujakwenda kwenye hiyo mikutano.Watu wamezidi kuhujumu waumini wao, tufunguke macho, kiongozi ambae neno lake ndiyo mwisho muogopeni, huyo siyo kiongozi ni tapeli tu. Na hana hata msaada kwa jamii. Anatafuta kula tu yeye na familia yake, ukiona kiongozi anmpatia kijana wake utawala kanisani ujuwe huyo ni tapeli na siyi kuongozi wa dini wa kweli, anchumia tumbo lake tu.

    ReplyDelete
  2. Tuwe makini jamani mimi ndugu yangu wakaribu amepigiwa simu na hawa matapeli.

    ReplyDelete
  3. Wewe ndie tapeli unayetaka kutangaza hiyo website kwa kutuongopea ...kuwa kuna matapeli .. michuzi na wewe hujashtuka tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...