mwendesha pikipiki akipita katika njia ya waendao kwa miguu,tena akiwa hana hata wasi wasi kana kwamba huko anakopita ni sahihi kwa chombo chake.wadau imekaaje hii??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Watu wapumbavu kama hawa ndio wananifanya nisitake kuishi Bongo...tena hapo utakuta anakupigia na honi umpishe, ingawa wewe ndo mwenye haki.

    ReplyDelete
  2. Huyo ni wa kumvua helmet unamchapa makwenzi tu.

    ReplyDelete
  3. Kwa hapa Dar, mbona vitu kama hivyo ni vya kawaida! Yaani kwa yule anayeshangaa, kinyume chake ndiye anaonekana wa ajabu! Hapa Dar na Bongo kwa ujumla msimamizi wa sheria kama hizo hayupo!!!

    ReplyDelete
  4. Hiyo ndio Bongo ya JK hamna sheria wala taratibu, na kama zipi Hazitekelezwi na kusimamiwa.
    Halafu bado tu wajinga wanataka kutoa kura zao kwa hao hao

    ReplyDelete
  5. Honi kibaao na matusi pia!!! Hawa jamaa katikati ya barabara kwao, kwenye njia za waenda kwa miguu pia kwao!!!

    ReplyDelete
  6. HAPO WADAU HATUNA LAKUSEMA,VIONGOZI MIJIHELA WANAJIGAWIA WENYEWE BADALA YAKUFANYA UTARATIBU WA KUWEKA ROAD CAMERA,JAPO HAPO DSM TU NA WALA SIO NCHI NZIMA,NA WALA HAKUNA HATA MWENYE HILO WAZO,NAPIA KUINGIA MJINI NILAZIMA WAWEKE CONJUCTION CHARGE,MOSONGAMANO UTAISHA,NAWATU WOTE WATATOSHA BARABARANI.MDAU UK.

    ReplyDelete
  7. Foleni zilivyo bongo, mwenye pikix2 na abiria wake simlaumu - tena usikute hiyo ni 'taksi' ambao wanashindaja na Bajaji.

    ReplyDelete
  8. Foleni ni kubwa mno!

    ReplyDelete
  9. Ni sawa tu anayo haki kwani barabara haipitiki imejaa maji na sisi wote hatujui haki yetu tukiwa kama walipa kodi. Kama makwenzituanzie na wana ccm ambao ndio madiwani wa jiji ambao ndio tutakaowachagua watuongoze tena kwa utendaji wao mbovu lakini sisi tunachagua chama. Tuache kulalamika hovyohovyo kwani ujinga ni wetu.

    ReplyDelete
  10. MIMI HUWA NASEMA SIKU ZOTE KUWA, MAMA WA MATATIZO YETU (WABONGO)YOOOOOTE NI UTOVU WA NIDHAMU. HATUNA NIDHAMU. UKISEMA MTU WA KUSIMAMIA SHERIA HAYUPO SI SAWA, HATA WAKIWEPO MILIONI KAMA NA WAO HAWANA NIDHAMU UNATEGEMEA NINI??!!!! LAKINI PIA HAO WASIMAMIA NIDHAMU HAWAWEZI KUWEPO KILA MAHALI. TUJIFUNZE KUWA NA NIDHAMU KWANZA HALAFU NDO TUGEUKIE KWINGINE, OTHERWISE HATUENDI KOKOTE.

    Mdau Gordon Chiggs, deslam

    ReplyDelete
  11. hatab wakiweka camera, tatizo la bongo ni enforcement of the law. Ukimkamata mtu anatoa hongo yanakwisha. Huko majuu ukikamatwa leseni yako inarecodiwa kwenye takwimu za mahakama, faini zake ni kubwa. Kosa lolote linalohusiana na chombo cha usafiri, kikiwa kinaendeshwa malipo yake yanaanzia kiasi cha shilingi laki moja kwenda juu kutegemeana na gari au pikipiki ilikuwa speed gani. Inaweza hata kufika laki tatu au nusu millioni. ( nimetumia pesa ya kitanzania) lakini hizo faini kama unaishi marekani ni dola nakama uko euruope ni europeana currency.
    sasa unajiuliza ufanye makosa halafu uipe serikali pesa au ufuate sheria. Halafu kama umekubuhu kufanya makosa unanyang'anywa leseni. Ni kitu kigumu sana kutokuwa na leseni, hasa marekani kwani leseni ndiyo kitambulisho kikuu. Siku hizi kupanda ndege wahitaji leseni na mambo chingu nzima yahitaji leseni.

    ReplyDelete
  12. Ni kwamba hapo kwenye sidewalk gari halienei, vinginevyo ungekuta magari pia yana-faulisha

    ReplyDelete
  13. nshimimana aka dumisaneSeptember 14, 2010

    Bongo wajanja tu ndo wanao peleka mkono kinywani.. huyo mshkaji anapiga honi alafu unasogea kama sio mjanja basi unadhani ni haki yake!?

    kumbe wewe ndio unakandamizwa.

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  14. This is done for being inconsiderate.Ikijitia uraia wema na kumwambia makosa yake ya kupanda tukutuku kwenye njia ya miguu,ukiwa na bahati atakufyonza au kukutukana,na ukiwa huna bahati pengine atakutia ndondi.
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  15. yani huyu baba is such a moron. Not only does he put lives of pedestrians indanger, but also himself..such a silly silly man!

    ReplyDelete
  16. MIMI NAFRIKIRI MAMLAKA ZINAZOTOA LESENI NA KIZISIMAMIA NDIO CHANZO JAMAA WA PIKIPIKI UNAKUTA ALIKUWA MKAMUA NG'OMBE ANAPANDA PIKIPIKI MOTO NO ELIMU YA CHOCHOTE BADILI LESENI MWENDESHA PIKIPIKI APIMWE AKILI NDIO AINGIE ROAD WANASUMBUA SANA

    ReplyDelete
  17. Yaani akinigusa tu, na hiyo pikipiki yake ndo atajua kama hii ni njia ya wapita kwa miguu au pikipiki!!!!!!

    Kama askari wa usalama barabari wameshindwa, hivi nyie watembea kwa miguu mnaopishana nae mmeshindwa nini kumzaba?!?!?!?!

    Dah! Natamani nikutane nae, aone kichapo chake, yan kwa mie lazima nimwanzishie, namweleza ukweli akijidai kupandisha sasa hapo ndo atajua kama popo ni mnyama au ndege

    ReplyDelete
  18. Yaani akinigusa tu, na hiyo pikipiki yake ndo atajua kama hii ni njia ya wapita kwa miguu au pikipiki!!!!!!

    Kama askari wa usalama barabari wameshindwa, hivi nyie watembea kwa miguu mnaopishana nae mmeshindwa nini kumzaba?!?!?!?!

    Dah! Natamani nikutane nae, aone kichapo chake, yan kwa mie lazima nimwanzishie, namweleza ukweli akijidai kupandisha sasa hapo ndo atajua kama popo ni mnyama au ndege

    ReplyDelete
  19. Bwana wee Ashugala
    Naona wewe ni jitu kali na shujaa na mtu aliyejaliwa nguvu. Lakini katika dunia hii utapigana na wangapi? Na siku moja utakutana na aliyejaliwa kuwa na nguvu kama wewe au kukuzidi wewe. Like a gun fighter in the westerns, one day, high noon, you will come across someone who is faster at the draw
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  20. naungana na mdau wa kwanza watu kama hao utakuta anakupigia honi sasa ukiangalia umpishe uende wapi tena na upo kwenye njia yako ya watembea kwa miguu

    bongo ukiwa mtu wa hasira kesi kila siku maana watu kama hao unakata makofi akijifanya kuzipanga unapiga vichwa 3 meno nje mchezo umeisha swain.....

    hapo wana usalama hawapo ila kwenye kusimamisha magari yasiokuwa na makosa ili kuvuta ulaji tu nakwambia huko nyumbani tutakuja kutoana roho..#@^%&*

    ReplyDelete
  21. vichwa 3 meno nje kula kona ndio hukumu ya watu kama hao kesho harudii maana ukingoja wana sheria wachukue sheria zinazotakiwa bongo watu kama hao hamna ila wapo wale wa kutembea na land cruser benz na kufakamia mihela ya walala hoi sasa hapo wataangalia matatizo madogomadogo kama hayo saa ngapi? matatizo hayatomuingizia mihela ya bure

    bongo imeoza na itazidi kuoza wanaosema bongo imeendelea kwa kuona majengo makubwa basi hajui maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...